Marekani: Mwanamke aliyepooza kwa zaidi ya Miaka 10 ajifungua, Baba wa Mtoto asakwa

Mwanamke aliyepooza kwa miaka isiyopungua 14, amejifungua mtoto na kusababisha mamlaka kufanya uchunguzi wa nani aliyempa mimba katika kituo cha kulelea wagonjwa wasiojiweza kilichopo Phoenix, Arizona nchini Marekani.

Mwanamke huyo alikuwa anatunzwa katika kituo kiitwacho Hacienda Healthcare. Lakini kitendo cha mwanamke huyo kubeba mimba ni ishara ya kufanyiwa unyanyasaji wa kingono katika kituo hiko, na kinachoshangaza zaidi ni ripoti kwamba waliokuwa wanamtunza hawakugundua kama ana mimba mpaka pale aliposhikwa na uchungu. Kwa msaada wa wauguzi, mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume tarehe 29 December, 2018 na mtoto inaripotiwa anaendelea vizuri kabisa.

Unyanyasaji wa kingono kwa mtu asiyejiweza ni kosa la jinai katika jimbo la Arizona, na msemaji wa polisi katika mji wa Phoenix aliliambia gazeti la Washington Post kwamba mamlaka zinafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Baada ya tukio hilo kutokea kituo cha Hacienda sasa kimeanzisha utaratibu wa wafanyakazi wa kiume kuingia na angalau mfanyakazi mmoja wa kike pindi wanapoingia katika vyumba vya wagonjwa wa kike.

Mpaka sasa hamna mtuhumiwa yoyote aliyekamatwa. Kwa sasa inasemekana polisi wameanza kuchukua sampo za DNA kwa wafanyakazi wanaume wote wa kituo hiko na kwa wale waliogoma kutoa sampo kwa hiyari polisi wamechukua hati ya mahakama ili kusaidia.

Source: CNN

https://edition.cnn.com/2019/01/09/us/arizona-woman-vegetative-state-gives-birth/index.html
wanaume ni watu hatari kuliko simba...
 
Haujui kitu ..bi- dada uwanaume ni shida " ndio maana unaona mpka makasisi wamekutwa na tuhuma za ubakaji huko ulaya /amerca

Hili swala sio la kulichukulia poa ujue " imagine watu wamesoma na kuelimika kisha wakaamua kumtumikia bwana " lakini wameshindwa kuishi kwenye misingi ya ustaarabu " misingi ambayo huwa ndio wanaihubiri " kwaajili ya genye tu " ...haha

Sent using Jamii Forums mobile app
Yana ukweli mchache sana hayo,..kikubwa ni kujua namna ya kujicontro tu.
Genye ni kitu simple sana.
 
Back
Top Bottom