Marekani: Mwanamke aliyepooza kwa zaidi ya Miaka 10 ajifungua, Baba wa Mtoto asakwa

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,301
Mwanamke aliyepooza kwa miaka isiyopungua 14, amejifungua mtoto na kusababisha mamlaka kufanya uchunguzi wa nani aliyempa mimba katika kituo cha kulelea wagonjwa wasiojiweza kilichopo Phoenix, Arizona nchini Marekani.

Mwanamke huyo alikuwa anatunzwa katika kituo kiitwacho Hacienda Healthcare. Lakini kitendo cha mwanamke huyo kubeba mimba ni ishara ya kufanyiwa unyanyasaji wa kingono katika kituo hiko, na kinachoshangaza zaidi ni ripoti kwamba waliokuwa wanamtunza hawakugundua kama ana mimba mpaka pale aliposhikwa na uchungu. Kwa msaada wa wauguzi, mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume tarehe 29 December, 2018 na mtoto inaripotiwa anaendelea vizuri kabisa.

Unyanyasaji wa kingono kwa mtu asiyejiweza ni kosa la jinai katika jimbo la Arizona, na msemaji wa polisi katika mji wa Phoenix aliliambia gazeti la Washington Post kwamba mamlaka zinafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Baada ya tukio hilo kutokea kituo cha Hacienda sasa kimeanzisha utaratibu wa wafanyakazi wa kiume kuingia na angalau mfanyakazi mmoja wa kike pindi wanapoingia katika vyumba vya wagonjwa wa kike.

Mpaka sasa hamna mtuhumiwa yoyote aliyekamatwa. Kwa sasa inasemekana polisi wameanza kuchukua sampo za DNA kwa wafanyakazi wanaume wote wa kituo hiko na kwa wale waliogoma kutoa sampo kwa hiyari polisi wamechukua hati ya mahakama ili kusaidia.

Source: CNN

https://edition.cnn.com/2019/01/09/us/arizona-woman-vegetative-state-gives-birth/index.html
 
Baada ya tendo unajilaumu hivi ndio nimefanya nini!!

Joto la mwili likipanda wanaume huwa tunakuwa vichaa, kichwa cha chini ndicho kinachofanya kazi zaidi kwa wakati huo.
Hatari san mkuu, ashki ni mbaya zaidi ya mzimu.
 
Mwanamke aliyepooza kwa miaka isiyopungua 14, amejifungua mtoto na kusababisha mamlaka kufanya uchunguzi wa nani aliyempa mimba katika kituo cha kulelea wagonjwa wasiojiweza kilichopo Phoenix, Arizona nchini Marekani.

Mwanamke huyo alikuwa anatunzwa katika kituo kiitwacho Hacienda Healthcare. Lakini kitendo cha mwanamke huyo kubeba mimba ni ishara ya kufanyiwa unyanyasaji wa kingono katika kituo hiko, na kinachoshangaza zaidi ni ripoti kwamba waliokuwa wanamtunza hawakugundua kama ana mimba mpaka pale aliposhikwa na uchungu. Kwa msaada wa wauguzi, mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume tarehe 29 December, 2018 na mtoto inaripotiwa anaendelea vizuri kabisa.

Unyanyasaji wa kingono kwa mtu asiyejiweza ni kosa la jinai katika jimbo la Arizona, na msemaji wa polisi katika mji wa Phoenix aliliambia gazeti la Washington Post kwamba mamlaka zinafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Baada ya tukio hilo kutokea kituo cha Hacienda sasa kimeanzisha utaratibu wa wafanyakazi wa kiume kuingia na angalau mfanyakazi mmoja wa kike pindi wanapoingia katika vyumba vya wagonjwa wa kike.

Mpaka sasa hamna mtuhumiwa yoyote aliyekamatwa. Kwa sasa inasemekana polisi wameanza kuchukua sampo za DNA kwa wafanyakazi wanaume wote wa kituo hiko na kwa wale waliogoma kutoa sampo kwa hiyari polisi wamechukua hati ya mahakama ili kusaidia.

Source: CNN

https://edition.cnn.com/2019/01/09/us/arizona-woman-vegetative-state-gives-birth/index.html
Tunaye ndugu kwenye familia aliyetokewa na jambo kama hilo mpaka Leo watu hawaelewi baba wa mtoto wake ni nani, huu ni mwaka wa 30, binti aliyezaliwa ana maisha mazuri ajabu nahisi kama baba yake yupo anatamani kujileta anashindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom