Marekani: Mwanamke aishi na maiti ya mamake nyumbani tangu 2016

Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
572
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
572 1,000
Mwanamke mmoja jimboni Texas, Marekani amekamatwa baada ya masalio ya maiti ya mamake inayooza kugunduliwa nyumbani wanakoishi pamoja.

Polisi wanaamini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 71 alianguka mnamo 2016.

Wanatuhumu kwamba binti yake mwenye umri wa miaka 47 alishindwa kumhudumia vizuri mamake aliyefariki "siku chache baadaye" kutokana na athari ya kuanguka huko.

Masalio ya mwili wa marehemu yalipatikana kwenye sakafu ya chumba kimoja. Binti yake na mjukuu wake marehemu walilala katika chumba cha pili katika nyumba hiyo.

Mjukuu wa marehemu alikuwa na miaka 15 wakati akiishi na maiti ya bibi yake. Na kutokana na hilo, mamake ameshtakiwa kwa 'kumdhuru mtoto' wa chini ya miaka 15.

Mjukuu huyo sasa anatazamwa na jamaa zao na anapokea usaidizi kutoka kitengo cha kuwalinda watoto.

Huenda mamake akakabiliwa na hadi miaka 20 gerezani na faini ya hadi $10,000.

Polisi wanasema marehemu bibi huyo aliheshimika katika jamii kwenye eneo hilo, na alifanya kazi kama karani na mwalimu msaidizi katika mojawapo wa shule katika eneo hilo kwa miaka 35.

Alipostaafu, alikuwa akifanya kazi ya kukusanya tiketi katika sherehe za michezo huko Seguin.
 
Kasie

Kasie

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Messages
13,704
Points
2,000
Kasie

Kasie

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2013
13,704 2,000
Kabla ya kumhukumu walimpima huyo mama kama hakuwa na matatizo ya akili?

Yawezekama kweli ukamfanyia hivo Mama yako mzazi na kukaa na maiti zaidi ya mwaka mmoja...!!!??
 
busha

busha

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Messages
1,052
Points
2,000
busha

busha

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2019
1,052 2,000
maisha na ustaarabu wa wazungu wakuto tembeleana na kujuliana hali kwa ndugu na jamaa mara kwa mara kuna changamoto zake.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
113,780
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
113,780 2,000
Ulaya kila mtu kivyakwe.... No sharing... Ukizidiwa pekeyako nyumbani ukashindwa hata kupiga simu... Siku wakikukumbuka wanakuta umeoza tayari
 
A

Alfan issa

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Messages
2,126
Points
2,000
A

Alfan issa

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2015
2,126 2,000
Duuh kweli aisee! Utaoza kwel miaka mitatu
Ulaya kila mtu kivyakwe.... No sharing... Ukizidiwa pekeyako nyumbani ukashindwa hata kupiga simu... Siku wakikukumbuka wanakuta umeoza tayari
 
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
4,139
Points
2,000
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
4,139 2,000
Dah ushirikina mpaka marekani! Kweli Hali ngumu!
 

Forum statistics

Threads 1,315,687
Members 505,292
Posts 31,867,021
Top