Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wa Uganda waliohujumu Demokrasia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,783
Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo vya usafiri dhidi ya maafisa wakuu wa serikali ya Uganda ambao wanaaminika kuhusika na njama ya kuhujumu mfumo wa demokrasia nchini Uganda, wakati wa uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata ulioandaliwa Januari tarehe 14 mwaka huu.

Rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo na tume ya uchaguzi, matokeo ambayo yalipingwa vikali na mgombea mkuu wa upinzani wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi, al maarufu Boby Wine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani , Anthony Blinken

Vitendo vya maafisa wakuu wa Serikali ya Uganda vilisambaratisha mchakato wa kidemokrasia nchini humo na ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Orodha ya maafisa waliowekewa vikwazo na Marekani hata hivyo haijatolewa lakini ripoti zilizotolewa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu zimeshutumu idara za usalama na ulinzi kwa kuhusika na mauaji, utekaji nyara na kukamatwa kwa wafuasi wa upinzani wakati wa msimu wa uchaguzi mkuu nchini Uganda.

Serikali ya Uganda imekanusha madai kuwa ilihusika na utekaji nyara wa wafuasi wa upinzani.

lakini hapo jana ilikiri kuwa zaidi ya watu elfu moja walikamatwa wakati wa kipindi cha uchaguzi .

Viongozi wa upinzani nchini Uganda wamedai kuwa zaidi ya watu 360 walitekwa nyara na maafisa wa ulinzi nyakati za usiku na hadi sasa hawajulikani waliko.
 
Haya mmbo ya vikwazo mbona hayasaidii kumtia mtu adabu hata kidogo. Ndilo tatizo la wazungu, eti UN wnamfanyia jiwe kumbukizi wakati ana mamia ya maiti alizobeba mgongoni mwake aliowaua.

Ajabu hata hawa wanaojiita viongozi wa dini jana walikuwa na kumbukizi. Wamesahau maumivu aliyowapatia watu... akina Shoo eti ni askofu, pumbavu ni mjasiliadini.... ana Mke na watoto atawalisha nini
 
Back
Top Bottom