Marekani kutoshiriki Michezo ya Olimpiki ili kupinga Ukatili unaofanywa China

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Marekani haitatuma wawakilishi rasmi kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi huko Beijing. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, njia mojawapo ya kukemea ukandamizaji wa jamii ya Uyghur nchini China.

"Hakuna afisa wa Marekani au mwanadiplomasia atakayekuwepo Beijing mwezi Februari," msemaji wa White House amesema. Kwa utawala wa Marekani, ni jambo lisilowazika kufanya "kana kwamba hakuna kilichotokea" wakati "haki za binadamu zinakiukwa mara kwa mara" nchini China, hasa katika mji wa Xinjiang. Katika suala hii maalum, Jen Psaki amefkwenda mbali na kutumia neno "mauaji ya kimbari" dhidi ya watu kutoka jamii ya Uyghurs.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanadai kuwa zaidi ya watu milioni moja kutoka jamii hiyo ya Waislamu walio wachache kwa sasa wanazuiliwa katika kambi.

Kabla ya uamuzi huo kurasimishwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitishia kuchukua "hatua madhubuti" ikiwa maafisa wa Marekani wataendelea kutoa wito wa kususia michezo ya Olimpiki kwa njia ya kidiplomasia.

Wazo hilo lilikuwa likifikiriwa kwa wiki kadhaa, na mkutano wa video kati ya Joe Biden na Xi Jinping haukutosha kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Wanariadha wa Marekani hata hivyo watashiriki katika hafla hiyo ambayo itafanyika kuanzia Februari 4 hadi 20. Na bado kutakuwa na wanadiplomasia wa Marekani katika mji huo ili kuhakikisha usalama wa wajumbe wake.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imeelezea furaha yake kwamba uamuzi huu unahusu masuala ya kisiasa pekee na kwamba wanariadha wa Marekani wanaweza kutetea nafasi zao, anaripoti mwandishi wetu wa Washington, Guillaume Naudin.

Kamati ya Olimpiki ya Marekani ilipinga kujitoa kabisa kwa Marekani, ikieleza kwamba kususia michezo hiyo huko Moscow mwaka 1980 na Los Angeles mwaka 1984, katika muktadha wa Vita Baridi, kumeonyesha kwamba matumizi ya kisiasa ya matukio haya yalikuwa kosa.

Wiki iliyopita, taasisi ya wataalam ya Marekani ilichapisha ushahidi wa kuhusika kwa rais wa China mwenyewe katika kile ambacho nchi nyingi za Magharibi zinakiona kuwa mauaji ya halaiki.

RFI Swahili
 
Hawa jamaa vituko sana, wao wanavyofanya ukatili huko mashariki yakati au ndio nyani haoni mkunduwe
 
Na china wawaambie wao wa marekani kuhusu ukatili wanaofanyiwa watu weusi kule Marekani kwenye black neighborhoods na hata maeneo mengineyo. Systematic racism.

Marekani anajifanya yupo so concerned na mambo ya ndani ya mataifa ya wengine kwake aaaaaaaah hataki kuguswa.

Miaka miwili nyuma hapa Russia kupitia Nigeria na Ghana alitengeneza keyboard warriors ambao kupitia mitandao ya jamii walitumia kuongea maswala ya unyanyasaji mbali mbali wanaofanyiwa watu weusi waliopo marekani kwa kutengeneza account fake ila zenye majina na picha za raia wa Marekani.

Marekani alichanganyikiwa maana duh ile ndio mojawapo ya vitu vilichangia sana issue ya Floyd kupamba moto na kushika kasi kwenye mitandao. Marekani ile kitu ilimshitua sana hadi Homeland security wakaingia mitamboni kubaini hii nguvu inatokea wapo mbona hawa blacks wapo so organized.

Ndipo akajua kuwa Russia amelipa pesa kutengeneza vikosi mtandao ambavyo vinakuwa controlled na raia wa Nigeria na Ghana ila ambao wapo Afrika ila profile zinaonekana ni za wamarekani.

Akatuma wapelelezi na forensic journalists wakaja kufanya follow up na kuandaa exclusive docuseries zinazocover hiyo issue kwa kirefu ili kumhusisha na kumuexpose mrussia na kuonyesha kuwa russia anamchafua Marekani.
 
Hawajasema hawatashiriki, ila hawata peleka mwakilishi yoyote wa kiserikali kama ilivyo kawaida yao, mfano Rais, first lady nk nk.
 
Malekani ni hopeless kweli,kwahiyo wanataka kufanya nn,wawape siraha Basi waingie mstuni kudai Uhuru huo wanaoutaka. USA leaders are bonded by dark spirit for sure!!
 
Back
Top Bottom