- Source #1
- View Source #1
Nimekutana na poster yenye taarifa kuhusiana na ubalozi wa Marekani kuisaidia CHADEMA kufanya maandamano, je ni upi uhalisia wake?
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.
Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa).
Ubalozi wa Marekani tarehe 9/09/2024 walitoa tamko lao kuhusu utekaji na mauaji ya Ali Kibao.
Siku ya jumatatu ya tarehe 23/09/2024 yalifanyika maandamano katika baadhi ya maeneo ikiwemo magomeni ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alikamatwa na watu wengine pia kama taarifa ya jeshi la Polisi ilivyoeleza.
Mara baada ya maandamano hayo imekuwepo taarifa Kupitia mtandao wa X ikidai kuwa Ubalozi wa Marekani wapanga kuisadia CHADEMA kufanya maandamano kesho 24/09/2024.
Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umeaibani kuwa taarifa hiyo Si ya kweli, mathalani kwa kutumia Google Reverse Image Search, JamiiCheck imebaini kuwa ujumbe huu haujawahi kuchapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya The Chanzo kama inavyodaiwa kwani hakuna kumbukumbu rasmi zinazoonesha historia ya ujumbe huo kuwahi kuchapishwa mtandaoni na ukurasa huo.
Kwa kurejea mpangilio wa utengenezaji wa Graphics zinazotumiwa na ukurasa waThe Chanzo, JamiiCheck imegundua mapungufu kadhaa ya Graphic inayosambaza ikiwemo aina ya maandishi (fonts) zilizotumika ni tofauti, lakini pia sehemu ilipoandikwa tarehe na aina ya mwandiko zimetofautiana.
Lakini pia kwa kupitia utafutaji wa Keywords SearchMathalani, kwa kutumia Keyword Search (Ubalozi wa Marekani wapanga kuisaidia) kama sehemu ya maneno yanayopatikana kwenye ujumbe huo, JamiiCheck haikupata ushahidi muhimu unaoelekea kwenye kurasa rasmi za The Chanzo wala ubalozi wa Marekani au chombo chochote cha habari cha kuaminika.
Lakini pia kurasa rasmi za ubalozi wa Marekani nchini Tanzania hawajachapisha wala kutoa taarifa yoyote kuhusiana na wao kuwasaidia CHADEMA maandamano kama ilivyoelezwa kwenye taarifa hiyo ya uzushi.