Marekani kulipiza kisasi kwa kodi ya kidigitali ya Ufaransa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani umependekeza ushuru wenye thamani ya dola bilioni 2.4 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Ufaransa kama jibini na mikoba ya wanawake, kulipiza kisasi hatua ya Ufaransa ya kuyatoza kodi makampuni maarufu ya kidigitali kutoka Marekani, kama Google, Amazon na Facebook.

Ofisi ya mwakilishi wa kibiashara wa Marekani amesema kodi hiyo mpya ya Ufaransa ilikuwa ikiyabagua makampuni ya kimarekani, na kuongeza kuwa ushuru utakaowekwa na nchi yake unaweza kufikia asilimia 100 ya thamani ya bidhaa za Ufaransa.

Ofisi hiyo imesema itasikiliza maoni ya umma wa Marekani kuhusu mpango wake, katika kikao kitakachofanyika kuanzia tarehe 6 hadi 7 za mwezi ujao wa Januari. Ufaransa imesema lengo la kodi yake ni kuyazuia makampuni hayo ya kimarekani kukwepa kodi kwa kuweka makao yake makuu katika nchi zenye viwango vya chini vya kodi barani Ulaya.
 
Back
Top Bottom