Marekani kufunga balozi zake 2 zilizopo Urusi kwa sababu za kiusalama

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Marekani inapanga kuzifunga ofisi mbili za ubalozi mdogo nchini Urusi kwa sababu ya masuala ya usalama na ulinzi.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema ubalozi mdogo kwenye mji wa Vladivostok na mwingine kwenye mji wa Yekaterinburg ndiyo zitafungwa baada ya mashauriano na balozi wa Marekani nchini Urusi, John Sullivan.

Taarifa ya Wizara hiyo imesema tayari shughuli kwenye ofisi hizo zilikwishapunguzwa tangu mwezi Machi kutokana na janga la virusi vya corona.

Katika miaka ya karibuni mahusiano kati ya Urusi na Marekani yamekuwa magumu kutokana na dhima ya mataifa hayo mawili kwenye mizozo nchini Syria na Ukraine na madai ya Urusi kuwa Marekani inaingilia mambo yake ya ndani.
 
Itakuwa wanatafuta "fronts" ili tusijali na kujadili ufyongo walofanya kwenye uchaguzi wao mkuu.

"This election is far from over!" Donald Trump

"There are certain disturbing issues unprecented in the history of the United States which we have witnessed in this election process that are even unthinkable in countries like Tanzania."~ Ruddy Guilliani.

"I don't even care about what they have to say." ~ Joe Biden
 
Ukisikia CIA inatoa ushauri kwamba balozi hizo zifungwe basi Urusi iwe makini kwamba kuna mpango unasukwa na agencies za kijasusi za nchi za magharibi, specifically USA wakiwa na lengo la ku-incite matendo ya kigaidi katika miji/majimbo tajwa huko Urusi hivi karibuni au Trump na Pompeo wana mpango wa kufunga/fukuza maafisa wa balozi ndogo za Urusi nchini Merikani.

Wenye matatizo ya kishenzi ni Trump na Pompeo hao ndio wamepania kuacha wamevuruga uhusiano wa USA na Urusi even farther kabla ya kuondoka Ikulu ili Biden apate wakati mgumu wa kuelewana na Putin, ndio walivyo. Kitu cha kwanza ambacho Rais Biden agefanya baada ya kuingia Ikulu ni kumtimua kazi Balozi wa Merikani nchini Urusi Bw.Sullivan mambo mengine yatafuata ili ku-normalise mahusiano mazuri baini ya nchi hizi mbili.
 
Back
Top Bottom