Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Marekani itafanya mazungumzo rasmi na wanamgambo wa Taliban kwa mara ya kwanza, tangu Marekani ilipoondoa vikosi vyake nchini Afghanistan.
Hayo yamethibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington, katika tangazo lililosema kwamba ujumbe wa nchi hiyo utakutana uso kwa uso na wawakilishi wa ngazi ya juu wa Taliban katika mji mkuu wa Qatar, Doha leo Jumamosi na kesho Jumapili.
Marekani inataka kuwahimiza watawala hao wapya wa Afghanistan kuheshimu haki za binadamu na kuruhusu mashirika ya msaada wa kiutu kuwafikia wenye mahitaji
Tangu kuchukuwa udhibiti wa nchi katikati ya mwezi Agosti, Taliban wamekuwa wakifanya kila juhudi kutambuliwa kimataifa. Marekani imesema kukutana nao haimaanishi kuuutambua utawala wao.
Chanzo: Muungwana blog