Marekani: Kikongwe wa miaka 91 adai hana mpango wa kustaafu jeshi la polisi

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,508
19,888
Katika hali ya kawaida ni vigumu sana kusikia mtu mwenye umri wa miaka 91 bado yupo kazini na wala hana mpango wa kustaafu, na kitu gani kinakuja haraka haraka kichwani mwako unaposikia kuwa yupo na hataki hata kusikia hilo neno kustaafu.

210326204800-officer-lc-buckshot-smith-exlarge-169.jpeg

Afisa mmoja wa polisi, Arkansas nchini Marekani maarufu kwa jina la “Buckshot” Smith amesisitiza hana mpango wa kustaafu licha ya kuwa na umri wa miaka 91.

Kikongwe huyo ambaye mwezi Mei atatimiza miaka 92 ametoa kauli hiyo iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

LC “Buckshot” Smith amefanya kazi hiyo ya kusimamia sheria kwa zaidi ya miaka 56 huku akiwa anakaribia kufikisha miaka 92, huku akisema astaafu mpaka pale Mungu atakapomtaka kufanya hivyo, ”Nitastaafu mpaka Mungu atakavyota kufanya hivyo.”

Akiwa na umri wa miaka 46, kIkongwe huyo aliwahi kustaafu lakini alikaa nyumbani mwezi mmoja pekee na kugundua ni ngumu kwake baada ya kumisi kazi.
 
Wazee wa hivi wanakuaga kauzu sana mtaani. Wabishi mixa bandidu kweli. Vina roho mbaya mbaya kweli.

Akikupita unaongea na demu lazima akutolee shombo na akawachomee "Enhe kijana, unaongea nini na huyu binti? Unataka kumharibia maisha yake, si ndio?.. Na wewe Binti si mtoto wa Mzee fulani? Mzee wako namjua sana tokea kijana mdogo, anaheshima zake unataka kumchafulia jina baba yako!!! Kwanini unakubali kudanganywa na huyu kijana? Mzee wako yupo au kasafiri?... Watoto wa siku hizi hamna adabu kabisa, sio kama wa enzi zetu..."

Ilimradi akutoe mchezoni. Kizee cha hivi kiliwahi kusababisha nihame mtaa niache kodi ya miezi minne kwa kunichomea kibanda kwa Mama mjumbe, nlikua najihemea kwa mtoto wa mama mjumbe.
 
Bila Shaka anapiga deiwaka ya kaz ya upolisi maana kwa umri wake s alitakiwa awe amestaafu au wenzetu hawana hiz mambo katika utumishi.wa umma

Mlioko state mtupe info

Cc Nyani Ngabu
 
Huyo hata kushika Bunduki haruhusiwi maana namuona anavyotetemeka hapo,ila wazee kama hao wanakuwaga bandidu namuona angekuwa Bongo ambavyo kangekataa rushwa hahahahaaaaaa
 
Anategemea dili njaa kukamata Wala ngada na sigara bwege wakimtoa na dolari 2 life's goes on majitaa
 
Hii itakuwa kampuni ya ulinzi makamanda maana huyu mzee Ana vijogoo vya kizushi kwenye kola hakuna jeshi la vijogoo alafu kwa mabega Hana havi ka ransi koplo maybe jeshi la wokovu huko Us
 
Back
Top Bottom