#COVID19 Marekani inatarajia kutoa 'booster vaccine' kwa watu wote waliopata chanjo

Sijui mpango wa hili/haya mataifa ni ipi.
Lakini kila kukicha wanaleta habari mpya.

walisema chanjo ni kwa walio chini ya miaka 18(if not mistaken)

lakini sasa wameshatoa ya watoto.

WORSE ENOUGH
sasa wanasema kwa waliopata chanjo tayari wanahitaji “BOOSTER”

specific kwa walipata from Pfizer and BioNTech. Although wamesema kwa walio na matatizo ya kudumu Au walio na afya isio imara(immune problems)

hofu yangu!
Itakuaje iwe lazima kila mwaka tuchome “BOOSTER”!?

kwa Ninacho amini,
To win the health system market game, is to creat a problem and promise for dependent solution!

what you think ndugu masomaji
 
They just want total protection

death due to Covid Kwa alaiochanjwa ni negligible compared to unvaccinated
Is your statement supported by a research or you just wrote it for the sake of writing.....nakupa homework try to find out death data for COVID-19 vaccine reactions for USA and other European countries,then ndo uje na tamko lako😁😁😁😁
 
Endeleeni kujazana ujinga!! Askofu Rasheed anadai chanjo ina madhara; je hiyo habari inaonesha kwamba chanjo ina madhara au mmeishia kusoma heading tu?
Ma anti-vaxxers ni kama kuku waliokatwa vichwa
 
Leo Jumatano, serikali ya Marekani inatarajia kutangaza kuanza kutoa chanjo ya pili kwa wale waliopata chanjo ya J&J ama ya tatu kwa waliopata chanjo zingine za kukabiliana na covid 19 kwa watu wote waliopata chanjo.

Awali, wiki iliyopita, taasisi ya afya na chakula ya Marekani, FDA ilitoa kibali kwa booster vaccine kwa wale wenye umri wa miaka 60 ama zaidi ama wale wenye magonjwa na ambao kinga yao ya mwili imeshuka, kitaalam wanaitwa immunocompromised patients.

Hii imetokana na ushahidi kutoka Marekani na Israel umeonyesha kua chanjo hupoteza uwezo wake ama ufanisi baada ya miezi 6 toka mtu amechanjwa hivyo anahitaji chanjo nyingine ili kuendelea kumpa mtu kinga zaidi.

Israel wao wameanza kutoa chanjo ya booster kwa watu wote. Hii pia ni baada ya kushuhudia kuongezeka kwa wagonjwa na vifo kwa watu waliochanjwa chanzo zote. Israel ni taifa ambalo limefanikiwa sana kwenye chanjo ya awali baada ya kuchanja zaidi ya 70% ya watu wake.


Du sasa binadamu kageuka'' nyani wa maabara''
 
Mkuu yani unamaanisha waliochanjwa ndo wanakufa zaidi??? Sasa hii huku bongo kwann tunataka kulazimishana watuache kidogo
Wacheni kusoma kwa kutumia viungo visivyohusika. Marekani wanasema wanaokufa na kulazwa hospital kwa wingi sasa hivi ni wale ambao walikataa kuchanjwa. ''While there are fresh surges of virus across the country, nearly all of the people becoming severely ill with Covid-19 now are completely unvaccinated.''
 
Booster shot ilikwishatangazwa Cambodia toka tarehe 1 ya mwezi huu wa nane, sasa wanafuata Marekani!
Cambodia wao wameenda mbali zaidi, kuwataka raia wachome hiyo booster kutoka katika chanjo tofauti na ile waliyochanjwa awali. Mfano kama dozi mbili za awali zilikuwa za AstraZeneca, booster shot itatakiwa iwe Sinovac!

 
Uzuri GwaJima tunamsikiliza,hajasema INA madhara,alisema mfano ,kama ina madhara unapochanja jeshi lote na watu wa afya wote unategemea nn?in case kuna madhara km nchi tutakuwa tuna hali gani kuwa na jeshi lenye shida at the same time wauguzi,drs nao wana shida?

Akashauri hata kwa wao iwe hiari!
Mnapenda sana habari za kusikia vipandevipande
Kama alivyowahi kuwaambia ana uwezo wa kufufua wafu na mkamPigia makofi, sio!! Btw, ana maana aliposema:-
...Mimi si-support. Na watu wangu wote, na mahala popote. ANAYEPENDA KUISHI, nakushauri. Na watu wa Kawe, mimi kama rafiki yako; bahati mzuri watu wa Kawe mna neema kuliko majimbo yote ya Tanzania; mmepata mbunge mtumishi wa Mungu! Ambae akiinua mikono yake anaombea jimbo la Kawe mtu mmoja mmoja. Nimeombea watu wa kawe; MSICHANJWE! Lakini anayetaka, karibu kwa AJILI YA HASARA YAKO
Anamaanisha nini anaposema "anayependa kuishi"? Anamaanisha anaposema (kama unataka kuchanja) kwa HASARA YAKO? Au kwavile hajataja neno madhara ndo unaoana hajasema ina madhara?!
 
Back
Top Bottom