Marekani inaihimiza Uingereza ijitoe katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Serikali ya Marekani inaunga mkono fikra ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano.

Mshauri wa masuala ya usalama wa rais Donald Trump wa Marekani amesema alipokuwa ziarani mjini London wataunga mkono "kwa shauku", Uingereza ikijitoa katika Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano

Akizungumza na waandishi habari John Bolton amesema rais Donald Trump anategemea kuiona Uingereza ikijitenga na Umoja wa ulaya kwa ufanisi ifikapo Oktoba 31.

Mshauri huyo wa rais anayeshughulikia masuala ya usalama ameongeza kusema rais Trump anatarajia kufikiwa makubaliano ya biashara kati ya Marekani na Uingereza.

Kabla ya hapo John Bolton alikutana kwa mazungumzo pamoja na waziri mkuu Boris Johnson na viongozi wengine wa serikali ya Uingereza.
 
I think the UK government is tired to be under the umbrella of EU.It want to be independent so that it might be great again but unfortunately that hopes won't happen , instead it will become weaker than before and it will be under US control.
 
Exactly I can call it a very reasonable fact and that's the reason why America are pushing so hard. Personally I feel sorry for this white folks
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom