Marekani inafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye malipo yoyote yanayohusu Dollar ya Marekani

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,448
17,147
Utawala wa Bwana Donald Trump unafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye manunuzi ya aina yoyote au wanaita dollar decoupling.

Dollar ya kimarekani ndio sarafu maarufu inayotumika kufanya malipo Duniani, zaidi ya 60% ya malipo Duniani yanafanyika kwa njia ya Dollar.

Dollar ndio safaru inayotumiwa na nchi nyingi Duniani kuthaminisha sarafu zao.

Trump anasema hii inaitwa financial nuclear option ya kuimaliza China.

US-China decoupling already under way, John Bolton says
 
Kwa nini DT haataki Yuan ishuke thamani na ikishuka huwa anapiga kelele nyingi?? Sasa wajaribu ivyo waone mziki wake

Actually Wachina na Warusi wana Gold reserve za kutosha kwenye Vaults zao, na kizuri zaidi ushirika wa BRICS wako mbioni kutosa Dollar na kuanza kutumia Yuan, fedha za kichina zimekwisha kubarika sana Duniani -

Mimi naona majigambo ya Trump yana lengo la kujipigia debe kwa wapiga kura, si unajua tena huu ni mwaka wa Uchaguzi nchini mwake hivyo anataka ajionyeshe kwamba yeye ndie mwamba wa kuwakomesha Wachina. Uchaguzi ukiisha utamuona Trump anakwenda kumbeleza Ti Xi Ping yaishe.
 
Hiili USA atasanda. China mpaka Sasa tayari ana Yuan Clearinghouse na tayari Kuna Nchi wanaitumia. Mpaka Sasa Duniani kote kutuma hela China na Kwengineko lazima hela zipite USA (SWIFT) na wanapata % kwa kila dola moja.Na iwapo USA atamstop Mchina matumizi ya Dola itakuwa Tzs to Yuan... Kenya Shillings to Yuan etc.
 
Yeah, China akiamua kutumia hela yake kibiashara inamaana dola inaenda kushuka thamani, nimekusima mkuu

Mmarekani uchumi wake upo hivi due to dollarization,naona Trump alijui hili mkuu!! Iwapo mfano Asia,Africa yote na ulaya wakawa wananunua na kuuza bidhaa with China in Yuan ,bila SWIFT kuwepo katikati .......asubuthuuu....
 
Hiiv jaman ni kwamba sisi ambao tuko Tanzania na si ajab wengi hapa hata Amsterdam tuu hamja cross ndio tunajua zaid ya hawa wamarekan? Kwamba wao wakati wanaamua haya hawajafikiria hilo?

Kwa hio all major banks pale kuanzia BA, JP, Chase bank, Lehman Brothers, Citi Bank, including Federal reserve hawa woote hawajaona haya ni sisi tu tunaona hii impact.....narudia tena msemo wake "we have gat all options on the table" kwa hio mchina yeye baada ya hilo achague njia yake then ndio tutaanza kuona zile options sasa pale mezan
 
Kama Mchina ana dollar zake, na anataka kununua mafuta ya MSaudi au dhahabu ya Mtanzania kwa dollar za Kimarekani, Mmarekani atamzuia vipi Mchina kutumia dollar?
... kama watakabidhiana maburungutu ya fedha kwa viroba sawa ila kama zitapitia through formal financial transactions SWIFT haikwepeki na hapo ndipo mchina anapochapiwa.
 
Hiiv jaman ni kwamba sisi ambao tuko Tanzania na si ajab wengi hapa hata Amsterdam tuu hamja cross ndio tunajua zaid ya hawa wamarekan? Kwamba wao wakati wanaamua haya hawajafikiria hilo? Kwa hio all major banks pale kuanzia BA, JP, Chase bank, Lehman Brothers, Citi Bank, including Federal reserve hawa woote hawajaona haya ni sisi tu tunaona hii impact.....narudia tena msemo wake "we have gat all options on the table" kwa hio mchina yeye baada ya hilo achague njia yake then ndio tutaanza kuona zile options sasa pale mezan
... bila kusahau wale mabilionea wanaokutana pale Breton Woods kujadili uchumi wa dunia eti nao hawajawaza hilo na badala yake wamewaachia wauza kuku wa Tandale wadadavue mambo hayo kwa niaba yao! Ajabu sana Mkuu.
 
Nakwambia dunia ina mambo sana hii mkuu
 
Hiiv jaman ni kwamba sisi ambao tuko Tanzania na si ajab wengi hapa hata Amsterdam tuu hamja cross ndio tunajua zaid ya hawa wamarekan? Kwamba wao wakati wanaamua haya hawajafikiria hilo? Kwa hio all major banks pale kuanzia BA, JP, Chase bank, Lehman Brothers, Citi Bank, including Federal reserve hawa woote hawajaona haya ni sisi tu tunaona hii impact.....narudia tena msemo wake "we have gat all options on the table" kwa hio mchina yeye baada ya hilo achague njia yake then ndio tutaanza kuona zile options sasa pale mezan
Na mimi nashangaa.
 
... kama watakabidhiana maburungutu ya fedha kwa viroba sawa ila kama zitapitia through formal financial transactions SWIFT haikwepeki na hapo ndipo mchina anapochapiwa.
Kinachotokea, kama hii habari ipo kama ilivyoandikwa na unavyosema wewe, ni Mmarekani kuharakisha watu kama Wachina na Warusi kutoka katika hiyo mifumo ya SWIFT.

Unafikiri Mtanzania akiambiwa ajisajili kwenye mfumo mpya wa Mchina, ambao si SWIFT, ambao utampa mabilioni ya dola, atakataa?

Mchina anaweza kutumia njia nyingine.

Mrusi kashaanza kuban American systems kama Visa na Mastercard.
 
Back
Top Bottom