Marekani imetangaza marufuku ya mwaka mmoja ya kuagiza mbwa kutoka nchi 113 kwa kuhofia ugonjwa wa kichaa cha mbwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Kituo Cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) kimetangaza marufuku ya mwaka mmoja ya kuagiza mbwa kutoka nchi 113 kwa kuhofia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Marufuku hiyo inahusisha mbwa wote, pamoja na wale wanaotumika kutoa msaada wa kifikra kwa wanaohitaji usaidizi wa wanyama hao na wale ambao wamekuwa katika nchi zenye hatari katika miezi sita iliyopita. Tangazo hilo linakuja wakati ambapo pamekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaomiliki mbwa kati kati ya janga la Corona.

''Mamia ya mbwa hawa walikuwa na vyeti bandia vya kuthibitisha matibabu ya kichaa cha mbwa'', CDC imesema.

"Hatua hii ni muhimu kuhakikisha afya na usalama wa mbwa walioingizwa Marekani na kulinda afya ya umma na kuzuia kuletwa tena kwa virusi mbali mbali vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa," CDC ilisema katika taarifa.

Marufuku hiyo inalenga nchi tofauti ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Brazil na Urusi.


Chanzo: Muungwana
 
Back
Top Bottom