Marekani imeshika nafasi ya kwanza kwa nchi yenye roho nzuri Dunani. Kwa Afrika, Kenya, Zambia na Sierra Leone zaongoza kuwa na roho nzuri

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,289
16,973
Taasisi ya Charities Aid Foundation ya Uingereza imeitaja Marekani kama nchi yenye roho nzuri (most generous country) Duniani, ikifuatiaa na Myanmar na New Zeeland huku nchi zenye watu wachoyo zaidi ikiwa ni China, Yemen na Ugiriki.

Kwa Afrika nchi kama Kenya, Zambia na Sierra Leoni zikishika namba moja kwa mchi zenye watu wakarimu zaidi na kwamba kwa hizo nchi ni rahisi sana mtu kumsaidia mgeni na hii inachangiwa na utamaduni wa kiafrika wa kusaidiana.

Kwenye world generous index Marekani imeshika namba moja kua ni nchi yenye roho nzuri, yenye watu wanaopenda kusaidia wengine.

The U.S. is the No. 1 most generous country in the world for the last decade The U.S. is the No. 1 most generous country in the world for the last decade
 
Nafikiri ni watu watoaji, sio wenye roho nzuri. Wametoa kwa kuwa wanazo sio lazima kuwa wanajali.
 
Kenya kulikuwa na matangazo ya harambee za kuchangia wanafunzi enzi zile za Moi.Sijui bado hiyo inaendelea?
Wanafunzi wa shule za msingi walikuwa wakipewa maziwa enzi hizo.
Wanamuziki wakubwa wa zamani kimbilio lao lilikuwa Kenya.Akina Mubarak Mwinshehe na wengine wengi.

Binafsi nilitamani kuwa Mkenya.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom