FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,491
- 8,027
Well said mkuu,lakini mimi nina maoni tofauti kidogo - binafsi naona this is an inside operation/job, hakuna cha ujasusi wala nini sijui - kuna wajanja walijipanga kupiga hela ndefu kwa kuingilia software zinazo tumiwa na PLCs kuongozea mfumo wa usafirishaji mafuta kupitia kwenye mabomba - haya mambo ya kuanza kusingizia former Soviet Union Republics na Urusi yenyewe huo ni usanii tu wenye lengo la kuzuga Wamerikani wenzao.
Kitu kingine, chukulia mfano wa mashambulizi ya kile wanacho kiita ugaidi kwenye twin towers NY-huo ni mpango ulio sukwa kifundi na Rais Bush Jr, Makamu wake Dick Chenny, Rumsfield pamoja na Israel lengo lao kuu lilikuwa kutafuta kisingizio cha kumuondoa madarakani Saddam Hussein kwa gharama yoyote ile, kisa? Saddam Hussein alituhumiwa kwamba alitaka kumuua Rais Bush Sr, wakati alipo kuwa ziarani Kuwait wakati huo akiwa ni bado Rais wa Merikani, hivyo dogo Bush alikuwa na ajenda za siri mbili: Ya kwanza alitaka kulipiza kisasi kwa kutokana na tuhuma za Hussein kutaka kumuua baba yake, ajenda ya pili ilikuwa kuiba mafuta ya Iraq, familia ya Bush inajihusisha sana na biashara ya mafuta huko kwao Texas - sijui kwa nini watu hawa kuhoji iweje Bush Jr adai Osama bin Laden ndie muhusika mkuu wa mashambulizi ya kigaidi kwenye twin towers cha ajabu badala ya kumfuata Osama huko Afghanistan yeye akili zake zote na resources zote za kijeshi aka zielekeza Iraq kwa Saddam Hussein,mpaka anatoa amri anyongwe adharani
Siku nyingine ntazungumzia kuhusu mbinu zilizo tumika kuporomosha majengo,ndege zilitumiwa losheni za juu tu impact zingeharibu losheni za juu tu na sio kuporomoja majengo mazima mazima almost at the same time!! This was unquestionably a Controlled demolishion/emplosion iliyo tekelezwa na demolishion experts by ringing high explosives kwenye columns za foundation, ntazungumzia vile vile vijana wa kisaudi Arabia walio daiwa ndio waliteka nyara ndege na kwenda kuzibamiza kwenye majengo - usanii mwingi ndio ulitawala kwenye operation nzima - As I said hilo ntalieleza siku nyingine - tuombe uhai.
Nyinyi ni waumini wa conspiracy theories?mkui itapendeza ukifanya hivo
Maana kuamini masuala kama controlled demolitions, kwamba vilipuzi vilipandikizwa ndani ya majengo kabla ya tukio. Kwamba Marekani ilikuwa ikitafuta justification ya kuivamia Afghanistan n.k. inahitaji kuwa muumini haswa wa masuala hayo.
Wapo pia wanaoamini kuwa dunia ni kama sahani ya kulia ugali. Wote hao wamo katika kundi moja linalofahamika kama conspiracists.