Marekani ilidukua Mawasiliano ya viongozi wa ngazi ya juu wa Ulaya kwa kutumia miundombinu ya mawasiliano ya Denmark

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mataifa kadhaa ya Ulaya yametaka kupatiwa majibu kufuatia ripoti kuwa Marekani iliwapeleleza viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hizo washirika kwa kutumia miundombinu ya mawasiliano ya Denmark kati ya mwaka 2012 hadi 2014.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wamesema kwa pamoja kuwa kuendesha ujasusi miongoni mwa mataifa washirika ni jambo lisilokubalika na kuwa wanataraji kupata ufafanuzi kutoka Washington na Copenhagen.

Matamshi hayo ya kutaka majibu yanafuatia ripoti ya uchunguzi iliyorushwa siku ya Jumapili na vyombo vya habari barani Ulaya ambayo imefichua kuwa taasisi ya usalama wa taifa ya Marekani NSA ilitumia mifumo ya mawasiliano ya Denmark kuwapeleleza wanasiasa wa ngazi ya juu nchini Ufaransa, Ujerumani, Norway na Sweden.

Inaarifiwa kuwa NSA ilifanikiwa kudukua mawasiliano ya ujumbe mfupi, mazungumzo ya simu na hata matumizi ya intaneti ikiwemo ya kansela Angela Merkel wa Ujerumani na viongozi wengine wakuu wa serikali.

Rais Macron ambaye jana alifanya mkutano kwa njia ya video na Kansela Merkel amesema hakuna nafasi kwa washirika wa Ulaya na Marekani kutiliana mashaka na ndiyo maana ni muhimu kwa Washington kufafanua kile kilichotokea.
"Hili halikubaliki miongoni mwa washirika na kwa hakika halikubaliki kabisa baina ya washirika wa Ulaya.

Ninaongozwa na msingi wa kuaminiana ambao unatuunganisha watu wa Ulaya na Marekani, kwa namna hiyo tunafanya kila kitu kwa usalama wa pamoja na hakuna nafasi ya kutiliana wasiwasi baina yetu." amesema Macron.
 
Hii habari ya mwaka gani. Mbona hili swala mie wa huku nanjilinji nalijua mda Sana! Ina maana France na wenzake Hawakuwahi kuelewa Marekani huwacheza shere kila Mara? Hata Snowden alisema.
Juu ya udukuzi ule , akihojiwa Rais Putin wa Urusi alisema anashangaa kwanini Russia haikuwa mlengwa mkuu wa jam o lile.
Mwwnyekiti wa chama kikuu Cha upinzani kule Ujerumani alipiga kelele akisema Marekani si taifa kuubwa la kuitisha kiasi kile Ujerumani.
 
Back
Top Bottom