Marekani: Hatuna uwezo wa kuishambulia kijeshi Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,868
Kukiri Waziri wa Ulinzi wa Marekani juu ya kutokuwa na uwezo nchi yake wa kuishambulia kijeshi Iran

Mara kadhaa katika miongo michache iliyopita Marekani imewahi kutishia kuishambulia kijeshi Iran.
Hususan katika kipindi cha urais wa George W. Bush, ambapo baada ya kuzishambulia kijeshi Afghanistan na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, suala la kuishambulia kijeshi Iran pia lilishika kasi sana, lakini kutokana na uwezo mkubwa wa kujilinda iliyonayo nchi hii, jambo hilo halikuweza kufikiwa.

Katika kipindi cha Barack Obama, rais wa zamani wa Marekani kutoka chama cha Democrat, yeye pia na kwa mara kadhaa alisisitizia kile kilichosemwa kuwa ni kuwepo machaguo yote mezani kwa ajili ya kukabiliana na Iran. Hata hivyo licha ya Obama kujitahidi sana kuishinikiza Tehran isimamishe miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani kupitia njia ya vikwazo vikali, lakini pamoja na hayo na ili kuitisha Tehran, kwa mara kadhaa alizungumzia uwezekano wa kutekelezwa shambulizi la kijeshi kama njia ya mwisho kwa ajili ya kukabiliana na miradi ya nyuklia ya nchi hii. Baada ya kuingia madarakani Donald Trump naye pia kama walivyokuwa watangulizi wake, ametumia vitisho vya kila namna dhidi ya Iran.

Katika uwanja huo tarehe 9 Mei 2018, yaani siku moja baada ya kutangaza kuiondoa nchi yake katika mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCPOA, Trump aliitishia pia Iran kwa kusema: "Iran ama lazima ifanye mazungumzo au kuna tukio jengine litatokea." Trump aliongeza kwa kusema: "Ninaiusia Iran isianze upya miradi yake ya nyuklia. Ninawausia kwa nguvu zote kwamba ikiwa wataendelea na shughuli hiyo, basi watakumbwa na hatma mbaya sana." Mwisho wa kunukuuu. Pamoja na kwamba baadhi ya weledi wa mambo waliyatafsiri maneno ya Trump juu ya hatma mbaya sana kuwa ni chaguo la kijeshi dhidi ya Iran, lakini matamshi ya hivi karibuni ya viongozi wa Marekani yanaonyesha kinyume na vitisho hivyo vya Trump.

Katika uwanja huo, James Norman Mattis, Waziri wa Ulinzi wa Marekani na katika matamshi yake mapya amekiri kwamba, nchi yake haina uwezo wa kufanya shambulizi la kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha Mattis akielezea uvumi ulioenezwa na vyombo vya habari kwamba Washington inapanga mpango wa kuzishambulia kijeshi taasisi za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa madai hayo ni njozi na ngano tupu.

Kadhalika hivi karibuni kanali ya televisheni ya ABC News ya Australia ikimnukuu afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo ilitangaza kwamba, serikali ya Marekani iko katika mchakato wa kupanga mipango ya kuzishambulia taasisi za nyuklia za Iran. Hata hivyo muda punde baadaye Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu wa Australia alikadhibisha ripoti hiyo na kudai kuwa habari hiyo ni dhana pekee ambayo imeegemea juu ya vyanzo visivyo na mashiko.

Kwa hakika suala la kukadhibishwa kadhia ya shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran kulikofanywa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, kumetokana na ufahamu wa viongozi wa Washington juu ya uwezo mkubwa wa kijeshi na wa kujilinda wa Iran, hususan katika uga wa makombora na vita visivyo na mlingano ambapo ni suala lisilo na shaka kwamba, iwapo nchi mbili zitaingia katika vita hivyo, basi Marekani itashuhudia kipigo kikali dhidi ya askari na taasisi zake za kijeshi zilizopo katika eneo la Mashariki ya Kati. Itafaa kuashiria kuwa, katika siku za hivi karibuni kumeongezeka mvutano wa kimaneno kati ya viongozi wa Iran na Marekani.

Itakumbukwa kuwa Jumapili ya tarehe 22 Julai mwaka huu, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwahutubu viongozi wa Marekani na katika kujibu vitisho wa Rais Donald Trump vyenye lengo la kuzuia uuzaji mafuta nje ya nchi hii, alisema kuwa , Iran imekuwa ikidhamini usalama wa eneo hili kwa kipindi chote cha historia, hivyo Trump hatakiwi kucheza na mkia wa simba, kwa sababu jibu la Iran litakuwa la kukatisha tamaa.

Katika kujibu, Trump alitoa maneno ya kuropokwa na yasiyo ya kawaida kwa kuitishia Iran na kile alichokisema kuwa ni 'hatma mbaya'. Katika ujumbe aliouandika kupitia mtandao wa kijamii ya Twitter Trump alisema: "Usitoe vitisho kwa Marekani hata kidogo kwa sababu utapata hasara kutokana na hilo au utakumbwa na hatma mbaya ambayo haijawahi kumpata yeyote katika historia." Mwisho wa kunukuuu. Hata hivyo badala ya matamshi hayo ya Trump kupewa uzito, yalikabiliwa na kejeli hususan za viongozi wa Marekani kwenyewe kutoka chama cha Democrat na hata katika mitandao mbambali ya kijamii ya nchi hiyo. Katika uwanja huo huo,

Naye Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran akijibu bwabwaja na vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran alisema kuwa, kuanzisha vita na taifa hili maana yake ni kuangamia suhula zote za Marekani.

Meja Jenerali Qassem Suleimani amesisitiza kuwa, endapo Marekani itaanzisha vita na Iran suhula zote za Washington zitaangamia na Iran ndio itakayoamua kumalizika kwa vita hivyo au la. Hakuna shaka kwamba, radiamali kali ya viongozi wa Iran dhidi ya vitisho vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya Iran ndiyo imewafanya viongozi wa ngazi ya juu wa Washington akiwemo Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo kulegeza kamba kuhusiana na Iran.
4bpo9161628acb13r1t_800C450-1.jpg
4bprfb712f662a183c5_800C450.jpg
4bn17032691144vqo7_800C450.jpg
4bpr13f3135191182fy_800C450.jpg
 
suala sio US wanashindwa kumshambulia Iran no ila moja wanahofia Russia ata react vipi na pili hawana uhakika kama Iran wanamiliki atomic bombs au lah! Maana zitarushwa Israel fasta kitu ambacho trump hatathubutu kusababisha kitokee
 
Mmarekani ana zingua banna ni libeti ata mtifua kiduku ni kaliwa. Sasa sibeti tena inaonekana kashakuwa muoga
 
Kukiri Waziri wa Ulinzi wa Marekani juu ya kutokuwa na uwezo nchi yake wa kuishambulia kijeshi Iran
ubwa wa kijeshi na wa kujilinda wa Iran, hususan katika uga wa makombora na vita visivyo na mlingano ambapo ni suala lisil
sawa. ila tuwekee link nasisi tusome jinsi wamarekani walivyokiri
 
Huyu ni popo tyu kila siku Iran
1.hana ushahidi wa anachoongea
2Israel inawachakaza vibaya Syria ila wako kimya wanaharisha tyu
3.uchumi wa Iran bado ni dhaifu sana kuhimili vita
4.Iran imezungukwa na maadui wengi hvo ni rahisi kuangushwa
5.marekani ina mataifa mengi yenye nguvu yatakayoipa saport tofauti na Iran Amby sioni mshirika yeyote wa muhimu
6.Teknolojia ya kijeshi na silaha mpya Iran bado mtoto mdogo sana
 
Yaani ukishakuwa na akili za kupiga kichwa chini hadi sugu linatokeza ktk paji la uso ujue ww ni fa.la kabisa, ndio ufala huo unaweza sema US haina uwezo wa kuishambulia Iran kijeshi..!! Ni fa.la tu ndio hajui Nguvu za kijeshi za US zikoje alafu anaandika upuuzi kama huu.. Iran ni kijitoto kidogo sana sanaa mbele ya US..
 
Kukiri Waziri wa Ulinzi wa Marekani juu ya kutokuwa na uwezo nchi yake wa kuishambulia kijeshi Iran

Mara kadhaa katika miongo michache iliyopita Marekani imewahi kutishia kuishambulia kijeshi Iran.
Hususan katika kipindi cha urais wa George W. Bush, ambapo baada ya kuzishambulia kijeshi Afghanistan na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, suala la kuishambulia kijeshi Iran pia lilishika kasi sana, lakini kutokana na uwezo mkubwa wa kujilinda iliyonayo nchi hii, jambo hilo halikuweza kufikiwa.

Katika kipindi cha Barack Obama, rais wa zamani wa Marekani kutoka chama cha Democrat, yeye pia na kwa mara kadhaa alisisitizia kile kilichosemwa kuwa ni kuwepo machaguo yote mezani kwa ajili ya kukabiliana na Iran. Hata hivyo licha ya Obama kujitahidi sana kuishinikiza Tehran isimamishe miradi yake ya nyuklia yenye malengo ya amani kupitia njia ya vikwazo vikali, lakini pamoja na hayo na ili kuitisha Tehran, kwa mara kadhaa alizungumzia uwezekano wa kutekelezwa shambulizi la kijeshi kama njia ya mwisho kwa ajili ya kukabiliana na miradi ya nyuklia ya nchi hii. Baada ya kuingia madarakani Donald Trump naye pia kama walivyokuwa watangulizi wake, ametumia vitisho vya kila namna dhidi ya Iran.

Katika uwanja huo tarehe 9 Mei 2018, yaani siku moja baada ya kutangaza kuiondoa nchi yake katika mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCPOA, Trump aliitishia pia Iran kwa kusema: "Iran ama lazima ifanye mazungumzo au kuna tukio jengine litatokea." Trump aliongeza kwa kusema: "Ninaiusia Iran isianze upya miradi yake ya nyuklia. Ninawausia kwa nguvu zote kwamba ikiwa wataendelea na shughuli hiyo, basi watakumbwa na hatma mbaya sana." Mwisho wa kunukuuu. Pamoja na kwamba baadhi ya weledi wa mambo waliyatafsiri maneno ya Trump juu ya hatma mbaya sana kuwa ni chaguo la kijeshi dhidi ya Iran, lakini matamshi ya hivi karibuni ya viongozi wa Marekani yanaonyesha kinyume na vitisho hivyo vya Trump.

Katika uwanja huo, James Norman Mattis, Waziri wa Ulinzi wa Marekani na katika matamshi yake mapya amekiri kwamba, nchi yake haina uwezo wa kufanya shambulizi la kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha Mattis akielezea uvumi ulioenezwa na vyombo vya habari kwamba Washington inapanga mpango wa kuzishambulia kijeshi taasisi za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa madai hayo ni njozi na ngano tupu.

Kadhalika hivi karibuni kanali ya televisheni ya ABC News ya Australia ikimnukuu afisa mmoja wa serikali ya nchi hiyo ilitangaza kwamba, serikali ya Marekani iko katika mchakato wa kupanga mipango ya kuzishambulia taasisi za nyuklia za Iran. Hata hivyo muda punde baadaye Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu wa Australia alikadhibisha ripoti hiyo na kudai kuwa habari hiyo ni dhana pekee ambayo imeegemea juu ya vyanzo visivyo na mashiko.

Kwa hakika suala la kukadhibishwa kadhia ya shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran kulikofanywa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, kumetokana na ufahamu wa viongozi wa Washington juu ya uwezo mkubwa wa kijeshi na wa kujilinda wa Iran, hususan katika uga wa makombora na vita visivyo na mlingano ambapo ni suala lisilo na shaka kwamba, iwapo nchi mbili zitaingia katika vita hivyo, basi Marekani itashuhudia kipigo kikali dhidi ya askari na taasisi zake za kijeshi zilizopo katika eneo la Mashariki ya Kati. Itafaa kuashiria kuwa, katika siku za hivi karibuni kumeongezeka mvutano wa kimaneno kati ya viongozi wa Iran na Marekani.

Itakumbukwa kuwa Jumapili ya tarehe 22 Julai mwaka huu, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwahutubu viongozi wa Marekani na katika kujibu vitisho wa Rais Donald Trump vyenye lengo la kuzuia uuzaji mafuta nje ya nchi hii, alisema kuwa , Iran imekuwa ikidhamini usalama wa eneo hili kwa kipindi chote cha historia, hivyo Trump hatakiwi kucheza na mkia wa simba, kwa sababu jibu la Iran litakuwa la kukatisha tamaa.

Katika kujibu, Trump alitoa maneno ya kuropokwa na yasiyo ya kawaida kwa kuitishia Iran na kile alichokisema kuwa ni 'hatma mbaya'. Katika ujumbe aliouandika kupitia mtandao wa kijamii ya Twitter Trump alisema: "Usitoe vitisho kwa Marekani hata kidogo kwa sababu utapata hasara kutokana na hilo au utakumbwa na hatma mbaya ambayo haijawahi kumpata yeyote katika historia." Mwisho wa kunukuuu. Hata hivyo badala ya matamshi hayo ya Trump kupewa uzito, yalikabiliwa na kejeli hususan za viongozi wa Marekani kwenyewe kutoka chama cha Democrat na hata katika mitandao mbambali ya kijamii ya nchi hiyo. Katika uwanja huo huo,

Naye Kamanda wa Kikosi cha Quds katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran akijibu bwabwaja na vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran alisema kuwa, kuanzisha vita na taifa hili maana yake ni kuangamia suhula zote za Marekani.

Meja Jenerali Qassem Suleimani amesisitiza kuwa, endapo Marekani itaanzisha vita na Iran suhula zote za Washington zitaangamia na Iran ndio itakayoamua kumalizika kwa vita hivyo au la. Hakuna shaka kwamba, radiamali kali ya viongozi wa Iran dhidi ya vitisho vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya Iran ndiyo imewafanya viongozi wa ngazi ya juu wa Washington akiwemo Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo kulegeza kamba kuhusiana na Iran.
View attachment 822051View attachment 822052View attachment 822055View attachment 822058
Nenda katafute kitu inaitwa Operation Nitron Zeus (NZ),Kwenye ile Documentary ya StuxNet kuna NSA agent aliongelea kidogo kuhusu hii operation.Hawa warekani wasikie tu achana nao kabisa.Fuatulia hii kitu utajua nini nasema.
 
Sidhani kama kweli Marekani haina uwezo wa kuishambulia Iran! Marekani haina huruma na vifo vya watu kwa kusingizia inatafuta silaha za maangamizi. Haijali kwa kuwa vita havipiganwi kwenye nchi yake! Cha kujiuliza, Marekani yenyewe je haina silaha za maangamizi!
 
Wanatafuta silaha za MASS DESTRUCTION wakati wao wana silaha za TOTAL DESTRUCTION!
Alafu kuna mijitu inaamini kwamba usa ndio wataleta Demokrasia duniani!
Pathetic walahi!
 
Back
Top Bottom