Marekani: Donald Trump ashtakiwa kwa pesa haramu anazodaiwa kumlipa nyota wa filamu za ngono

Protect

Member
Apr 4, 2020
94
299
Donald Trump anakuwa rais mstaafu wa kwanza wa Marekani kushitakiwa, baada wazee wa mahakama ya Manhattan jijini New York kupiga kura ya kumshitaki Trump

Trump anatuhumiwa kumlipa hela, Stormy Daniels mcheza sinema za kikubwa ili akae kimya juu ya tuhuma ya mahusiano yao.

=============

Donald Trump amefunguliwa mashtaka na jopo kuu la mahakama ya wilaya ya Manhattan katika jimbo la New York baada ya uchunguzi kuhusu pesa haramu anazodaiwa kulipwa nyota wa filamu za ngono Storm Daniels, gazeti la New York Times limeripoti Alhamisi.

Amekuwa rais wa zamani wa Marekani wa kwanza kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wakati ambapo anagombea tena urais mwaka ujao.

Mashtaka hayo, yaliyotokana na uchunguzi ulioongozwa na mwanasheria mdemocrat wa wilaya ya Manhattan Alvin Bragg, yanaweza kubadili mwelekeo wa kinyang’anyiro cha urais cha mwaka wa 2024.

Awali, Trump alisema kwamba angeendelea kufanya kampeni za uchaguzi wa kumteua mgombea atakayekiwakilisha chama cha Republican ikiwa angeshtakiwa kwa uhalifu.

Jopo kuu la mahakama ya Manhattan lililoitishwa na Bragg mwezi Januari lilianza kusikiliza ushahidi kuhusu jukumu la Trump katika malipo ya Daniels siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa 2016 ambao aliishia kushinda.

Daniels, mwigizaji na muongozaji maarufu wa filamu za ngono ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, alisema alipokea pesa hizo ili asifichuwi kitendo cha ngono alichofanya na Trump mwaka wa 2006.

Trump anakabiliwa pia na kesi nyingine mbili za uchunguzi wa uhalifu. Trump amekosoa vikali hatua hiyo ya kumfunglia mashtaka, akidai imechochewa kisiasa.
 
Swali ni je ata surrender?
Stormy Daniels huyu hapa, picha muhimu
Screenshot_20230331-045024.png
 
Ukipita huku ni issue za LGBTQA (lesbian, gay, bisexual, transgender, intersex, queer, asexual and other sexually or gender diverse) , ukipita kule mara issue za Pornography, Media platforms kubwa zimeamua kutufeed up matakata mpaka akili zetu zikae sawa na kuona nikitu cha kawaida but in reality sio kitu cha kawaida.

Ndio shida ya kutegemea source of information kutoka kwa jirani anakupangia cha kuona na kusikia, tusipo kuwa makini moral values zetu zitadidimia na kupotea kabisa.

We have to Watch Out😠

Wamarekani wamewalazimisha kufuatilia media zao??! Malalamiko ya kitoto.

Wewe fuatilia habari za mfalme Zumaridi kwenye local media zenu.
Ukipita huku ni issue za LGBTQA (lesbian, gay, bisexual, transgender, intersex, queer, asexual and other sexually or gender diverse) , ukipita kule mara issue za Pornography, Media platforms kubwa zimeamua kutufeed up matakata mpaka akili zetu zikae sawa na kuona nikitu cha kawaida but in reality sio kitu cha kawaida.

Ndio shida ya kutegemea source of information kutoka kwa jirani anakupangia cha kuona na kusikia, tusipo kuwa makini moral values zetu zitadidimia na kupotea kabisa.

We have to Watch Out

Similar Discussions

Back
Top Bottom