Marekani angeivamia Iran halafu asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo, halafu Urusi, China, nk ziipatie Iran silaha je, angetoboa?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Hivi Marekani angejichanganya leo akaamua kuivamia Iran kwa kuitumia ardhi ya Iraq lakini asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo kama alivyowekewa Urusi.

Halafu Iran isaidiwe silaha mfululizo na Urusi, China, India, na nchi zingine za kiarabu, je Marekani angestahimili kwa muda gani? Ujue kupigana ukiwa umewekewa vikwazo ni kama kupigana ukiwa umefungwa pingu!
 
Umuwekee vikwazo USA Basi husitumie, Pepsi, Coca-Cola, Colgate,Google, Facebook, watsapp, Tweeter,

Husitumie Dollars, Master card, visacard, paypall, husitumie Boeing, ARV, chanjo za magonjwa. Ulipie 1/3 za mchango kwa UN. Ulipie 2/3 ya bajeti ya WHO

Hudumia kambi za wakimbizi, asa Africa, fafhiri UNHCR, UNO, WFP.

Baada ya hapo muwekee US vikwazo
 
Umechanganya!! Umoja wa mataifa hauhusiki katika kuiwekea vikwazo Urusi pia hautahuisika kuiwekea vikwazo marekani. Kwa hiyo michango yake UN ataendelea kupeleka! Dola za kazi gani, si makaratasi tu hayo? Akiwekewa vikwazo tunaachana na dola tunakubaliana kutumia kila nchi pesa yake! Wakimbizi wataendelea kuhudumiwa na UN maana yenyewe haitahusika.

Ukweli ni kwamba Marekani atapigwa ka mtoto mdogo!!
 
Hivi Marekani angejichanganya leo akaamua kuivamia Iran kwa kuitumia ardhi ya Iraq lakini asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo kama alivyowekewa Urusi. Halafu Iran isaidiwe silaha mfululizo na Urusi, China, India, na nchi zingine za kiarabu, je marekani angestahimili kwa muda gani? Ujue kupigana ukiwa umewekewa vikwazo ni kama kupigana ukiwa umefungwa pingu!!
Hawezi kutoboa wale Afghastani kakaa miaka 20 hakuna cha maana
 
Hivi Marekani angejichanganya leo akaamua kuivamia Iran kwa kuitumia ardhi ya Iraq lakini asisaidiwe na nchi nyingine, awekewe vikwazo kama alivyowekewa Urusi. Halafu Iran isaidiwe silaha mfululizo na Urusi, China, India, na nchi zingine za kiarabu, je marekani angestahimili kwa muda gani? Ujue kupigana ukiwa umewekewa vikwazo ni kama kupigana ukiwa umefungwa pingu!!
Anatoboa, USA sio mchezo
 
Marceneries wangetoka Dunia nzima kuja kuipiga USA ,nchi nyingi sana zingeosaidia Iran kuipiga USA, USA ni dhaifu sana ,
Inachukiwa sana, nakuhakikishia Kuna nchi za NATO zingetoa misaada kwa Siri ili kuiadhibu USA.

Na hii ndio sababu kubwa amabyo inapelekea USA kuingia vitani na wapambe.kuogopa aibu ya kupigwa peke yake.
Ona mifano midogo TU

USA ilipelekea askari wake somalia,ilijikuta inadhalililishwa na wababe wa kivita wa Somalia,akina Mohamed Farah Aidiid.Gen Morgan na wenzao.

Askari wa Marekani walipigwa na wasomali,wakauliwa,wakatekwa na baadhi Yao wakafungwa kwenye magari kwa nyuma wakiwa miguu imefungwa kamba na kufungwa kwenye magari,wakawa wanaburuzwa magari yakipita mitaani.

Kitendo hicho kiliibua chuki ya wananchi wa USA dhidi ya Serikali Yao na hatimae Serikali ikatoa agizo majeshi ya USA yaliyoko somalia yaondoke huko.

Na huo ukawa ni ushindi wa makundi hayo ya kisomali.

USA ilishindwa somalia.
 
Marekani akiwekewa vikwazo na China maana yake China iache kuuza bidhaa zake Marekani, kwa mwaka China inauza zaidi ya dola bilioni 400 kwa Marekani. Kwa hiyo China wawe vilaza waache kupata bilioni 400 kwa mwaka wabaki kwa Russia kupata dola bilioni 50 kwa mwaka, hii ni 1 ya 8.

Wakati huo China ikose patents zote za Marekani. ZTE ilipigwa sanctions na Marekani mpaka leo hatuoni simu zake, Huawei ilipigwa sanctions mpaka ikafungua biashara ya kufuga nguruwe ili kutosheleza profits. Patents za teknolojia ya simu nyingi ni za makampuni ya Marekani. Hata TCMS wataambiwa hakuna kuuza microchips kwa China wala Russia, Samsung Electronics mnayoona hii Marekani ikitaka ipotee sokoni ndani ya miaka minne inaweza potea. Ukipiga marufuku wasitumie foundry tech ya US kutengeneza chips zao za Exynos, au kufanya outsourcing ya chips kutoka kwa Qualcomm ya Marekani. Kwahiyo Samsung nao watachagua upande wa Marekani kuliko China na Russia.

China akishindwa kuzalisha zaidi kwa ajili ya kuuza Marekani atapunguza mahitaji ya gesi na mafuta kutoka Russia na kwingineko, hapo Russia anapunguza mapato, soko la mafuta duniani linashuka uchumi wa OPEC wote unaporomoka na dunia kwa ujumla inaingia mdororo wa uchumi. Marekani inaweza zalisha mapipa milioni 15 ya mafuta kwa siku ukijifanya unaikomoa, kwa siku inatumia mapipa milioni 19 hizo nne zinazokosa kwenye mlinganyo inatafuta hata Libya inawahonga wanaiuzia extra.

Kampuni kama Boeing zinaacha kufanya kazi China na Russia. Pia Dell, HP, Apple, Sony, etc. GPS inafungwa wabaki na GLONAS zao na BeiDou ambazo sio reliable na hazina global support. Android system inafungwa na iOS tuone ni Mwafrika gani ataanza kujaribisha systems ambazo hajawahi sikia. Facebook, WhatsApp, Twitter, Instagram zinafungwa kwao na kwa vifaa wanavyotengeneza. Warusi wabaki na VKontakte (ambayo najua 98% ya wabongo hawajawahi hata kuisikia) na Wachina wabaki na kina WeChat, Weibo na TikTok. Ukiachana na TikTok ni nani duniani hapa atataka aache hizo nyingine atumie VKontakte au Weibo na WeChat?

South Korea, Japan, UK, Germany, France, Australia, Italy, Spain, Canada zitasimama na Marekani. Israel na Switzerland wanaweza chagua kuwa neutral, Waarabu vigeugeu kupindukia watasoma upepo ila wengi watakuwa upande wa Marekani. Yani Qatar aache kuwa upande wa Marekani ambako kila giant aliyeko kule anajiweza na gesi hana, aende kushiriki na China ambako Russia anamuuzia gesi kwa fujo?
 
Umuwekee vikwazo USA Basi husitumie, Pepsi, Coca-Cola, Colgate,Google, Facebook, watsapp, Tweeter,

Husitumie Dollars, Master card, visacard, paypall, husitumie Boeing, ARV, chanjo za magonjwa. Ulipie 1/3 za mchango kwa UN. Ulipie 2/3 ya bajeti ya WHO

Hudumia kambi za wakimbizi, asa Africa, fafhiri UNHCR, UNO, WFP.

Baada ya hapo muwekee US vikwazo
Hivyo vyote ulivyotaja haviwezi kwenda bila uwepo wa Dunia ,marekani anahitaji dunia tofauti unavyofikiri Dunia haiwezi kwenda bila US au unahisi hayo makampuni hayana mbadala .

Hata US wanafahamu Hilo ndio maana wanatumia nguvu kubwa kutengeneza ushawishi na kukubalika duniani na wanakuwa wakali wakikuona tishia kwenye ushawishi wao
 
Mleta mada utakuwa mbea au huna kitu kichwani una mihemko utadhani pre mature ejaculation yaani china inauza bidhaa USA dola bil. 400 na zinazouzwa Urusi ni bilion 50 halafu ukadai ni 1/20 hivi ni matatizo ya hesabu au ni upumbav? Unamaanisha 400÷50 =20?
 
Marceneries wangetoka Dunia nzima kuja kuipiga USA ,nchi nyingi sana zingeosaidia Iran kuipiga USA, USA ni dhaifu sana ,
Inachukiwa sana, nakuhakikishia Kuna nchi za NATO zingetoa misaada kwa Siri ili kuiadhibu USA.
Dah!... You are too 'emotional' mpaka unashindwa kuona uhalisia....

Hizo nchi za Nato ambazo zingeisaidia Iran kisiri ni zipi ?

Udhaifu wa USA ni upi ?....umeupimaje ?
USA ilishindwa somalia.
Kwani USA ilikuwa vitani na Somalia ?
 
Umechanganya!! Umoja wa mataifa hauhusiki katika kuiwekea vikwazo Urusi pia hautahuisika kuiwekea vikwazo marekani. Kwa hiyo michango yake UN ataendelea kupeleka! Dola za kazi gani, si makaratasi tu hayo? Akiwekewa vikwazo tunaachana na dola tunakubaliana kutumia kila nchi pesa yake! Wakimbizi wataendelea kuhudumiwa na UN maana yenyewe haitahusika.

Ukweli ni kwamba Marekani atapigwa ka mtoto mdogo!!
Akili yako ndo imeishia hapo?
 
Yaani Trump alijitoa WHO, shirika liliyumba maana 2/3 ya hela anatoa US, hao china na Russia wanachangia vihela vya nyanya kwenye UN agencies
 
Back
Top Bottom