Marejesho ya Mkopo wa vyuo vikuu

rimbocho

Member
Jan 11, 2010
73
3
Ndugu zanguni wana JF, ninaomba kueleweshwa kidogo juu ya urejeshaji wa mkopo wa vyuo vikuu
1. Ni kwa nini wanasiasa waliweka seal yaani watakao lipa ni wale walio maliza vyuo vikuu kuanzia 1994 na kuendelea na si vinginevyo?
2. Je mtu kusoma na kupata kazi si moja ya mapato ya serikali kwani katika mshahara kila mwezi unalipa kodi ambayo ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya nchi?
3. waliokuwepo bungeni wakati wa kupitisha hoja hiyo walikuwa ni wale waliomaliza chuo before 1994?
4. Kwa wale ambao hawana mkataba na serikali wa namna walivyokopeshwa je watarudisha nini na kwanani kwani bodi miaka ya 1994 ilikuwa haipo, na pia kulikuwa hakuna mkataba na wanafunzi hao wa enzi za no bodi ya mkopo?
 
Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhy....nyamaza! usilikumbushe hili, naona kama llimesahaulika
 
hahaha.... rimbocho!! hoja hii hebu tulia kwanza. taratibuu usiwaamshe
 
Mbona wameshaanza kudai,mie nakatwa kwenye mshahara toka July10.Kudai mafisadi wala??
nchi hii sijui kunakwenda wapi?He Mungu tusaidie waja wako.Usome kwa shida,kazi upate kwa shida,wao waje wakukate pesa kwa ajili ya kampeni chafu za Mama,mtoto .
 
Mbona wameshaanza kudai,mie nakatwa kwenye mshahara toka July10.Kudai mafisadi wala??
nchi hii sijui kunakwenda wapi?He Mungu tusaidie waja wako.Usome kwa shida,kazi upate kwa shida,wao waje wakukate pesa kwa ajili ya kampeni chafu za Mama,mtoto .

Kweli wanakata @ mwezi!
 
Mkuu hata mimi nashangaa sana hii system sijui jamaa wanatupeleka! wapi Mimi nimeingia 2004 hapo UDSM, sijasaini form zozote za mkataba wa kurudisha pesa mpaka niliposaini nadhani ilikuwa 2007, cha ajabu nadaiwa toka mwaka 2004.

I hate this Fraud system, inachanganya sana na unapokuwa unasoma nako hautulii darasani kazi kufuatilia mikopo muda mwingi, ukija kutulia darasani nako Lecturer naye hatulii anafuatilia makato bodi ya mikopo, akitulia darasani, vifaa hakuna vya kufundia, what the hell is that?

Ukiuliza, bodi bado ina changamoto nyingi ambazo muda si mrefu watazimaliza, sasa miaka kibao inapita na majibu hayo hayo.

Serikali ya mafisadi inatumia hela nyingi sana kuingia madarakani jamani, utadhani watanzania tumelogwa kuendelea kuwapa kura. Hivi kwa nini watanzania tusiamue kutoa adabu mwaka huu, DR Slaa hakika utashinda! vijana wajitokeze wapige kura, hata madingi wapenda ccm wapigeni mkwara waitose ccm mwaka huu.

Sitaki kusema ccm hakuna wenye moyo wa uzarendo lakini kama mzalendo yuko ndani ya samaki waliooza wote wameoza. Hakuna huruma tena, MADINGI, MAMAZA wanaipenda ccm kwa sababu ya buku tano na kumi kumi za mida hii ya uchaguzi.


China and Korean don't have tolerance margins for Fraud people, ni kunyongwa tu! ndiyo maana saizi wezi wa kichina wamekimbilia nga'ambo kama Africa ili kutuibia, Lakini sisi tunasema wameonewa.
 
Jamani mimi nakatwa toka 2007 kama 11,000 ivi kwa mwezi wakati wakati namaliza 2004 hakuna form tuliokubaliana kuwa nitalip.SERIKALI YA KIDHALIMU BWANA.
Alafu hata hawasemi mpaka sasa wamekusanya kiasi gani na inatumika kufanya nini?
CCM dhambi ya kuwanyonya ata maskini itakula kwenu chezeni na mafisadi bse ata Mungu hawatambui but kilio cha maskini waweza pata laana
 
vyuo vimefungwa sasa hizi , kwa sababu ya uchaguzi na vikifunguliwa wewe utaona wanafunzi watakavyohangaishwa na bodi ya mkopo. Nitshangaa kama baadhi ya wanafunzi nao wamevalishwa makofia na kuuza kura zao ilihali kama wakkipa ccmakamba wanajua kitakachowapata
 
Sh sh sh ... Let the sleeping dogs continue sleeping!
Wale wote waliosoma kabla ya Bodi ya Mikopo kuundwa majina yao hayako kwenye database ya wanaodaiwa na sioni kama serikalini kuna mtu mwenye wazo la ku-retrieve hizo data.
Ushauri wangu, kama una nia ya kupigania uongozi wa siasa jipeleke mwenyewe ukalipe, lakini kama ni mbeba box kama mimi usipoteze muda wako na hilo deni.
 
Bora CHADEMA waingie tuondokane na kero hii! Jamani si nasikia utafiti umewapa asilimia 47 za ushindi na CCM 41%?:lol:
 
Hakuna anayedaiwa labda wanakukata kwa makosa mpwa, nilishaandika sana hapa ukumbini kuhusu hii na nikanukuu pia baadhi ya machapisho kuwa...kama tunachangia tena chini ya sera ya uchangiaji huduma, basi hatudaiwi! Hakuna sehemu yoyote "kisheria" iliyosema kuwa tumekopeshwa, yote yanaonyesha kuwa ni costshare otherwise kama unalipa na serikali nayo ilipe... USIDANGANYIKE MPWA, AU njoo tugange njaa hapa kwene ze eni gioo zzzz! huku hawajafika bado
 
Kijana Elli kwa wale wafanya kazi wa Serikali ni kweli huwa wanakatwa fedha za kurejesha mkopo huo kwa mwezi.

Nyinyi ambao hamukatwi basi mumebahatika.

Sasa jee munataka bado elimu iendelee kuwa bure hamutaki hata kuchangia kidogo? Serikali itaweeza kukidhi mahitaji hayo kweli?

Enzi zile tulikuwa tunachangia kwa kwenda jeshini na kujenga taifa bure mwaka mmoja, na kupata mshahara kidooooogo sana ambao ulikuwa unatosha kwa chakula tu. Hiyo gari ndiyo ilikuwa unaiona kwa barabarani tu na waliokuwa nazo walikuwa wakieleweka wanafanya kazi gani.

Ndio wastaafu wa enzi zile hawakuweza kumiliki hata nyumba.
 
Ni kweli unachosema ila ninaxhosema ni kwamba, hatukukopeshwa kwani serikali haikopeshi bali ni uchangiaji, that means, serikali na sisi tunachangia... hapo ndo kwene tatizo, kuchangia si vibaya endapo tungekua tunachangia kwa njia inayoeleweka na sikulazimisha kuchangia kiujanja ujanja, mfano; mimi ninalipa P.A.Y.E na makato mengine kwa sera inayoeleweka na si kwa kigezo kwamba nilikopeshwa, serikali hainidai ila labda tunadaiana, au tunadaiwa ndo maana ya cost-share mpwa.

karibu kitimoto mpwa,
 
Katika Kampeni za sasa, ni chama gani kimesema kikiingia madarakani kitawasamehe wale "wadaiwa wa serikali" wa mikopo ya elimu ya juu? Ingekuwa ni hit kubwa.
 
Back
Top Bottom