Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Jana chama cha CUF kimetoa tamko rasmi kuwa hakitashiriki katika uchaguzi wa marejeo tarehe 20 Machi 2016.
CCM chama kikuu chengine Zanzibar kimetoa msimamo wake zamani kuwa kitashiriki, kwa kuona hakina njia mbadala ya kubaki alau kujipa matumaini ya kubaki madarakani.
Vyama vyengine 14 viliobaki havina mvuto kwa wazanzibari, lakini nao pia wanaamini njia ya kurejea uchaguzi unaweza kuvinyanyua vyama hivyo na pengine kuwa mshirika wa SUK baada ya uchaguzi na hasa kuangalia matakwa ya katiba.
1.Wakati CCM itaichukulia kwa tahadhari kubwa kauli ya CUF ya kususia uchaguzi, isije ikapigwa bao, watahakikisha kuwa wanatumia nguvu zote ili ishinde. Hivyo uwezekano wa vyama vyengine vidogo kutoa ushindani wa aina yoyote haupo.
2.CUF kwa kuhofia CCM kupata ushindi mkubwa wanaweza pia kuijtokeza kwenda wingi kupiga kura za MARUHANI kuonesha tu uchukivu wao au kuporwa ushindi wao.
3.Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi uliofutwa na iliotangulia vyama 14 vilivobaki kwa umoja wao havijawahi kupata kura zaidi ya 2,000. Hivyo basi kama uchaguzi utafanyika bila ya CUF ni wazi kuwa CCM watashinda kwa kishindo na nafasi ya pili itashikwa na chama kidogo ambacho mgombea wake atapata kura sizaidi ya 1,000
4.Kwa kukidhi haja ya Katiba CCM kama mshindi wa kwanza itatoa Rais na na Makamo wa kweanza Rais itabidi kwenda kwa mshindi wa pili atakaepata kura sizaidi ya 1,000(projection) na bila ya kuwa na Mwakilishi au diwani hata mmoja!Hivyo Zanzibar itaunda Serikali ya karne ya kioja. Kura yangu inakwenda kwa RUHANI