Marehemu Roy alikuwa anajua sana

Siko na hakika ila nahisi atakuwa mj.

Sina demu kama unavyoniona mpenzi
Ndiyo maana nimekuchagua wewe ukidhi yangu mahitaji
Na siyo kwamba sitaki demu
Ila sijaona mwenye sifa zaidi yako wewe mailka wangu
Dah
Nmekumbuka mbali sana
Enzi za kutoroka shule kwenda club ruaha international iringa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asaiv mim nampenda Black yule jamaaaa yuko Vzr kwa upande wangu
 
MAHMOUD ZUBEIRY
“Hallow, Hi?”ilikuwa sauti nyororo ya mwanadada ikinisalimu, mara baada ya kufika kwenye kiji-soo (grocery) moja eneo la Keko Juu, Dar es Salaam.
Wakati nimetuliza kumbukumbu na kumtazama kwa makini nikidadisi nilikuta naye wapi dada yule, akanipachika swali; “Kama umenisahau vile? Mimi naitwa Enika, tulikutana Habari Corporation, nilikuja kumtembelea Rashid Kejo, tunasoma naye TSJ (sasa IJMC)”.
Naam hapo nilimtambua, wakati huo Enika alikuwa bado hajawa mwanamuziki maarufu. Wimbo wake `Baridi Kama Hili’ ndio kwanza unatoka mwishoni mwa mwaka 2003.
Pembeni yake alikuwa ameketi kijana mmoja mrefu, mweusi na kw amwonekano ni mtaratibu hadi kwenye kuzungumza, Enika akanitambulisha: “Huyu anaitwa Roy, ni kaka yangu, yupo hapa G. Records,”.
Njilifurahi kufahamiana na Roy, kwa muhtasari tangu ile akawa rafiki yangu hadi wa kutembeleana, alikuwa anakuja kwenye ghetto langu yeye na mdogo wake, G-Square kusikiliza nyimbo za Hip hop.
Mimi ni mpenzi wa Hip hop, kadhalika Roy, alikuwa hivyo, hakika tulikuwa marafiki, watani, kwa kipindi kifupi.
Wakati huo, Roy ndio anamtoa kijana Mr. Blue na wimbo wake Blue Blue, tangu hapo nikaanza kuandika kwa wingi habari G. Records.
Nakumbuka wakati fulani wa sakata la Hip hop haiuzi, Roy alisimama kidete kutetea, akisstiza muziki huo unauza, lakini kwa msanii anayeufanya vizuri tu na si mbabaishaji.
Roy alikuwa producer wa ukweli na mara nyingi alipenda kufanya kazi usiku, akiamini ni ndiop kipindi ambachoi akili yake inkuwa imetulia na kufanya kwa uhuru.
Zaidi mchana alifanya marekebisho madogo na kusikiliza kazi alizofanya usiku uliopita, alipenda pombe, huo ni ukweli na tulikuwa tunakunywa naye, wakati mwingine hadi usiku wa manane.
Wakati fulani Ruge Mutahaba wa Clouds FM aliwahi kutuita mimi na Roy: “Nyinyi wabishi mnaiop[enda Hip hop, njooni tuzungumze ili mjue kwa nini Hip hop haiuzi,”.
Tulikwenda na Roy Rozana Bar, Buguruni ambako Clouds FM walikuwa wanafanya onyesho la madansa, Dance la Fiesta, tulibishana kwa hoja, mifano na hali halisi, ingawa hadi tunamaliza kikao, hakukuwa na suluhu, zaidi ya kila mmoja kushikilia msimamo wake.
Roy alikuwa mtu mwenye kumheshimu yeyote, kufanya kazi na yeyote, alichokuwa akichukia yeye ni kitu kimoja tru, dharau, hakupenda dharau hata kidogo na wasanii wengi wenye majina waliokwenda G. Records kifua mbele, alikuwa akiwatoa nishai.
Tulianza kupotezana na Roy baada ya mimi kuhama nyumbani Keko na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea, mitaa ya Sinza. Baadaye naye alitibuana na Dj Gulu au G-Love na kutengana, hivyo kwenda kaunzisha studio yake mwenyewe, G2 ambayo ilipata umaarufu baada ya muda mfupi tu.
Roy alikuwa producer gumzo na kipenzi cha wasanii wachanga, aliwainua wengi kama mmojawapo akiwa ni Matonya, Noorah mbali na Mr. Blue.
Ukiketi kwenye kipindi cha muziki wa Bongo Fleva, nyimbo za G2 zilikuwa zinatawala. Wakati fulani, alimfunika kabisa P. Funk aliyekuwa anaongoza.
Kwa sababu ya majukumu ya maisha, utu uzima tulizidi kupotezan na Roy na tukawa tunaonana mara moja moja, au wakti mwingine kurushiana salamu kwa njia ya simu.
Lakini siku zote niliendelea kumheshimu Roy kwa sababu ya kazi yake, siyo muziki tu, hata matangazo yake ya biashara ni ya kiwango cha juu.
Nakumbuka Roy aliniambia mwaka 1985 akiwa Uingereza alipokuwa anasoma alishiriki mashindano ya kupiga piano na kushinda na tangu hapo akaamua kuwa mtayarishaji wa muziki na matangazo ya Radio na TV kama kazi yake rasmi.
Kabla ya G Records, Roy alikwishafanya kazi Sound-Crafters na aliwahi kurekodi wimbo wake mwenyewe, uliokwenda kwa jina la `Overnight’. Alishiriki pia kutayarisha albamu ya kwanza ya X- Plastaz.
Sina nafasi ya kutosha kumuelezea zaidi Roy, aliyeaga dunia Jumatatu ya Oktoba 6, mwaka 2008 baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu, lakini kwa kiasi kikubwa alikuwa `bidhaa’ adimu kwenye anga za Bongo Fleva.
Buriani Roy Bukuku, Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi, Amin. Hakika Bongo Fleva imepata pigo la kubwa, naongea na wewe ndugu msomaji
 
G - 2 ilikuwa ya kwake roy...mwanzo aliajiriwa G record ya G lover.. pale chang'ombe.. na hit song zote karibu na jina alilipatia G record.. enzi za mr blue anatoka, aby skills, alikiba, bjb, snoop lee, Enika.. wengi nilikuwa nawajua sababu nyumba yetu ilikuwa jirani na G record
Mgulani primary school?
 
Daah!Roy alikua anajua sana
Nadhani sasa tunadili na kizazi kipya mno si kile kilichofanya mziki kipindi kile,nimeusoma huu uzi kwa muda lakini kote naona masifio tu ya third parties/yaani sio wale washriki kwenye game,Nitakayoyasema naomba tusameheane kma nimewakwaza mashabiki wake lkn naongea kma mshiriki kwenye game na ninao uonge ni ukweli kadri niujuavyo mimi.Kifupi jamaa alikuwa ni wa kawaida mno ila kwa kibongo bongo alionekana anajua biti zake loko mno produktion ya kubahatisha ni ile frutloop tu ndo aliyotumia enzi hizo,mi nilishindwa kufanya kazi kwake sabab hakuwana uwezo kipindi hicho ukakaa nae akakusikiliza unavyo floo kisha akakutengenezea biti papo kwapapo alikuwa hawezi hata ana mwanae mmoja ndo alikuwa ana mwachia studio alikuwa hamna kitu,kifupi nilipokwenda nikamsikilizisha masongi yangu na nkataka namna nyimbo yangu biti yake iende kimfumo gani jamaa akachomoa akasema sisi hapa unalipa hela halafu tunakupa biti ambazo tumekwisha zitengeneza unaenda kufanya mazoezi aliponisikilizisha hizo biti ndo nlichoka midundo ile ya loko loko kama biti za majani infact walikuwa wanaigana biti wakati mimi nataka biti classic hata kama si internatn basi zinzofanana ndo tuliposhindwana hapo halafu alikuwa harsh sana,sorry nmeongea nachokijua huu ndo ukweli wangu kama nimewaumiza mashabiki wake si lengo langu bali ni kui balance mizani tu
 
Mkuu enzi hizo ftuity loops ndiyo ilikuwa software available kwa hapa tz na pia vifaa vilikuwa havija advance computer zenyewe pentium ram 1gb, tofauti na sasa.MJ mwenyewe kwenda digital aliwezeshwa na marehemu Rodney motie Mengi.
Nadhani ulimtembelea siku za mwanzo alikuwa hajaweza kuimaster fruity loops baadae akaweza ndiyo maana akina blu walikuwa wanaandika wimbo mpaka melody, ndiyo wanarekodi kwa kuwasikiliza wanaimbaje.
Sasa hivi mambo yamebadilika vifaa vingi, softwares za kumwaga plugins kama zote, youtube ina maknoledge mengi ma producer wanajisomea.
Ndiyo maana unasikia ngoma za s2kizzy ni balaa tupu.
 
Nadhani sasa tunadili na kizazi kipya mno si kile kilichofanya mziki kipindi kile,nimeusoma huu uzi kwa muda lakini kote naona masifio tu ya third parties/yaani sio wale washriki kwenye game,Nitakayoyasema naomba tusameheane kma nimewakwaza mashabiki wake lkn naongea kma mshiriki kwenye game na ninao uonge ni ukweli kadri niujuavyo mimi.Kifupi jamaa alikuwa ni wa kawaida mno ila kwa kibongo bongo alionekana anajua biti zake loko mno produktion ya kubahatisha ni ile frutloop tu ndo aliyotumia enzi hizo,mi nilishindwa kufanya kazi kwake sabab hakuwana uwezo kipindi hicho ukakaa nae akakusikiliza unavyo floo kisha akakutengenezea biti papo kwapapo alikuwa hawezi hata ana mwanae mmoja ndo alikuwa ana mwachia studio alikuwa hamna kitu,kifupi nilipokwenda nikamsikilizisha masongi yangu na nkataka namna nyimbo yangu biti yake iende kimfumo gani jamaa akachomoa akasema sisi hapa unalipa hela halafu tunakupa biti ambazo tumekwisha zitengeneza unaenda kufanya mazoezi aliponisikilizisha hizo biti ndo nlichoka midundo ile ya loko loko kama biti za majani infact walikuwa wanaigana biti wakati mimi nataka biti classic hata kama si internatn basi zinzofanana ndo tuliposhindwana hapo halafu alikuwa harsh sana,sorry nmeongea nachokijua huu ndo ukweli wangu kama nimewaumiza mashabiki wake si lengo langu bali ni kui balance mizani tu
mzee bado unafanya mziki?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom