Marehemu Nyerere Asitumiwe Kisiasa!

Hivi mpaka Nyerere anakufa alikuwa Mwanachama wa chama kipi?Au alirudisha kadi ya CCM?
 
Mkuu Kamundu,

Heshima mbele, naomba kuuliza hivi CCM kwa kufanyia mkutano wake mkuu Butiama, wamemtumiaje Marehemu Mwalimu Nyerere kisiasa?
NANI KAWAZUIA CHADEMA KUFANYA MKUTANO BUTIAMA????MIMI NINANG"ATUKA LAKINI NINAENDELEA KUAMINI BILA CCM MADHUBTI NCHI YETU ITAYUMBA.
 
Ninajua hakika kuwa hairuhusuwi na wala si afya katika JF kujibizana ama kurushiana vijembe.

Lakini sijui wajibu alio nao Nguru Ndoto ni upi?
Kwa haraka najiaminisha kuwa wapo watu hadi leo hawajui sababu kuu za CCM kuwa na nguvu sana dhidi ya vyama vingine vya siasa.

Hili linanifanya nione kuwa hadi mtu anafikia kuingia kwenye Forum kubwa ya kimataifa inayohitaji watu kuwa na uwezo wa kufanya uchambuzi mkubwa wa kina kuhusu mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii eti mtu huyo hawezi kujua sababu mbaya zinazoifanya CCM kuwa chama giant against vingine, basi kazi ya kukomboa fikra za watanzania bado ni mbichi kabisa.

Hebu fikiria daktari ambaye hajui kuwa kidonda kisipooshwa kitaoza anatambia elimu ipi ya uganga. Labda kakaririshwa kuhusu kazi yake ya uganga na ya kuwa hajui ukweli kuhusu bacteria wanavyoshambulia mwili

Nitamwomba mwenyekiti kwa ridhaa yake tuanzishe darasa la MAKUZI YA CHAMA CHA SIASA ili tuepuke kupeleka ulimwenguni hoja za wasomi toka Tanzania zilizofubaa kiasi cha kuidhalilisha elimu ya nchi yetu.

Kwa utambulisho tu "Udogo wa vyama vya upinzani Tanzania ni Ukubwa wa CCM". Labda kwa kurahisisha zaidi hoja hii yangu niseme kuwa SABABU YA KUNAWIRI KWA CCM NDIYO SABABU YA KUKONDA KWA VYAMA VINGINE.

Tuonane majaliwa.
 
Back
Top Bottom