Marehemu Nyerere Asitumiwe Kisiasa!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,325
8,129
Hey guys mimi naona si vizuri kumtumia Nyerere kisiasa. Ni vizuri kumuongelea kwa mazuri lakini kwenda kwenye kaburi lake na kutumia kijiji chake kuweka mipango ya kuwadanganya watanzania kuhusu ufisadi si vizuri. Kitu kingine cha kuangalia ni kwamba CUF na CHADEMA wakitaka kufanya kama CCM je wataruhusiwa? Huu ni wakati wa CCM kubadilika na kuacha kuogopana na kutishia walarushwa laana za Nyerere. Wala rushwa wanatakiwa kufungwa. Vilevile CCM wanatakiwa kuelewa kwamba Watanzania wanabadilika na itakuwa vigumu sana kwa sasa kuficha siri za rushwa kwani dunia imekuwa ndogo sana karne hii. Mimi naomba tuache kumtumia Nyerere kwa siasa, na nimesikitishwa na hatua ya CCM kumtumia mtu aliyefariki.
 
Wao wanasema Nyerere si wetu bali wao wana CCM .Wakimaliza wanataka tuimbe yeye ni Baba wa Taifa sasa sijui wale ambao si wana CCM watamkubali vipi ? Akili zao bwana zimejaa watu kama Kingunge unategemea nini ?
 
Watu wenye hadhi kama ya J.K Nyerere wanapofariki ni heshima na kiswahili fasaha kama neno 'hayati' likatumika badala ya 'marehemu'.
 
Nyerere sio Mwanzalishi wa DP, CUF au CHADEMA ni Mwanzilishi wa CCM, kubali kataa, Nyerer ni mwanasiasa...Nyerere ni mwanasiasa hata iweje..alipinga watu, alifanya kampeni za siasa..

Rais Reagan wa Marekani (1980-88) ni hayati hayupo na anatumiwa kama symbol ya siasa za conservative katika Republican party,hata mdahalo mmoja ulifanyika Reagan Library, California.

Chama sio urai, ni ushindani na sera...Sababu Nyerere ni mwanasiasa, eti Ubaba wa Taifa wake una utata upi..Hizo siasa za kitoto sasa , eti huyu wenu, mnamtumia kisiasa?..why not? they man had Politics damuni, ame inspire politicians, mahiri wa kutoa hoja na kuchana opponents wake.. wewe na Key-board na Mouse unamuona Kingunge hafai, wazazi wenu, babu zenu walikuwapo, mbona they didnt stand out zaidi ya Ngombale-Mwiru..Siasa ni competition, if you want a friend in politics, get a dog
 
Unatarajia nini Mwenyekiti anapokuwa na wasaidizi kama hawa, zaidi ya kuambiwa Nyerere ni wetu (CCM) na wala sio wenu!!Wahenga walisema "Utu uzima dawa" lakini hapa mi nakataa. Kwa umri huu watawezaje kupambana na "RA, Edo, Karag, ..."

CCM imebaki kuwa kama ZanuPF!!

img8983xy5.jpg
 
Attachments

  • IMG_8983.jpg
    IMG_8983.jpg
    159.8 KB · Views: 67
Unatarajia nini Mwenyekiti anapokuwa na wasaidizi kama hawa, zaidi ya kuambiwa Nyerere ni wetu (CCM) na wala sio wenu!!Wahenga walisema "Utu uzima dawa" lakini hapa mi nakataa. Kwa umri huu watawezaje kupambana na "RA, Edo, Karag, ..."

CCM imebaki kuwa kama ZanuPF!!

WRONG, Dead Wrong...CCM siyo kama Zanu PF, wameshinda chaguzi karibu zote in modern time, toka 1992 wanashinda, hata useme wanaiba, wanashinda mpaka udiwani...

Everybody loves a winner, ThINK BIG dont whine...Nafasi katika chama ni ushindani, hao wote uliotaja waliwahi kuwa kwenye dog house ya chama kwa wakati mmoja au mwingine...Mnaongea utafikiri CCM inakufa Jumanne vile..

CCM siyo timu ya soka, cricket wala kikapu, game yao iko kwenye siasa za Bongo, vijijini, udiwani n.k, helikopta, kanga, T-shirt,Pilau Chang'aa , everything siasa za Bongo, na score katika chaguzi iko hivi (nikumbushe)

CCM 3- Wapinzani 0 toka vyama vingi vianze...

Siasa sio medicine, nawa mikono kila dk 5,Wachukie CCM, lakini wanashinda...KANU, ZANU-PF hazishinda..CCM Wins
 
Nyerere sio Mwanzalishi wa DP, CUF au CHADEMA ni Mwanzilishi wa CCM, kubali kataa, Nyerer ni mwanasiasa...Nyerere ni mwanasiasa hata iweje..alipinga watu, alifanya kampeni za siasa..

Rais Reagan wa Marekani (1980-88) ni hayati hayupo na anatumiwa kama symbol ya siasa za conservative katika Republican party,hata mdahalo mmoja ulifanyika Reagan Library, California.

Chama sio urai, ni ushindani na sera...Sababu Nyerere ni mwanasiasa, eti Ubaba wa Taifa wake una utata upi..Hizo siasa za kitoto sasa , eti huyu wenu, mnamtumia kisiasa?..why not? they man had Politics damuni, ame inspire politicians, mahiri wa kutoa hoja na kuchana opponents wake.. wewe na Key-board na Mouse unamuona Kingunge hafai, wazazi wenu, babu zenu walikuwapo, mbona they didnt stand out zaidi ya Ngombale-Mwiru..Siasa ni competition, if you want a friend in politics, get a dog

Nyerere ni wa CCM na ame inspire wanasiasa wengi . Mbona CCM hajapatikana hata mmoja kama Mwalimu akaokoa hii Nchi yetu ? Wewe Nguru Ndoto una matatizo sana .
 
Umekosea kuuliza swali..Nyerere na Karume wameanzisha CCM, hiyo ni historia..ubishi hamna hapo.

Nyerere ni Mwanasiasa, Mwalimu pia..Ubishi haupo. Unayedai ukombozi au uokoaji upi? kumpenda au kutompenda Kikwete ni haki yako na maoni yako..Makundi CCM yapo,kwa sababu upinzani upo ndani ya chama lakini,, nisikilize... hata mgogoro uwe vipi within CCM, kwenye chaguzi, Kiteto, na wapi, ushindi huwa zaidi kwa Chama cha Mapinduzi..na hata useme nchi inahitaji uokoaji, sidhani kama watu wote CCM wanajisikia kama wewe..Wengine hawafurahii sababu ya kudhofika kisiasa na kupiga kelele, wapinzani wanafikiri hiyo gari ya ku-magnify kelele na tofauti za chama ni gari la ushindi..Halina mafuta gari hilo, Chalinze empty tank, ikija Kampeni za uchaguzi, CCM itashinda kwa kiwango kikubwa, uokoaji ni kwamba wapinzani hawajaweza kuchukua talent za wanasiasa walioko CCM kuwasaidia, wachache walikuja wakarudi baada ya mikutano ya NCCR Tanga, ugomvi ambao ni tofauti na wa CCM..Physical altercation nini..uokoaji ni broad sana.kupi haswa

Tanzania ni kubwa, CCM ni kubwa ina watu wengi, wanasiasa na sasa hata wafanyabiashara,ni wengi, chama ni kikubwa, tofauti zitakuwepo tu, wapinzani tatizo kuu ni njaa ya kifedha ni mzigo kwao kisiasa, inaeleza kwanini matatizo ya Pesa kama EPA yamekuwa hoja isiachwa hata dakia 1.

Nyerere ame inspire wanasiasa wengi tu, wengi anawajua--Akina Kambona walijiona wana akili zaidi yake hawakuzalisha chama chochote imara zaidi ya CCM ya Nyerere na Karume (Historia)

Sasa hata mwanasiasa kama Nyerere bado ni Baba wa Taifa,,,hilo nalo halina ubishi.
 
acha kukazania siasa za vyama wewe, kosa la Ngurudoto ni kwa nini CCM haijatoa kiongozi kama nyerere ? you better be kiding. Viongozi hawatengenezwi bana ! Mbona vyama vya upinzani pia hata havijadiriki kutoa kiongozi kama nyerere ambaye ametoka ccm na kuiokoa nchi (kama ulivyosema)? ccm did, how about wapinzani ?
 
Mkuu Kamundu,

Heshima mbele, naomba kuuliza hivi CCM kwa kufanyia mkutano wake mkuu Butiama, wamemtumiaje Marehemu Mwalimu Nyerere kisiasa?
 
Tunaposema Nyerere ni "Baba wa Taifa", tunamaanisha ni mwasisi wa Taifa hili (yaani Tanzania) na wala si Baba wa Taifa kutokana na kuwa mwanzilishi wa chama (yaani CCM). Ndio maana inapotokea mtu (ama kiongozi) yeyote anayesema Nyerere ni wetu na sio wenu, tunamshangaa kwani sisi ni wa Taifa gani?? Nenda Rwanda, Burundi uwaambie Nyerere ni wetu, watakuelewa lakini sio Tanzania kwa waTanzania!!

Unapozungumzia siasa za Rais Reagan, unakosea yeye si Baba wa Taifa la US kwahiyo yeye ni lazima atumike kwenye siasa, kama ilivyokuwa hapa kwetu kumtumia Mkapa (kuwa ni wa CCM) hilo tunalikubali. Fuatilia history ya US!! Kuna mtu anaitwa Washington, George (1789 - 97).

Kingung'e akituambia Mkapa si wetu huyo tunamkubalia (huyu ni kizazi cha CCM!) na ndio maana sasa amegeuka kuwa "sio mwanasiasa"
 
Unatarajia nini Mwenyekiti anapokuwa na wasaidizi kama hawa, zaidi ya kuambiwa Nyerere ni wetu (CCM) na wala sio wenu!!Wahenga walisema "Utu uzima dawa" lakini hapa mi nakataa. Kwa umri huu watawezaje kupambana na "RA, Edo, Karag, ..."

CCM imebaki kuwa kama ZanuPF!!

img8983xy5.jpg

Do you need to say more? You can see what is happening... ... ...
 
Mkuu Kamundu,

Heshima mbele, naomba kuuliza hivi CCM kwa kufanyia mkutano wake mkuu Butiama, wamemtumiaje Marehemu Mwalimu Nyerere kisiasa?

Mkuu Field Marshall ES,

Usiwe na shaka wengine ni wale wa lile kundi moja ulilosema siku ile... Ati Nyerere asitumiwe kisiasa wakati ni Model wa Kisiasa...

Ama kweli Jahazi linaenda Mrama, ni Utaelezea vipi Siasa za Tanganyika/Tanzania/Afrika, TANU,ASP,CCM na Siasa za Ujamaa duniani bila kumtaja nyerere.

Ikimbukwe kwamba kuna wakati Nyerere alishaona chama chake CCM hakiendi vizuri lakini hakua amejitoa CCM mpaka mauti yalipomfikia...

Sasa leo ati Atengwe na Siasa za CCM. ama kweli Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni.
 
Tunaposema Nyerere ni "Baba wa Taifa", tunamaanisha ni mwasisi wa Taifa hili (yaani Tanzania) na wala si Baba wa Taifa kutokana na kuwa mwanzilishi wa chama (yaani CCM). Ndio maana inapotokea mtu (ama kiongozi) yeyote anayesema Nyerere ni wetu na sio wenu, tunamshangaa kwani sisi ni wa Taifa gani?? Nenda Rwanda, Burundi uwaambie Nyerere ni wetu, watakuelewa lakini sio Tanzania kwa waTanzania!!

Unapozungumzia siasa za Rais Reagan, unakosea yeye si Baba wa Taifa la US kwahiyo yeye ni lazima atumike kwenye siasa, kama ilivyokuwa hapa kwetu kumtumia Mkapa (kuwa ni wa CCM) hilo tunalikubali. Fuatilia history ya US!! Kuna mtu anaitwa Washington, George (1789 - 97).

Kingung'e akituambia Mkapa si wetu huyo tunamkubalia (huyu ni kizazi cha CCM!) na ndio maana sasa amegeuka kuwa "sio mwanasiasa"

Sasa hawa ni watu walewale, au akisema Nyerere si wenu hujui kuwa anamaanisha kisiasa?..uoga uliopindukia sasa..NCCR au TLP ina haki ya kumkumbatia Mrema kama ambavyo CUF kumkumbatia Seif Sharif Hamad...CCM inaweza kukumbatia Nyerere kisiasa, na Mwinyi na Mkapa na Kikwete..hao ni CCM.

Think Big always, Reagan ni Mwanasiasa Republican na George Washington wa Marekani ni Baba wa TAIFA LA Marekani "Muasisi", nae ni mwanasiasa..Reagan ni Republican atatumiwa kisiasa kama Nyerere ukizingatia umri na kizazi cha Reagan na Nyerere ni sawa vs George Washington 18th centuary..George Washington ni mwanasiasa wa Federalist Party ambacho kilipata ushindani kushinda pia.Siasa ni ushindani na Sera.dhambi ya siasa na ubaba wa Taifa haupo!!
 
Unatarajia nini Mwenyekiti anapokuwa na wasaidizi kama hawa, zaidi ya kuambiwa Nyerere ni wetu (CCM) na wala sio wenu!!Wahenga walisema "Utu uzima dawa" lakini hapa mi nakataa. Kwa umri huu watawezaje kupambana na "RA, Edo, Karag, ..."

CCM imebaki kuwa kama ZanuPF!!

img8983xy5.jpg

AGALIA NYUMA, I SEE PEOPLE, REAL PEOPLE...WAPINZANI <<<<< PEOPLE..

MUULIZE MGOMBEA URAIS WA MAREKANI MICHAEL DUKAKIS (1988), USITUMIE PICHA KWENYE SIASA..IT MAY GO AGAINST YOU..

I SEE PEOPLE HATA BUTIAMA,,SIASA NI WATU
 
Sijui unaposema asitumiwe kisiasa una maanmna gani wakati alikuwa mwanasiasa, mwenyekiti wa CCM na supposedly baba wa taifa.

Ukiniambia Nyerere asitumiwe kupotosha au ku spin nitakubali.Lakini kumtumia Nyerere kisiasa ni halali sio tu kwa CCM baloi hata wapinzani.Usikatae wito, kataa neno. Usikatae Nyerere kutumika kisiasa, kataa Nyerere anavyotumiwa kisiasa.

Be specific please.
 
Textbook politics, kwenye katiba na pretentious documents zingine kama hizo.

Tunazungumzia ideals na siyo kinachotokea.Siasa zisizo spin is an illusion to be pursued but never attained.
 
Umekosea kuuliza swali..Nyerere na Karume wameanzisha CCM, hiyo ni historia..ubishi hamna hapo.

Nyerere ni Mwanasiasa, Mwalimu pia..Ubishi haupo. Unayedai ukombozi au uokoaji upi? kumpenda au kutompenda Kikwete ni haki yako na maoni yako..Makundi CCM yapo,kwa sababu upinzani upo ndani ya chama lakini,, nisikilize... hata mgogoro uwe vipi within CCM, kwenye chaguzi, Kiteto, na wapi, ushindi huwa zaidi kwa Chama cha Mapinduzi..na hata useme nchi inahitaji uokoaji, sidhani kama watu wote CCM wanajisikia kama wewe..Wengine hawafurahii sababu ya kudhofika kisiasa na kupiga kelele, wapinzani wanafikiri hiyo gari ya ku-magnify kelele na tofauti za chama ni gari la ushindi..Halina mafuta gari hilo, Chalinze empty tank, ikija Kampeni za uchaguzi, CCM itashinda kwa kiwango kikubwa, uokoaji ni kwamba wapinzani hawajaweza kuchukua talent za wanasiasa walioko CCM kuwasaidia, wachache walikuja wakarudi baada ya mikutano ya NCCR Tanga, ugomvi ambao ni tofauti na wa CCM..Physical altercation nini..uokoaji ni broad sana.kupi haswa

Tanzania ni kubwa, CCM ni kubwa ina watu wengi, wanasiasa na sasa hata wafanyabiashara,ni wengi, chama ni kikubwa, tofauti zitakuwepo tu, wapinzani tatizo kuu ni njaa ya kifedha ni mzigo kwao kisiasa, inaeleza kwanini matatizo ya Pesa kama EPA yamekuwa hoja isiachwa hata dakia 1.

Nyerere ame inspire wanasiasa wengi tu, wengi anawajua--Akina Kambona walijiona wana akili zaidi yake hawakuzalisha chama chochote imara zaidi ya CCM ya Nyerere na Karume (Historia)

Sasa hata mwanasiasa kama Nyerere bado ni Baba wa Taifa,,,hilo nalo halina ubishi.

ubishi upo tena mkubwa. mkuu historia huijui, bora baadhi ya wakati kusoma au kuuliza wenye kujua.

ccm haikuasisiwa na hayati mzee karume na marehemu nyerere.

hayati mzee karume aliuwawa na wapinga mapinduzi mwaka 1972 pale makao ya afro shirazi, wakati huo alikuwa rais wa afro shirazi na si mwenyekiti wa afro shirazi(walikuwa hawatumii mwenyekiti, mwenyekiti lilitumika kwenye baraza la mapinduzi)

ccm ilizaliwa mwaka 1977 miaka mitano baada ya kifo cha hayati karume na wakati huo rais wa asp alikuwa ni mzee wetu Aboud J Mwinyi.

sasa tuseme waanzilishi wa suala hili walikuwa ni mwalimu nyerere alileta wazo hili ktk kikao alichoalikwa cha ASP makao makuu kiswandui na kutoa wazo hilo na hatajina alilitoa yeye na kwa upande wa zanzibar walikuwapo watu kama hayat SH Thabit Kombo kina na Nassor moyo, Mtoro Rehani kingo, washoto na wengineo na ASP ilifata taratibu za vikao vya chama kuchukua ushauri wa kuunganisha vyama kama ambvyo TANU ilifanya.

jitahidi kusoma kwanza kaka.

na hii ndio raha ya JF tuko watu wa sehemu mbali mbali na uelewa mbali na ndio inayoifanya JF kua makini
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom