Marehemu Mbunge wa Muhambwe(Kigoma), Atashasta Nditiye alipata ajali lini na wapi?

KARIBU MTAKUWA VICHAA YAANI SERIKALI ITOE TAARIFA YA UONGO KUWAFURAHISHA VICHAA KAMA WEWE KAMA HUKUPATA HABARI NI WEWE NA KAMA HUAMINI NENDA KAMUULIZE MKE WAKE NA WABUNGE WENZIE MUWE NA AKILI HATA ZA KUPANGA POST
Jifunze kuandika; kuandika Sentensi nzima in Caps inaonesha IQ yako ni ndogo sana
 
Mabunge yaliyopita wabunge wa upinzani hususani Chadema walikuwa mstari wa mbele kudadisi na kuujulisha umma pale sintofahamu yoyote inapotokea, anasema mzee Mgaya.

Hebu fikiria mbunge anapata ajali Dodoma tena imehusisha gari tatu na pikipiki na zote zimekokotwa hadi polisi lakini wapiga kura wake na wananchi hawapati taarifa? Anauliza Mgaya.

Hata PM mh Majaliwa amesikitika sana kwa serikali kutotaarifiwa juu ya ajali hiyo na hata wapiga kura wake ambao wangeweza kumuombea badala yake wanaarifiwa tu msiba tena baada ya wabunge wa CCM kuanza kuhoji yuko wapi mwenzetu Nditiye?

Mzee Mgaya anaomba udhaifu huu uliotokea kwenye ofisi ya Katibu wa bunge usijirudie tena.

Mgaya anamalizia kwa kusema " Tumeanza kuwakumbuka akina Mnyika "

Maendeleo hayana vyama!
 
Wahenga walipata kusema "Shetani akizeeka hujigeuza na kuwa Malaika"

Hivi huyu Mzee si ndiyo alikuwa anafurahia zile 99% za kijani kule Bungeni?? Leo hii tena ameona umuhimu wa wapinzani Bungeni??
Wabunge wenyewe ndiyo akina Babu Tale 😀😀

Ndiyo kwanza 2021 hadi tufike 2025 tutaona mengi
 
Back
Top Bottom