Marehemu Mbunge wa Muhambwe(Kigoma), Atashasta Nditiye alipata ajali lini na wapi?

Requal

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
872
1,000
Habari za jioni wakuu

Nimeona taarifa za msiba za huyu mheshimiwa naibu Waziri wa zamani na sababu ya kifo chake imeelezwa ni ajali..

Binafsi sijawahi hata kuona picha wala hababri kuhusu hii ajali yake inayotajwa kuondoa uhai wake, hii ni ajali kweli au ni futa linatumaliza huku tukificha ukweli?

Hivi inawezekanaje Mbunge na Naibu waziri wa zamani apate ajali alazwe siku mbili tena katikati ya jiji la Dodoma halafu habari zake zisisambae wakati RAS tu wa ARUSHA zilisambaa within a second

Mwenye angalau picha ya ajali yake aweke hapa.

Haiwezekani mtu mkubwa kama yule apate ajali halafu asiwepo wa kujua

Mnakumbuka wakati ule Mh Chenge alipomgonga Mtu wa Bajaji usiku wa manane lkn muda ule ule habari ilifika humu jamvini na vyombo mbalimbali vya habari?
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,064
2,000
Haiwezekani kiongozi wa umma anapata ajali halafu wananchi hawapewi taarifa , hii nchi inao wenyewe ambao ni sisi wananchi , hapa ni lazima Spika Ndugai na wenzake watoe maelezo ya kutosha ili waeleweke , au la tuambiwe ajali ya Nditiye ni ya kuanguka bafuni ambako si rahisi watu kuona , lakini vinginevyo hakuna ajali yoyote ya barabarani ambayo ni ya siri .

Juzi Katibu Tawala wa Arusha amefariki kwa ajali lakini tumeonyeshwa hadi gari alilopata nalo ajali lilivyoharibika , na tukaelezwa alikuwa anatoka wapi na kuelekea wapi , huyu mnayetaka kuficha ajali yake ametenda kosa gani ?

Rais wa Tanzania Dr Magufuli aliwahi kusema kwamba Watanzania siyo Wajinga sana .

Tuambiwe ukweli ili tuelewe
 

Englishlady

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
2,177
2,000
Duuu

Sasa tunalazimisha kila kifo ni kushindwa kupumua.

Tunahoji hadi ajali?
Tunapata faida gani tukisema tunakufa kwa Corona?

Kwani hamkusikia Magu? Kwamba waliopata chanjo ndio wameleta corona ya ajabuajabu? Na akasema hatafanya lockdown.

Mnataka awaambie mlale majumbani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom