Marehemu Hanter Lyamuya kuagwa Leo jumapili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marehemu Hanter Lyamuya kuagwa Leo jumapili.

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Gang Chomba, May 9, 2010.

 1. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Siku za Mwanadamu za kuishi hapa duniani zinahesabika...

  Kwa wale woote wanaomfahamu Uncle wetu huyu ambaye alikuwa anafanya kazi katika kampuni moja ya clearing & forwading basi mnaarifiwa kuhudhuria Ibada ambayo itaambatana na kuaga Sura ya Marehemu katika kanisa la Lutheran hapa Muhimbili kuanzia saa 6 mchana wa jumapili hii ya tarehe 09/05/2010.

  Marehemu Hanter alifahamika na wengi kutokana na upendo aliokuwa nao kwa wanadamu, kuwa mkweli na muwazi, mwepesi wa kuomba msamaha pindi anapomkwaza binadamu mwingine, mpole, mkarimu, asiyependa sifa na makuu, aliyekuwa mstari wa mbele kutetea haki, aliyepambana mpaka mwisho ktk kuhakikisha wanyonge wanapata wanachokistahili.

  Na weengi watamkumbuka Uncle Hanter kwa kuwa na moyo wa kuwafundisha wageni kazi zinazohusu maswala hayo aliyokuwa anadili nayo.

  Mwenyezi Mungu alimchukua mpendwa wetu huyu Baada ya kuugua maradhi ya Figo na Moyo.

  Na hapa ndipo tunapokumbushwa kuwa hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kuhesabu nywele za kichwa chake.

  basi pia hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kukwepa umauti. Cha msingi tumuombee ili apumzike kwa amani milele Daima.

  NB: nasi tujisogeze mikononi mwa muumba, kwani hatujui siku wala saa tutakayopoteza pumzi na kuaga Dunia.
   
Loading...