Elice Elly
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 1,268
- 1,593
Mara kwa mara vijana wa CCM waliomwagwa mitandaoni kupiga propaganda kuwa Chadema imekufa inaonekana wazi wanapata tabu sana baada ya kuona malengo yao hayajatimia.
Lengo la CCM ilikuwa ni kuona Chadema imekufa kabla ya 2020, na mpaka sasa kwa kujifurahisha wanawasadikisha wale walio watuma kuwa Chadema imekufa japo wanajua wazi kuwa Chadema ina nguvu sana na IPO imara sana.
Ili kuwafurahisha wale waliowatuma,vijana wa CCM wamekuwa na mikakati nchi nzima kupita kuweka bendera za CCM maeneo ya bara barani na maeneo mengine mbali mbali ili wale walio watuma wakiona bendera nyingi za CCM waamini kuwa Chadema sasa imekufa.Mikakati hii inafanya hasa miji ambayo CCM hawakubaliki.
Lakini baada ya kuona Zoezi la kuiua Chadema ni gumu sana,sasa wameona watumie mbinu mpya japo siyo mpya yaani kumpiga Mchungaji na kondoo watawanyike,kitu ambacho hawatafanikiwa.kuna mbinu hii ya kumchafua M/kiti wa Taifa wa Chadema Mh.Mbowe lakini yote ni katika jitihada za kuiua Chadema. Hili nalo halitafanikiwa kwa sababu Chadema ni chama cha zama Hizi. Ni sawa na kijana wa sasa umlazimishe kuuupenda Muziki wa zamani wakati zama Hizi ni zama za Muziki wa kisasa.
Hivi wanapaswa kutambua kuwa pamoja na nguvu zote wanazotumia ni ngumu kuwabadili vijana wapende msondo ngoma (CCM) wakati wanajua kuna Muziki wa sasa (Chadema): hivi niwasihi kumtesa Mbowe,kumfungulia kesi,kumuharibia Biashara zake,kumtengenezea kashfa mnazo zijua nyinyi hakuwezi kubadili kizazi hiki.
Nashauri tumieni nguvu nyingi kujenga umoja wa kitaifa na siyo kutumia nguvu na gharama Kubwa kwaajili ya kuibakiza CCM madarakani. CCM haiwezi kubaki madarakani kwa gharama ya kuwafunga akina Mbowe, kuharibu Biashara zao,kuwatengenezea kashfa za ajabu ajabu nk.Mtawafanyia hayo yote lakini ni ngumu kukibadili kizazi hiki.
Sent using Jamii Forums mobile app