Marehemu Dr. Mgimwa alikuwa ni kiongozi asiyependa kujilimbikizia mali, hapa ndipo nyumbani kwake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,860
5,801

[h=2]THURSDAY, JANUARY 2, 2014[/h][h=3][/h]

Hapa ndipo nyumbani alipozaliwa na alipokuwa akiishi aliyekuwa waziri wa fedha na mbunge wa jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa na ndipo atazikwa hapa
Hii ndio nyumba ya waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa iliyopo jimboni Kalenga ambako ndipo alipozaliwa ikiwa na bendera ikipepea nusu mlingoti

Hii ni nyumba anayoishi mama yake ambayo ipo jirani na yake

Wanachama wa CCM wakibadilisha bendera nyumbani kwa aliyekuwa waziri wa fedha jioni ya leo .usikose kujua habari zaidi kesho juu ya maisha ya waziri Dr Mgimwa. Picha na Francis Godwin

MICHUZI

hebu tuonyeshe na zile za huku dar sasa.maana nyumbani inaweza kuwa hivyo ila huku sasa ana majumba ya maana

Usiseme kitu ambacho hauna uhakika nacho. Hizo za Dar ungetuonyesha wewe maana umesema kwa uhakika inaonekana unazijua.

RIP.WAZIRI
 
Wewe ni mwongo, Marehemu kujenga Kalenga, nenda katupigie picha nyumba yake ya kalenga utulete

Asili ya Marehemu ni kiponzero, watu wa huko huwa ni selfish hawana hulka ya kurudi na kuendeleza makawao
 
Prove US WRONG Men...
 
hata mramba kijijini kwake nyumba ya kawaida lakini huko tegeta nasikia anamiliki mtaa tena mijengo ya ghorofa,nani hajipendi?

wewe umefika kijijini kwa Mramba?...........na hii tabia ya "nasikia" sio nzuri sana
 
Kumbe watu aina ya Nyerere walikuwepo. RIP WAZIRI

Mmh kwangu mi najiuliza alikuwa akipeleka wapi fedha? Maana alishawahi kufanya kazi benki ya NBC kama manager na hatimaye mkurugenzi, then akaenda chuo cha benki kuu mwanza, diwani wa CCM, Waziri wa fedha! Vp ashindwe kujenga nyumba ya maana aishi kwenye vibanda hivyo kama vya shamba boys? Hata siamini, na ninaanza kuwa na wasiwasi hata na aina ya ugonjwa uliomuua.
 
Kiongozi makini huyu. Watu aina ya mwalimu hawapendwi na viongozi nchi hii. Ndio maana hata huko SA alikuwa akijitibu mwenyewe.
 
Kumbe bado tulikuwa na viongozi wachache Wajamaa wa ukweli, walimuishi Nyerere kwa maneno na matendo!.
Kwa maisha haya hapa duniani, huyu jamaa ni Mbinguni Moja kwa Moja!.
RIP Dr. Mgimwa!.
Pasco.

Awali ya Yote Nami niungane na wale wote waliotoa pole kwa familia ya Marehemu Dr.William Mgimwa kwa kupoteza Nguzo yao muhimu katika familia. Pia natoa pole kwa watanzania wenzangu wote kwa kumpoteza kiongozi wetu.

Ningependa kutoa ushuhuda wangu juu ya Dr Mgimwa kwamba alikuwa mtu mnyenyekevu, muadilifu na mchapakazi hodari. Wakati wa uhai wake, hakuwa mtu wa kujikweza wala kuyavaa madaraka makubwa aliyokuwa nayo. Alikuwa muumini wa msingi mkuu wa TANU kwamba "cheo ni dhamana"

Kwa wale wanaoifahamu hazina vizuri, ile waiting room ya Waziri siku zote imekuwa ikijaa wageni wenye asili ya asia na wengineomkwa ajili ya kutafuta favours mbalimbali.....ilikuwa hivyo kwa mawaziri wengi waliopita Hazina. Lakini alipokuja Dr Mgimwa,watu wale walipotea kabisa, kwasababu walimjaribu na kupata habari yao- Dr Mgimwa alisimamia sheria,taratibu na haki. Hivyo kijiwe kile kikawa kichungu kwa watu wa dili na mishen mjini.

Mawaziri wenzake watakuwa ni mashuhuda, ilikuwa ukienda kwake kumuomba akusaidie kupata bajeti kwa ajili ya shuughuli za wizara yako pale ilipokwama- alihakikisha hauondoki ofisini kwake mpaka jibu la uhakika limepatikana. Hata kama jibu lenyewe lilikuwa negative, ungeondoka pale umeridhika kabisa kwani alihakikisha unaelewa fika sababu za msingi za kuchelewa pesa za wizara yako. Lakini alikuwa haishii hapo, aliendelea kufuatilia mpaka afanikishe jambo lako na lazima angekupa mrejesho.

Vilevile watumishi wa Hazina watakuwa mashuhuda Mzee Mgimwa alikuwa anaheshimu mtu mkubwa na mdogo, hakujali cheo, jinsia au umri uliokuwa nao. Aliheshimu zaidi utu,weledi, na mchango wa mtu kwenye kufanikisha majukumu ya taasisi. Hakuyumbishwa na mtu yoyote hata Wahisani ambao walizoea kudictate matakwa yao kwa Serikali. Alikuwa very calm na msikivu na kisha alirespond kwa kila hoja kisayansi mpaka unamkubali.

Ilipokuja kwenye matumizi ya rasilimali za umma, mzee Mgimwa alionyesha mfano wa uadilifu. Mfano wakati anateuliwa kuwa Waziri wa Fedha, alipewa Manaibu Waziri Wawili tofauti na ilivyokuwa kabla ya uteuzi wao ambapo kulikuwa na Naibu Waziri Mmoja. Hivyo,kulikuwa na shortage ya gari moja lenye hadhi ya kumbeba Waziri. mhe Mgimwa aliamua gari alilokuwa anatumia Waziri wa Fedha (Mhe Mkulo) VX-V8 apewe mmoja wa Manaibu wake. Lakini hakuishia hapo, akawakataza watendaji wasipoteze fedha kununua gari jipya la Waziri, bali apewe moja ya pool cars za pale Wizarani- ndio kisa cha Dr Mgimwa toka ameteuliwa mpaka alipofariki alikuwa akitumia Landcruiser Standard nyeupe ambayo kwenye wizara nyingine hata Wakurugenzi hawapandi kwasababu wanaona hazina hadhi. Lakini si hivyo tu,matumizi yake ya gari la Serikali yalikuwa pale tu alipokuwa na shughuli za Serikali tu. Mara zote Jioni na weekends alipokuwa na shughuli binafsi kama vile kwenye vikao vya wana Kalenga, Harusi, Misiba n.k alikuwa akijiendesha mwenyewe kwenye gari lake binafsi Jeep Cherokee nyeupe. Mara ya mwisho nilimkuta Shopaz Plaza akijifanyia shopping mwenyewe, akibeba mizigo yake mwenyewe, akijiendesha mwenyewe.

Kwa hakika Marehemu Dr.William Mgimwa alikuwa kiongozi wa mfano. yapo mengi ya kujifunza kutoka kwake.
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Dr.William Mgimwa,Mahala Pema Peponi.
 
People should be able translate their education and earnings into quality of their lives and those around them(parents,and others) I see use of firewood and lack of water there....I would expect better from him with all that he had.
 
aliyekuwa anasema huyu mzee mzigo ni nani,na tena aliongelea songeaaaaaaaaa,
 
Back
Top Bottom