Marehemu ananiuliza kama naweza sasa hivi

strategist22

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
656
594
Nakumbuka kama ni jana japo miaka zaidi ya minne imepita, tangu rafiki yangu alipo umaliza mwendo, naamini yuko mahali salama maana alikuwa mtu poa sana.

Ni mtu tuliefahamiana toka vidudu, tumecheza cha ndimu wote tumesoma primary moja tumeshinda wote muda mwingi. Mara kwa mara tumeadhibiwa pamoja kwa kufanya ukorofi mtaani au shuleni.

Tulipo maliza kidato cha nne, akaenda Dar kwa kaka yake, uliendelea kuchati na kupigiana simu. Mimi nikabaki kijijini kwetu nipo nipo tu.

Jamaa kaka yake alisoma mambo ya information technology, jamaa yangu muda wote huo alitumia kujifunza computer maintenance, alikuwa ananisimulia tu anaweza kufanya repair ya hardware na software nasikia tu kwake kuna window hard disk. Hata sijawahi kufikiria vinafananaje. Maana hata computer nilikua naziona stationery tu huko.

Mimi nilienda advance yeye alienda chuo kusoma diploma .Niliporudi baada ya kumaliza kidato cha sita nilikutana naye nyumbani anaumwa .

Tulikuwa tunapiga stori sana, alinipa mwanga wa huko chuo nakotegemea kwenda. Alikuwa anapenda nijifunze basic computer maintenance aliniambia nikiwa vizuri nikiwa chuo nitaweza kupata pesa ndogo ndogo za ufundi .Tukaanza kujifunza,kwa theory kidogo na vitendo. Lakini kila muda ni akitaka tusome nasema tuanze kesho tuanze kesho, baadae, baadae. Nilizani tunao muda mwingi,na kesho sikuiona kufika

Siku ya mwisho tulipiga sana stori juu ya maisha huko chuo alisisitiza sana nijitahidi katika hicho anachonifundisha na tujitaidi kugusa vitu vingi vya muhimu lakini hadi amemaliza mwendo alinifundisha hardware tu nayo nishasahau saivi. Siku hiyo ya mwisho tuliagana saa nne asubuhi nilijiimu shamba, taarifa ya msiba ilinikuta huko machozi yalianza kumwagika, mwili ulikufa ganzi.

Toka hapo nikajifunza na hadi sasa najifunza wakati uliokubalika ni sasa, hakuna wakati mwingne tunaoweza kuanza kazi yetu njema itakayotufanya tuwe na maisha ya kufana.

Mwisho sikufanikiwa kwenda chuo ,hadi leo computer maintenance ni hadithi kwangu, kingereza ni mtiani mzito pia hayo yote jamaa alinisisitiza sana.

Tatizo lipo hapa mara nyingi huwa naota nipo naye tunapiga stori maeneo yaleyale tuliyopenda kukaa, hasa kwenye kivaranda chetu ,lakini mambo ambayo naongea naye ni yale yale computer, kingereza, chuo , lakin Mimi huwasichangii kitu chochote. Siku moja niliota ana niuliza umeweza saivi kutengeneza computer yangu?

Kuna laptop alinipa , ilikuwa mbovu haiwaki Kwa ajili ya kujifunzia ,vifaa vya ndani na vinavyokaa na kazi yake na kama vina shida unagunduaje na unafanyaje marekebisho. Nachokumbuka hapa zaidi ni processor na processor fen. Kabla sijamjibu anachouliza huwa ninashtuka ,imenitokea hivi zaidi ya mara nne. Laptop nilimkabidhi baba yake baada ya msiba.

Mwanzo nilipowasimulia nyumbani wakaniambia ,kawaida unamfikiria sana ,na pia hiyo hali itapita tu ,lakini hadi leo huwa na muota ,sio kila siku. Wengine waliniambia ni roho ya mauti imekuandama kemea la utakufa na wewe karibuni ,rafiki yako anakuita kuzimu ,mkemee sana.
Hakuna mfu aneye rudi tena , wengine wananiambia anaujumbe anakupa.

Kwa wataalamu wa mambo mengi nisiyoyafahamu haya yanayodaiwa kuwa ya kufikirika ,nawaomba mje mnisaidia hii ndoto huwa na maana ipi maana tuna kuwa maeneo yaleyale ,stori zilezile Ila Tu Mimi huwa sichangii chochote.Ni kama ndoto Tu za kawaida? au ni zaidi ya ndoto za kawaida? Nifanye nini katika hali kama hii?


Shukrani sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna babaangu mlezi alikuwa Bwana mifugo alikufa kwa ajali ya piki piki usiku wa saa mbili mwaka 2012 nikiwa chuo mwaka wa pili! Nilimwacha nikienda chuo mwaka 2010! Nilimkataza asimuoe mama mmoja hivi ambae nilikuwa na mashaka nae! yeye alimuoa baada ya mimi kuondoka!

Ugomvi ulizuka akakasirika akaenda Morogoro kumuona mwanae aliporudi tu akafa kwa ajali mbaya sana ya pikipiki tena usiku porini kutoka Tumbakose akienda Rofati Huko Wilaya ya Chemba Dodoma. Hadi juzi nimemuota akiwa kwenye shamba zuri lililopandwa kwa mistari akitoa maelekezo fulani hivi Namuota mara kwa mara tukiongea japo huwa sikumbuki naongea naye nini! Nilikemea hiyo hali ikaondoka lakini imerudi tena juzi juzi hapa!!!!SIJUI NI KWANINI!!!
 
Ndoto ni mlango mmojawapo ambao binadamu anafanya mawasiliano na upande wa pili wa ulimwengu wa mwili yaani upande wa ki-roho.
Binadamu tumekuwa tunapuuza sana ndoto mbalimbali tunazoota tukiamini kila kitu ni kawaida. Kwa nini ndoto moja ijirudie mara kwa mara?? Yamkini kuna ujumbe muhimu unapewa bila wewe kuufanyia kazi.

Samahani kukukuliza maswali yafuatayo, 1. Unafanya shughuli gani kwa sasa??? 2. Hali yako kiuchumi imekaaje???.

Ukiwa unajiandaa kujibu hayo maswali, nakushauri kwa Imani yako Ongea na Mungu akupe kwa lugha nyepesi utayoielewa na katika hili nakushauri achilia sadaka kwa ajili ya ndoto hiyo. Mungu ni muaminifu atakuambia.
 
Ndoto ni mlango mmojawapo ambao binadamu anafanya mawasiliano na upande wa pili wa ulimwengu wa mwili yaani upande wa ki-roho.
Binadamu tumekuwa tunapuuza sana ndoto mbalimbali tunazoota tukiamini kila kitu ni kawaida. Kwa nini ndoto moja ijirudie mara kwa mara?? Yamkini kuna ujumbe muhimu unapewa bila wewe kuufanyia kazi.

Samahani kukukuliza maswali yafuatayo, 1. Unafanya shughuli gani kwa sasa??? 2. Hali yako kiuchumi imekaaje???.

Ukiwa unajiandaa kujibu hayo maswali, nakushauri kwa Imani yako Ongea na Mungu akupe kwa lugha nyepesi utayoielewa na katika hili nakushauri achilia sadaka kwa ajili ya ndoto hiyo. Mungu ni muaminifu atakuambia.
Baada ya muda kupita na kufanya mengi Kwa kiasi chake ,sasa nipo chuo , diploma .Kuhusu uchumi sipo vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom