Marehemu Ally Zona amezikwa jioni hii Katika Kijiji cha Semngano Wilayani Muheza

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
WanaJF nichukue fursa hii kuwataarifu kuwa Marehemu Ally Zona amezikwa jioni hii katika kijiji cha Semngano kilichopo katika Kata ya Kilulu Wilayani Muheza Mkoani Tanga. Msiba uko Tanga Mjini. Mwili wa Marehemu baada ya kuswaliwa ulisafirishwa kuelekea Muheza kwa Mazishi.

Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Tanga Mjini walishiriki msibani hapo na baadaye Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Muheza wakiongozwa na Katibu wao Bw. Martini Kifua na Katibu Mwenezi Bw. Rajab Mhina walishiriki katika Mazishi na kukabidhi Mchango wao wa Rambirambi kwa Baba Mkubwa wa Marehemu. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMENI.
 
Naungana na wote walipatwa na madhara hayo. Msiba huu ni wetu sote wapenda amani. Tunaomba vyombo vya dola tukio hili liwe la mwisho, na lisijitokeze tukio jingine tena linalofanana na hilo. Napenda kuchukua fursa hii kulaani vikali wale wote walioanza kurushiana lawama hata kabla ya mwili wa marehemu kuhifadhiwa. Nalaani vikali wanaojifanya wanaunda tume ya kuchunguza kitu ambacho tayari kiko wazi, wahusika wanafahamika.
 
RIP Ally, politician wanakaa meza moja na kupeana mikono wakidai tukio hili liwe la mwisho, Any way nashauri CHADEMA itoe semina Elekezi kwa jeshi la polisi kwani ndio linaonekana somo la uraia halijawaingia vizuri, au ndio yale matatizo ya kutumia vyeti vya watu kupata Ajira
 
rip ally, politician wanakaa meza moja na kupeana mikono wakidai tukio hili liwe la mwisho, any way nashauri chadema itoe semina elekezi kwa jeshi la polisi kwani ndio linaonekana somo la uraia halijawaingia vizuri, au ndio yale matatizo ya kutumia vyeti vya watu kupata ajira

kwani kuulizia rambirambi kuna ubaya gani maana tukijua ni kiasi gani tutajua chadema wamewajibikaje kwanza kwanini viongozi wa kitaifa hawakuhudhulia
 
kwani kuulizia rambirambi kuna ubaya gani maana tukijua ni kiasi gani tutajua chadema wamewajibikaje kwanza kwanini viongozi wa kitaifa hawakuhudhulia

Pumba hizi.....kalishe ng'ome utapata maziwa zaidi!
 
Rip kamanda. Japo hawatachukuliwa atua alimuua ila najua damu yake lazima iwaandame wale wote waliohusika. Rip kamanda.
 
Hivi ccm wametoa rambirambi sh ngapi? Manake puppies wao ndo waliofanya mauaji! Nape alikuwepo?
kwani kuulizia rambirambi kuna ubaya gani maana tukijua ni kiasi gani tutajua chadema wamewajibikaje kwanza kwanini viongozi wa kitaifa hawakuhudhulia
 
Back
Top Bottom