Marehemu alipwa mshahara kwa miaka 3,2009 alipandishwa cheo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marehemu alipwa mshahara kwa miaka 3,2009 alipandishwa cheo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutunga M, Mar 25, 2010.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Nimesoma kwenye gazeti moja litolewalo mkoani kagera,liitwalo malengo yetu juu ya mtumishi aliyekufa kuendelea kulipwa mshahara na kupandishwa cheo,hivi ufisadi kama huu nani anautazama ?


  Na Anthony Mayunga-Bunda.
  HALMASHAURI ya wilaya ya Bunda imeingia kwenye kashifa kubwa baada ya
  kubainika kumlipa mshahara Mwalimu aliyekufa mwaka 2007 na
  amepandishwa daraja mwaka 2009 huku fedha yake haijulikani
  anayeichukua.

  Kashifa hiyo iliyoibuliwa juzi kwenye kikao cha kawaida cha baraza la
  madiwani na kuwaacha wajumbe wakiwa na mshangao ,inazidi kuonyesha
  wazi kuwa tume iliyopita kuhakiki watumishi hewa haikufanya kazi kama
  ilivyotakiwa .

  Akiongea kwa masikitiko katika kikao hicho diwani wa kata ya Kibara
  Venance Kamonyore alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha ofisi ya
  mkurugenzi kuendelea kupokea mshahara wa Marehemu Mwalimu Charles
  Mwijarubi aliyekuwa shule ya msingi Namibu kata ya Kibara aliyekufa
  mwaka 2007.

  “Niliwahi kumuuliza mkurugenzi inakuwaje mtu amekufa mwaka 2007
  mshahara wake unaendelea kuja mpaka sasa ,la kushangaza mwaka 2009
  alipandishwa daraja na mshahara kuongezeka,ndugu zake wanataka kujua
  nani anachukua fedha zao,”alihoji diwani.

  Alisema kuwa ndugu zake walikuwa tayari kwenda wizarani kudai hizo
  fedha na ufisadi wa kutumia jina la marehemu kujipatia fedha hizo
  ambazo familia yake hazijazipata.

  “Toka nimeongea na Ded sijapata majibu ,hivi kweli fedha hizo
  zinarudoshwa hazina na kwa nini jina hilo liendelee kuonekana kama
  yuko kazini ili hali amekufa sasa ni mwaka wanne?”alihoji.
  Hoja hiyo iliyosisimua baraza ilimfanya mkurugenzi mtendaji Cyprian
  Oyier kujitutumua kuijibu,akikiri kuwa aliambiwa na diwani na
  kufuatilia ili jina hilo liondolewe na mshahara usiwe unakuja.

  “Nilimweleza Dt ahakikishe wanawaandikia hazina jina hilo
  liondolewe,yuko hapa atajibu,kama mshahara huo unakwenda wapi,maana
  kama jina halijaondolewa utaendelea kuja,”alisema mkurugenzi.
  Hata hivyo kaimu mweka hazina Stela Msangya hakuweza kujibu tuhuma
  hiyo mpaka mwisho wa kikao hali ambayo inazidisha mashaka juu ya
  tuhuma hiyoiliyoibuliwa ghafla .

  Kaka wa Marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwalimu mstaafu
  Mwijarubi akiongea na gazeti kwa njia ya simu alisema kuwa wao
  wanafuatilia kuona ufisadi huo wa kutumia majina ya marehemu kupata
  fedha.

  “Huo ni mpango wa hao wataalam maana haiwezekani kumpandisha marehemu
  daraja tena akiwa na miaka miwili amekufa ,na wakijua kama haku na
  hujuma hapo ,huu ni mchezo uliozoeleka na si mara ya kwanza lazima
  tujue kiini chake,”alisema.

  Alidai kuwa mpaka risti za mishahara ya mwezi januari ipo na wanayo na
  kuwa mrithi wa mali za marehemu ambaye ni kijana wake James Charles
  Mwijarubi alimfikia diwani mwezi februari baada ya kupata taarifa na
  katika ufuatiliaji walibaini ukweli wa mambo.

  Baadhi ya madiwani walisikitishwa na mchezo huo ambao walidai ni
  kashifa kubwa kwa halmashauri huku wakidai kuwa tume zinazoundwa
  kuchunguza watumishi hewa hazijazaa matunda kwa kuwa majina hewa bado
  yapo sekta za elimu na afya.

  CHANZO:Gazeti Malengo Yetu,toleo la jumanne ya wiki hii
   

  Attached Files:

Loading...