March 30, 1867: Kosa kubwa la Kihistoria walilofanya URUSI na kuwapa nafasi US kuwa Kiranja wa Dunia

mi nataka kujuwa kama Mrusi alifanya juhudi zozote kuirudisha Alaska.je kama alifanya hivyo Marekani alichukuwa uamuzi gani
Juhudi ya nini mkuu wakati wameuziana kihalali serikali na serikali.
Mikataba ikasainiwa cheki inatoka na ipo hadi leo na nimeiattach pale juu.
Hata wamarekani wengi wanadhani Russia walinyang'anywa kibabe hapana mkuu it was a legal deal.
Na kiongozi wa urusi Alaska pamoja na warusi wengine wakaondoka, likapigwa gwaride urusi wakashusha bendera yao us wakapandisha yao wakapeana mikono kazi ikaisha kwa mawazo ya viongozi wachache waliotawala kifalme Czars au the alexanders.
 
Dunia ni duara kwa maana hiyo Urusi na Marekani ni majirani upande wa kaskazini mashariki katika majimbo ya Siberia-Urusi na Alaska-Marekani.
Haaaaaaaaaa kuna mstali wa Greenwich uliopita katikati ya Urusi na America. Wazungu wametukalilisha tumecholewa mstali wa Greenwich unaopita Accra Ghana, London wakaita upande Huu ni Magharibi(west) na Mashariki(East). Kwa kuwa America ipo West na Urusi ipo East Dunia ni duara utakuwa unazunguka kutoka America to Urusi. Sijajua kama katikati ya America na Urusi kuna mstali mwingine unaotenga upande wa West na East kituko ndo kinaanzia hapo.
 
Washenzi sana hawa wafalme. yani ingekua haijauzwa hii dunia ingekua mahala salama maana wababe wanaogopana sio siri. Nimecheki ile midhabau kwenye hiyo tunel mkuu hadi nakaribia kutokwa na machozi. Hao wafalme walafanya kosa kubwa sana.

Hivi mkuu urusi hawawezi irudisha laska tena kwa kuvunja hayo makubaliano ikiwezekana walipe na fidia tuu mambo yaishe maana najua hiyo ardhi itakua na mambo mema sana chini yake.

Vipi kipindi hicho na hao raia wa alaska walirudi urusi au naoo waliuzwa?
Haya mambo mkuu haiwezekani kabisa. Maana wafuatiliaji wa mambo wanasema hata kama ingeendelea kuwa russia WW1
Baada ya hawa wafalme kuangushwa, Bado wazungu Wa ulaya na US wangepiga zengwe ili hiyo Alaska ibaki kwa Canada au US au iwe nchi ya kujitegemea ingawa hapo kungekuwa angalau na uwezekano wa kujadiliana warudishiwe. Sio Tu hawawezi kuidai sidhani kama wanaweza kufikilia hilo maana Russia kurudi alaska ni afadhali iwe WW3 kuliko wao kukaa puani mwa US.
Pale walikaa warusi kadhaa wengi wa wakazi wa pale walikuwa ni waeskimo. Ila warusi waliondoka. Leo unaposikia ugomvi wa marekani na russia kwenye media alaska ni tofauti huko wanawasiwasi ikitokea WW3 russia watapitia huko na kuingia canada na kushuka hapo chini kwa wababe US wapigane uso kwa uso.
WW3: 'Get ready for Russian invasion' Americans in Alaska told to prep for IMMINENT ATTACK
 
Hiyo Alaska Urusi walipataje kumiliki Kwa kupambana au ilikuwaje.
ni eneo ambalo lilikuwa halijagunduliwa na wote, Ila warusi wajasiliamali waliingia pale na kupachukua. Baadae kukatokea vita kati ya Urusi na Uingereza na washirika wake, Kwa kuhofia kuwa wakishindwa wataipoteza alaska au watakuwa hawana pesa ya kuihudumia kuliko kukosa yote wakaamua kupeleka wazo kwa wamarekani wawauzie. Lakni ilikuwa ni hofu tu maana bado kwa rasilimali za alaska hadi leo imesharushisha pesa ya kununuliwa kwake kwa US zaidi ya mara 400
 
Alaska inaonekana kama ni sehemu ya Marekani kabla kuuzwa.
Nahisi palitokea ushawishi mpaka wakapauza.

Mimi hapa kwangu nimefanya hivo kuna kijisehemu kwa mbele ni cha jirani yangu ila kwa mtu mgeni akiona atasema cha kwangu nikaongea nae nikampa pesa kidogo nimekachukua.
mkuu kihalali alaska ilipaswa kuwa canada
north_america.gif

July 1, 1867 Ndio Canada ikawa nchi kamili ya kujitegemea huku US wakiwa wameshajichukulia Bingo.
 
Lakini mimi naona kama Alaska imeungana na Canada. Sasa ilikuwaje isiwe mali ya Canada originally!!?
Wakati haya yote yanafanyika Canada haikuwa nchi officially. Imekuwa nchi miezi michache baadae US washafanya hii biashara. Kama US kusingekuwa na Vita vitana na tetesi za vita enzi hizo kati ya wenyewe kwa wenyewe zilizowafanya wawe weak kiasi wangeweza Kuinunua na Canada pia kutoka kwa waingereza.
 
bora alaska waliuza kuliko crimea walivyoitoa kama zawadi...US huwa wajanja sanahasa kwe kuplan mambo ya mbelen kuliko russia
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA njoo utie Baraka zako hapa

MWANZO:

Mkuu Mseza,
Urusi alifanya makosa makubwa sana kuuza Alaska lakini tusema tu kwamba alikuwa hana jinsi yoyote zaidi ya kufanya vile. Ikumbukwe Urusi imemuuzia Marekani Alaska 1867 lakini miaka 11 nyuma yani mwaka 1856 Urusi alipigana Vita ya Crimea (CRIMEAN WAR) dhidi ya falme za Ufaransa, Uingereza na Uturuki. Hili lilipelekea Urusi kushindwa vita, kuzorota kiuchumi hasahasa baada ya kunyanganywa majimbo yake muhimu yaliyo karibu na bahari nyeusi. Shughuli nyingi za kiuchumi nchini Urusi zilkwama hasahasa baada ya kuzuiwa kutumia bahari nyeusi kama hapo mwanzo. Urusi kuona anazidiwa ikabidi mwaka 1856 kusaini mkataba wa amani wa Paris (Pact of Paris 1856) na hayo mataifa matatu ambapo Uingereza na Ufransa walimlalia sana. Kabla ya hivi vita Urusi ndiyo lilikuwa taifa lenye nguvu nyingi barani Ulaya kiasi cha kuwapa changamoto kubwa Waingereza, Waturuki, Waprashia, Waaustria na Wafaransa hivyo huu ukawa ndiyo muda muafaka wa kummaliza kabisa hasimu wao. Hivyo basi baada ya Ufalme wa Uingereza kuona kwamba Ufalme wa Urusi umezorota kijeshi wakapanga mkakati madhubuti wa kuvamia majimbo yake muhimu likiwemo jimbo lake la ALASKA kupitia nchi ya CANADA ambayo huko nyuma ilikuwa koloni la Uingereza.

Muingereza angefanikiwa kufanya hivi basi ni dhahiri kabisa Ufalme wa Urusi usingeweza kulinda hilo jimbo la mbali kama tu alishindwa kulinda majimbo yake ya karibu kama Sevastopol kwenye Vita ya Crimea ya mwaka 1853-1856. Hivyo wakiwa wamechanganyikiwa wakaamua tu kuuza ili wapate faida yoyote kuliko kukosa kabisa, maana kama falme ya Uingereza ingefanikiwa kuivamia ALASKA hata zile hela ambazo Marekani alilipa sijui kama angepata. Ikumbukwe kwamba kipindi hiki Uingereza alikuwa anachuana na Urusi kwasababu Urusi alikuwa na ndoto ya kuvamia dola la Uturuki ili kufika Mashariki ya kati. Lakini Muingereza alihisi kama akiuachia Ufalme wa Urusi kufika Mashariki ya kati basi hawataishia hapo ni lazima tu wangefika India na Mashariki ya mbali ambapo Muingereza alikuwa na maslahi makubwa kiuchumi; hivyo ili kuzuia Urusi isikue zaidi akaamua kufanya fitna za kijeshi hasa kwenye sehemu zenye umuhimu mkubwa kiuchumi kwa ufalme wa Urusi.

Warusi baada ya kung'amua kwamba Uingereza ina mpango huo dhidi yake wakaamua kuwawahi mapema angalau wapate hata kitu kidogo kuliko kukosa kabisa. Walipeleka mawazo kwenye serikali ya Marekani na yakapokelewa kwa mikono miwili, tena wakafanya hadi na sherehe ya makabidhiano. Hivyo sheria ilitumika na wala hakuna kosa lolote japo Warusi wengi hadi leo wanaulalamikia sana ule mkataba.

Lakini kwanini Ufalme wa Urusi Uliamua kuizia Marekani pekee?
Sababu muhimu kabisa ni hizi zifuatazo hasa pale unaposoma historia ya Ulaya.

1. Sababu za kimkatati- Marekani kuanzia mwaka 1783 hadi kufika 1945 ilikuwa inaendeshwa na sera kuu mbili kubwa ambazo waasisi wake waliziweke. Sera ya kwanza Inaitwa THE MONROE DOCTRINE na ISOLATION POLICY: Ambapo Monroe Doctrine ilikataza kwa nchi yoyote ile duniani kuingilia maslahi ya taifa la Marekani iwe ni barani Amerika Kaskazini au Amerika Kusini. Isolation Policy ilisema kwamba Marekani haifungamani na taifa lolote lile duniani hasa yale ya Ulaya hivyo itafanya biashara na kila taifa. Hii ilisaidia kuepusha migogoro na kukua haraka kiuchumi. Sasa Ulaya kulikuwa na sera inayotwa "ULINGANIFU WA NGUVU" au "THE EUROPEAN BALANCE OF POWER" ambapo mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa yanazuiana yasikue kiuchumi wala kijeshi kwasababu taifa moja lilikua sana kiasi cha kumzidi mwenzie ni lazima italeta matatizo na vurugu hivyo kupelekea vita baina yao. Marekani alikuwa siyo mfuasi wa hii sera hivyo basi Urusi akaona kwamba Uingereza au taifa lolote la Ulaya likipata ALASKA ni lazima litakuwa na uchumi mkubwa kutokana na rasilimali zake hivyo kuharibu "ULINGANIFU WA NGUVU" au "THE BALANCE OF POWER" barani Ulaya hivyo kimkakati akaamua kuiuzia Marekani taifa ambalo lilikuwa halifungamani na upande wowote na lisingeleta madhara.

2. Sababu za Kibiashara na kibinadamu- Kwasababu Marekani hafungamani na taifa lolote ingekuwa rahisi sana kwa Urusi kuendelea kufanya biashara kwenye eneo lile bila kupata bugudha yoyote ile. Lakini kubwa zaidi ni usalama wa raisi wa kirusi waliokuwa Waorthodoksi ambao walianzisha makazi yao humo Alaska. Lakini kwasababu alikuwa na ugomvi na mataifa ya Ulaya basi ALAKSA ingeangukia mikononi kwa Ufaransa au Uingereza ingeharibu BALANCE OF POWER.

3. Historia nzuri ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili- Wakati Marekani anadai uhuru kutoka kwa Uingereza kuna kipindi ya miaka ya 1700's Uingereza aliomba msaada wa kijeshi kutoka Urusi ili wakawapige waasi lakini Malkia wa Urusi Catherine The Great alikataa na akawaambia Warusi kwamba itakuwa na faida sana kwa Urusi kama Marekani itakuwa taifa huru hivyo kuleta ushirikiano Imara wa kibiashara na taifa hilo. Upande wa pili wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani 1861-1864 Urusi ilikuwa inafanya biashara sana na Marekani na pia ilikuwa inaitambua serikali ya Abraham Lincoln kama ndiyo halali wakati mataifa ya Ulaya yalikuwa yanafanya sana biashara na majimbo yalioasi ya nchi za kusini mwa Marekani. Hivyo niseme tu uhusiano wao ulikuwa mzuri na Urusi aliona angekuwa salama sana kutokana na haya mambo ambayo imewahi kuwafanyia Wamarekani katika nyakati zao za shida. Hivyo biashara zao, watu, pamoja na maslahi yao yaliyokuwepo yamebakia ALASKA hata baada ya Mauzo yalikuwa kwenye mikono ya taifa salama la watu wanaoaminika.

HITIMISHO:

Kwa mtazamo wangu Makosa ambayo yamemfanya Marekani kuwa Kiranja wa dunia hii siyo hili la ALASKA pekee. Mataifa ya Ulaya yamechangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na tathmini hafifu juu za siku za mbeleni. Mfano mwaka 1783 Marekani, Uingereza na Ufaransa walisaini mkataba wa Paris (Paris Treaty of 1783) ambao kwa mara ya kwanza Uingereza alikubali kuitambua Marekani kama taifa huru na kuamua kusitisha vita vya Uhuru. Ufaransa alipigia debe sana Marekani kuwa nchi huru akitegemea kwamba baada ya hapo Marekani haiwezi kujitawala yenyewe hivyo isingefika mbali na angeitawala yeye. Lakini kwa bahati mbaya Ufaransa ilikosea Mahesabu kwasababu miaka sita tu baada ya huu Mkataba Mapinduzi ya Ufaransa (French Revolution) ya mwaka 1789 yakaanza na Ufalme wa Lous XVI uliokuwa na ndoto ya kutawala Marekani ukaanguka.

Upande wa pili Uingereza aliiacha Marekani iwe huru kwasababu aliogopa kwamba Marekani inaweza kuungana na mataifa kama Ufaransa na Uhispania ambayo ni hasimu kwake hivyo kupelekea yeye kupoteza majimbo mengi zaidi ya yale ambayo Ufaransa aliyasaidia Makoloni ya Marekani kumnyang'anya muingereza. Hivyo akaamua kukubali na kutoa eneo kubwa sana kwa serikali ya Marekani kwasababu asingefanya hivyo Marekani walikuwa wanataka kufika hadi CANADA na kulifanya jimbo lao. Mwaka 1812-1814 hili lilithibitika kwenye Vita Vikali baina ya Uingereza na Marekani (Anglo-American War 1812) Marekani alitaka kuingia CANADA lakini alishindwa na matokeo yake THE WHITE HOUSE ilichomwa moto yote; mataifa yote mawili yakaishia kusaini mkataba wa amani.

Wanahistoria wengi wanasema mkataba huu wa Paris wa Mwaka 1783 ni moja kati ya mikataba mitano mikubwa na muhimu sana kuwahi kutokea, ambayo imebadilisha historia ya dunia mbali kabisa na Ule wa Westphalia (Peace of Westphalia) wa mwaka 1648 au Versailles (Versailles Peace Treaty) wa 1919. Kwasababu huu mkataba usingefikiwa na taifa la Ufaransa na Uingereza wangeamua kukubaliana tu kuhusu mgawanyo wa maslahi huenda taifa la Marekani lingesambaratika au lisingekuwa kubwa kama ilivyo leo. Mfano mzuri wa hili ni kipindi cha (MOROCCAN CRISIS 1905-1906) ambapo Uingereza na Ufaransa japo ni maadaui waliamua kuungana ili kumzuia Mjerumani asitawale Morocco au kipindi cha (FASHODA INCEDENT 1898) ambapo Ufaransa alikubali kumuacha Muingereza achukue sehemu kubwa ya eneo la MTO NILE WA MISRI kwasababu walikuwa wanazuia nguvu ya Ujerumani ambalo ndilo lilikuwa taifa kubwa linalokua kwa kasi kipindi hicho. Hivyo kama wangeendelea kupigana wenyewe ni dhahiri wangemtengeneza Mmarekani wa pili; na kama huu mkakati ungetumika 1783 basi Marekani ingekuwa bado ni mali ya Uingereza au Ufaransa.
 
Kibaya zaidi binadamu hata hawezi kujifunza kutokana na makosa ya mwingine, mijadala mingi humu, imejawa na roho hii, eti katiba mpya, tume huru, vyote ni visingizio tu au vilio vya wasiyemjua adui awapigae, wanavuva tu. Kwanza katiba si lazima iandikwe, watu wanaiishi tu, hivi tuishivyo ndo katiba yetu ilivyo wala si ile ya akna Msekwa, 77. Na wala rasimu ya Warioba haituakisi vyema, ss ni wabinafsi na tunaupenda, wezi na tunaupenda, mafisadi na tunaupenda, mtu mwizi ndye mtafutaji mzuri wa kusifika, mtiifu lofa, mara ngapi tunawaabudu hadi makanisani, huku tukiwajua vyema kuwa ni fisadi au jambazi kabisa wa mtaani ajulikanae kabisa, tunampa heshima kubwa ktk jamii, mpiganaji, mjanja, anajua kutafuta,mjanja na baya zaidi hata Mungu wenu mnayejifanya kumwabudu mnamdhiaki, eti jamaa amebarikiwa sana na Mungu, hamyajui haya? Katiba mpya hata iandikwe na Mungu bila kuiua hii roho ni kazi bure, hata huko mbinguni sijui kulikuwepo na katiba nzuri tu, ubinafsi ulipomwingia mmoja Vita kuu ikatokea, sio dhumuni ni mfano tu.
nakupa malike mingi mingi mkuu
 
Mpaka wa karibu kabisa Kati ya US au Jimbo la Alaska na urusi ni visiwa vinavypoishana kwa umbali wa km 4 tu. Unaweza kwenda us kutokea Russia hata kwa kuogelea mkuu tatizo upande wa russia Kuna baridi kali na barafu. Ni wajasiliamali wasioogopa kuchukua risk wa kirusi ndio walivuka na kupaona Alaska enzi hizo USA wanamatatizo yao mengi tu hata wazo la kuitafuta Alaska h alikuwepo. Baadae serikali ya kifalme czars wakapamiliki. Ndio maana hapo Alaska walikutana na matycoon wajasiliamali wakichina. Usione mchina anaingia hadi huko vijijini mtimibilo alianza kutafuta sehm zenye risk kitambo sana.
Thanks, kwa ufafanuzi
 
Na lililo kubwa zaidi hapa la kujifunza ni roho ya UBINAFSI, umimi. Hii ni dhambi kuu kuliko zote. Mtu anaejifikiria yeye tu, familia yake tu, ukanda wake tu, dini yake tu, au kabila lake kwanza kabla ya utaifa wake, ni muhaini, adhabu yake ilipaswa kuwa kubwa zaidi ya muuaji (murderer). Mbinafsi atatengeneza ARV fake apate faida, atapokea 10% kuuza migodi, atashirikiana na adui kuiangamiza nchi, nk. Ubepari ni zao la ubinafsi. Changu badala ya chetu. Shida tupu.
Umenena Mkuu, Ubinafsi ndio mama wa Unyonge wa binadamu, katika Ubinafsi mbwa yu na thamani kubwa kuliko jirani yangu, na wafanyao hayo ni sisi tukeshao makanisani na misikitini.
"Maisha ni Furaha, kama haipo ni Upuuzi. Na hakuna Furaha ya mtu bali Watu"
 
Back
Top Bottom