March 30, 1867: Kosa kubwa la Kihistoria walilofanya URUSI na kuwapa nafasi US kuwa Kiranja wa Dunia

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
usa_vs_russia.jpg

Kuna sababu nyingi za kiuchumi,Kiintelijensia, Conspiracy, Kisiasa, Kidini hata kihistoria kwa nini US ni Taifa kubwa na hana mpinzani Duniani. Kuuzwa kwa ALASKA March 30, 1867 ninatafsiri kuwa mlango mkubwa kwa Marekani Kufanikiwa.

MAISHA YA ALASKA CHINI YA RUSSIA
Sakhalinmap.gif

Enzi hizo alaska ilikuwa ni kituo cha biashara ya kimataifa.Mji mkuu uliitwa na warusi Novoarkhangelsk. Hapa alaska walikuja watu wa mbalimbali maana kulikuwa na biashara nono kama njia ya kulifikia soko ambalo ilikuwa ni US. Watu walileta Sufi,Majani ya chai,Pembe,Mazao maana ilikuwa ni shortcut ya kupeleka bidhaa US.huku wakirudi makwao wengi wakiwa ni wachina na samaki kutoka alaska. Kulikuwa na viwanda, migodi ya makaa ya mawe na fununu ya uwepo wa dhahabu yaani dunia bado inashangaa kwa nini Russia waliuza?

UROHO WA WANASIASA NA KUJIINGIZA KWAO KWENYE BIASHARA BADALA YA KUTUMIKIA WANANCHI ULIVYOKOLEZA UUZWAJI WA ALASKA.
View attachment 450264View attachment 450265
Mbabe hapo juu ni Alexander Baranov, alipewa kazi ya kuisimamia Alaska. Alifungua mashule na kuwafundisha lugha wazawa wa alaska, kilimo na kama haitoshi akao binti wa hapo. RUSSIA AMARICA COMPANY (RAC) ya kirusi ilikuwa ndio gangwe wa biashara zote pale alaska ikiwemo na migodi ya Makaa ya mawe. Hii iliundwa na wajasiliamali shupavu walilipa kodi za mamilioni kwa Serikali ya Russia maana walipata faida zaidi mara 1000.Watawala na familia zao walijimilikisha hisa kwenye kampuni hilo na kujitajirisha sana.

MAUZO YA ALASKA KWA WAMAREKANI
Alaska_Purchase_(hi-res).jpg

JLM-1867-Emanuel-Leutze-Purchase-of-Alaska.jpg

Uamuzi wa kuuzwa kwa ALASKA uliibua hisia mbalimbali kote marekani na Urusi. Vyombo vya habari urusi vilipiga kelele na kuhiji Tutauzaje ardhi ambayo tumeihangaikia kiasi hicho? Ardhi ambayo Madini hadi dhahabu imepatikana na pia kuna mawasiliano? Huko USA pia magazeti yalihoji, Yaani kwa nini serikali ikatumie kodi za wananchi kwenda kununua barafu, eneo lenye waeskimo wanaoishi kama wanyama?Hata bunge la congress lilikataa. Baada ya mvutano mkali Hundi ilisainiwa ya ununuzi wa eneo lenye hekari 1.5Millioni kwa pesa za kitanzania 14Milioni wakinunua kila hekari kwa shilingi 10,000 ya kitanzania na alaska kuwa chini ya USA.

MAREKANI WASHEREKEA NA URUSI WAJUTIA
447897-Old-gold-mine-tunnel-around-Salmon-Glacier-Hyder-Alaska-Stock-Photo.jpg

GetFile.aspx

Haikuchukua muda mrefu US waligundua Dahabu nyingi sana huko alaska,Mafuta,Chuma na Mbao. Ndani ya miaka kadhaa wakawa wamesharudisha pesa yao na faida Lukuki. Alaska ikaiingizia serikali ya marekani mamillioni ya pesa kuliko walivyotarajia. Huku urusi wakiishia kutoa visingizio vya vita vya crimea kuwa Uingeleza ingewashinda na kuwanyang'anya alaska bora waliiuza lakini ikumbukwe viongozi walikuwa wameshajinufaisha na kushiba.

MAMBO YALIVYO SASA DUNIANI, INGEKUWAJE KAMA ALASKA INGEKUWA RUSSIA?
Russian-Nuclear-Missiles.jpg

1029516410.jpg

Ili kuelewa vizuri hapa baada ya vita vya pili vya dunia kullibuka Vita vikubwa duniani vya Kijasusi na Hujuma kati ya USSR na wadau wake na US na wadau wake. Sisi tunaofuatilia redioni Tunaadithiwa ilikuwa ni Vita baridi. Lakini katika Ulimwengu wa INTELLIJENSIA,UJASUSI,HUJUMA,UDUKUZI walioshiriki wanasema ilikuwa ni zaidi ya vita moto.
Itakumbukwa Mtambo wa Nyuklia wa siri ulivyotaka kujengwa Cuba baada ya US kuanza kuweka yake Uturuki Ballistic Missiles kuitisha (pitia link hapo) Urusi. Cuban Missile Crisis - Wikipedia. Kama alaska singeuzwa, Hiyo ingekuwa kama TAIWAN kwa china, Badala ya Cuba sasa US ingekuwa katika wakati mgumu sana, Wengine wanasema ingechukuliwa kibabe kipindi cha WW1.

Hii ndio dunia yetu
Karibuni kwa maoni na michango kuiangalia Dunia kutokea Kona hii.
Note:Hii ni Thread imeegemea kwenye Siasa,Uchumi na Vita sio Dini na conspiracy theories

Michango ya wadau
************************************************************
Mkuu Mseza,
Urusi alifanya makosa makubwa sana kuuza Alaska lakini tusema tu kwamba alikuwa hana jinsi yoyote zaidi ya kufanya vile. Ikumbukwe Urusi imemuuzia Marekani Alaska 1867 lakini miaka 11 nyuma yani mwaka 1856 Urusi alipigana Vita ya Crimea dhidi ya falme za Ufaransa, Uingereza na Uturuki. Hili lilipelekea Urusi kushindwa kushindwa vita, kuzorota kiuchumi hasahasa baada ya kunyanganywa majimbo yake muhimu yaliyo karibu na bahari nyeusi. Shughuli nyingi za kiuchumi nchini Urusi zilkwama hasahasa baada ya kuzuiwa kutumia bahari nyeusi kama hapo mwanzo. Urusi kuona anazidiwa ikabidi mwaka 1856 kusaini mkataba wa amani wa Paris (Pact of Paris 1856) na hayo mataifa matatu ambapo Uingereza na Ufransa walimlalia sana. Kabla ya hivi vita Urusi ndiyo lilikuwa taifa lenye nguvu nyingi barani Ulaya kiasi cha kuwapa changamoto kubwa Waingereza, Waturuki, Waprashia, Waaustria na Wafaransa hivyo huu ukawa ndiyo muda muafaka wa kummaliza kabisa hasimu wao. Hivyo basi Ufalme baada ya Ufalme wa Uingereza kuona kwamba Ufalme wa Urusi umezorota kijeshi basi wakapanga mkakati madhubuti wa kuvamia majimbo yake muhimu ikiwemo jimbo lake la ALASKA kupitia nchi ya CANADA ambayo huko nyuma ilikuwa koloni la Uingereza.

Muingereza angefanikiwa kufanya hivi basi ni dhahiri kabisa Ufalme wa Urusi usingeweza kulinda hilo jimbo hilo la mbali kama tu alishindwa kulinda majimbo yake ya karibu kama Sevastopol kwenye Vita ya Crimea ya mwaka 1853-1856. Hivyo wakiwa wamechanganyikiwa wakaamua tu kuuza ili wapate faida yoyote kuliko kukosa kabisa, maana kama falme ya Uingereza ingefanikiwa kuivamia ALASKA hata zile hela ambazo Marekani alilipa sijui kama angepata. Ikumbukwe kwamba kipindi hiki Uingereza alikuwa anachuana na Urusi kwasababu Urusi alikuwa na ndoto ya kuvamia dola la Uturuki ili kufika Mashariki ya kati. Lakini Muingereza alihisi kama akuuachia Ufalme wa Urusi kufika Mashariki ya kati basi hawataishia hapo ni lazima tu wangefika India na Mashariki ya mbali ambapo Muingereza alikuwa na maslahi makubwa kiuchumi; hivyo ili kuzuia Urusi isikue zaidi akaamua kufanya fitna za kijeshi hasa kwenye sehemu zenye umuhimu mkubwa kiuchumi kwa ufalme wa Urusi.

Warusi baada ya kung'amua kwamba Uingereza ina mpango huo dhidi yake wakaamua kuwawahi mapema angalau wapate hata kitu kidogo kuliko kukosa kabisa. Walipeleka mawazo kwenye serikali ya Marekani na yakapokelewa kwa mikono miwili, tena wakafanya hadi na sherehe ya makabidhiano. Hivyo sheria ilitumika na wala hakuna kosa lolote japo Warusi wengi hadi leo wanaulalamikia sana ule mkataba.

Lakini kwanini Ufalme wa Urusi Uliamua kuizia Marekani pekee?
Sababu muhimu kabisa ni hizi zifuatazo hasa pale unaposoma historia ya Ulaya.

1. Sababu za kimkatati- Marekani kuanzia mwaka 1783 hadi kufika 1945 ilikuwa inaendeshwa na sera kuu mbili kubwa ambazo waasisi wake waliziweke. Sera ya kwanza Inaitwa THE MONROE DOCTRINE na ISOLATION POLICY: Ambapo Monroe Doctrine ilikataza kwa nchi yoyote ile duniani kuingilia maslahi ya taifa la Marekani iwe ni barani Amerika Kaskazini au Amerika Kusini. Isolation Policy ilisema kwamba Marekani haifungamani na taifa lolote lile duniani hasa yale ya Ulaya hivyo itafanya biashara na kila taifa. Hii ilisaidia kuepusha migogoro na kukua haraka kiuchumi. Sasa Ulaya kulikuwa na sera inayotwa "ULINGANIFU WA NGUVU" au "THE EUROPEAN BALANCE OF POWER" ambapo mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa yanazuiana yasikue kiuchumi wala kijeshi kwasababu taifa moja lilikua sana kiasi cha kumzidi mwenzie ni lazima italeta matatizo na vurugu hivyo kupelekea vita baina yao. Marekani alikuwa siyo mfuasi wa hii sera hivyo basi Urusi akaona kwamba Uingereza au taifa lolote la Ulaya likipata ALASKA ni lazima litakuwa na uchumi mkubwa kutokana na rasilimali zake hivyo kuharibu "ULINGANIFU WA NGUVU" au "THE BALANCE OF POWER" barani Ulaya hivyo kimkakati akaamua kuiuzia Marekani taifa ambalo lilikuwa halifungamani na upande wowote na lisingeleta madhara.

2. Sababu za Kibiashara na kibinadamu- Kwasababu Marekani hafungamani na taifa lolote ingekuwa rahisi sana kwa Urusi kuendelea kufanya biashara kwenye eneo lile bila kupata bugudha yoyote ile. Lakini kubwa zaidi ni usalama wa raisi wa kirusi waliokuwa Waorthodoksi ambao walianzisha makazi yao humo Alaska. Lakini kwasababu alikuwa na ugomvi na mataifa ya Ulaya basi ALAKSA ingeangukia mikononi kwa Ufaransa au Uingereza ingeharibu BALANCE OF POWER.

3. Historia nzuri ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili- Wakati Marekani anadai uhuru kutoka kwa Uingereza kuna kipindi ya miaka ya 1700's Uingereza aliomba msaada wa kijeshi kutoka Urusi ili wakawapige waasi lakini Malkia wa Urusi Catherine The Great alikataa na akawaambia Warusi kwamba itakuwa na faida sana kwa Urusi kama Marekani itakuwa taifa huru hivyo kuleta ushirikiano Imara wa kibiashara na taifa hilo. Upande wa pili wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani 1861-1864 Urusi ilikuwa inafanya biashara sana na Marekani na pia ilikuwa inaitambua serikali ya Abraham Lincoln kama ndiyo halali wakati mataifa ya Ulaya yalikuwa yanafanya sana biashara na majimbo yalioasi ya nchi za kusini mwa Marekani. Hivyo niseme tu uhusiano wao ulikuwa mzuri na Urusi aliona angekuwa salama sana kutokana na haya mambo ambayo imewahi kuwafanyia Wamarekani katika nyakati zao za shida. Hivyo biashara zao, watu, pamoja na maslahi yao yaliyokuwepo yamebakia ALASKA hata baada ya Mauzo yalikuwa kwenye mikono ya taifa salama la watu wanaoaminika.
byMalcom Lumumba
 
Mkuu stori ni nzuri..ila ulitakiwa uwe more detailed sana! Hiki kisa mtu ili akipate vizuri ungeweka vinagaubaga vilivyovyanywa na vyombo vya usalama..

Tulitaka tuune mivutano iliyotekea hadi jamaa wakapata Ardhi ya alaska...
Je baada ya Russia kugundua kuwa amefanya kosa kuuza alaska kilitokea nini?
Hakukuwa na jitiahda za kuirudisha alasaka?

So far Big mkuu! Ila tia vitu zaidi
 
urusi haina msimamo kabisa kwani mpaka sasa sijagundua why waliuza hiyo alaska je ni matatizo ya kiuchumi au nini?
 
Nina amini kuwa kuna jambo la kukijifunza hapa:
-Wale waliokuwa na uchu na ubinafsi leo hii hawapo wanaojuta ni wajukuu na vitukuu. Hivyo ndivyo wajukuu wetu na vitukuu watakavyojuta tunapo uza rasilimali zetu kwa wageni bila kufikiria kizazi kijacho."Majuto ni mjukuu".
 
Nina amini kuwa kuna jambo la kukijifunza hapa:
-Wale waliokuwa na uchu na ubinafsi leo hii hawapo wanaojuta ni wajukuu na vitukuu. Hivyo ndivyo wajukuu wetu na vitukuu watakavyojuta tunapo uza rasilimali zetu kwa wageni bila kufikiria kizazi kijacho."Majuto ni mjukuu".
Na lililo kubwa zaidi hapa la kujifunza ni roho ya UBINAFSI, umimi. Hii ni dhambi kuu kuliko zote. Mtu anaejifikiria yeye tu, familia yake tu, ukanda wake tu, dini yake tu, au kabila lake kwanza kabla ya utaifa wake, ni muhaini, adhabu yake ilipaswa kuwa kubwa zaidi ya muuaji (murderer). Mbinafsi atatengeneza ARV fake apate faida, atapokea 10% kuuza migodi, atashirikiana na adui kuiangamiza nchi, nk. Ubepari ni zao la ubinafsi. Changu badala ya chetu. Shida tupu.
 
Kibaya zaidi binadamu hata hawezi kujifunza kutokana na makosa ya mwingine, mijadala mingi humu, imejawa na roho hii, eti katiba mpya, tume huru, vyote ni visingizio tu au vilio vya wasiyemjua adui awapigae, wanavuva tu. Kwanza katiba si lazima iandikwe, watu wanaiishi tu, hivi tuishivyo ndo katiba yetu ilivyo wala si ile ya akna Msekwa, 77. Na wala rasimu ya Warioba haituakisi vyema, ss ni wabinafsi na tunaupenda, wezi na tunaupenda, mafisadi na tunaupenda, mtu mwizi ndye mtafutaji mzuri wa kusifika, mtiifu lofa, mara ngapi tunawaabudu hadi makanisani, huku tukiwajua vyema kuwa ni fisadi au jambazi kabisa wa mtaani ajulikanae kabisa, tunampa heshima kubwa ktk jamii, mpiganaji, mjanja, anajua kutafuta,mjanja na baya zaidi hata Mungu wenu mnayejifanya kumwabudu mnamdhiaki, eti jamaa amebarikiwa sana na Mungu, hamyajui haya? Katiba mpya hata iandikwe na Mungu bila kuiua hii roho ni kazi bure, hata huko mbinguni sijui kulikuwepo na katiba nzuri tu, ubinafsi ulipomwingia mmoja Vita kuu ikatokea, sio dhumuni ni mfano tu.
 
Alaska inaonekana kama ni sehemu ya Marekani kabla kuuzwa.
Nahisi palitokea ushawishi mpaka wakapauza.

Mimi hapa kwangu nimefanya hivo kuna kijisehemu kwa mbele ni cha jirani yangu ila kwa mtu mgeni akiona atasema cha kwangu nikaongea nae nikampa pesa kidogo nimekachukua.
 
Back
Top Bottom