Marathon kuwapatia Geay, Giniki Shs.161 milioni ikiwa wataibuka washindi Oregon Marekani

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,238
24,097
MASHINDANO YA RIADHA YA DUNIA

July 16 2022​

Eugene, Oregon USA


Kama watashinda mbio za marathon za 42km Jumapili ya tarehe 17 July 2022, basi wanariadha wa Tanzania Emanuel Giniki GISAMODA | Profile | World Athletics Emmanuel Giniki 2:10:39' nafasi 200 kwa ubora duniani huku Gabriel Geay ambaye muda wake 2:04:55' unamuweka ktk nafasi 26 kwa wakimbiaji kasi zaidi dunia, watavuna mamilioni ya pesa kwenye mashindano ya riadha ya dunia yanayofunguliwa leo Ijumaa nchini Marekani.

Kubwa ni kuwa muda ambao wanariadha hao wa Tanzania ktk rekodi zao unawapa nafasi ya kutoa upinzani mkali na hata kuwepo nafasi ya kuibuka na medali ya dhahabu, fedha au Shaba hii ni kutokana na kuhesabika kimichezo na rekodi zao kuwa ni miongoni mwa wanariadha bora duniani wa masafa hayo marefu ya mbio za marathon na lolote linaweza kujitokeza la kuishangaza dunia na taifa la Tanzania,.

Shirikisho la Riadha la dunia (WA) limetangaza kitita cha dola 70,000 kwa bingwa wa mashindano hayo ambayo ni zaidi ya Sh 161 milioni.

Wakimbiaji hao wa mbio za marathon toka Tanzania watashindana na wakimbiaji tajwa bora duniani toka nchi za Ethiopia, Maroc, Kenya, Uganda, Belgium, Eritrea, Republic of South Africa n.k source : Oregon22 | WCH 22 | World Athletics
 
Emanuel Giniki GISAMODA

Emanuel Giniki GISAMODA​

Birth Date: 18 May 1988
Place of Birth: HANANG
Country of birth: TAN
Age: 29
Gender: Men
Height (cm): 164
Weight (Kg): 50

cjs_9336.jpg
Gabriel Geay of Tanzania was fourth in 2:07:53. Boston, MA, April 18, 2022, 126th Boston Marathon
 
Emanuel Giniki GISAMODA

Emanuel Giniki GISAMODA​

Birth Date: 18 May 1988
Place of Birth: HANANG
Country of birth: TAN
Age: 29
Gender: Men
Height (cm): 164
Weight (Kg): 50

cjs_9336.jpg
Gabriel Geay of Tanzania was fourth in 2:07:53. Boston, MA, April 18, 2022, 126th Boston Marathon
Mtu anazaliwaje 1988 na anakuwa na miaka 29
 
17 July 2022
Eugene Oregon, USA

MATOKEO YA MICHUANO YA DUNIA, MBIO ZA MARATHON 42 Kilometa, OREGON 2022

Hatimaye michuano ya riadha ya dunia Eugene Oregon USA ya marathon kilometa 42 yamekamilika.

Mkimbiaji wa Tanzania Gabriel amefanikiwa kumaliza ktk muda mzuri wa 2: 07 : 31' na kushika nafasi ya saba huku mwenzie Emanuel Giniki Gisamoda akishindwa kumaliza michuano hiyo migumu.

Nafasi ya kwanza imeenda kwa Tamirat Tola 2:05:36' wa kutoka Ethiopia ikiwa ni recodi mpya ya michuano hiyo.

Nafasi ya pili pia imechukuliwa na mkimbiaji Mosinet Geremew 2:06:44 toka Ethiopia huku ya tatu ikienda kwa Bashir Abdi wa Belgium 2:06:48'

Nafasi ya nne mCanada Cameron Lewis 2:07:09' na nafasi ya tano ni Geoffrey Kamworor 2:07:14' kutoka Kenya huku Seifu Tura wa Ethiopia 2:07:17' na mtanzania Gabriel Gerald Geay 2:07:36 nafasi ya sita.

  1. 11804 Tamirat TOLA
    ETH
    ETH 2:05:36 CR
  2. 21796 Mosinet GEREMEW
    ETH
    ETH 2:06:44
  3. 31570 Bashir ABDI
    BEL
    BEL 2:06:48
  4. 41646 Cameron LEVINS
    CAN
    CAN 2:07:09 NR
  5. 52085 Geoffrey KAMWOROR
    KEN
    KEN 2:07:14 SB
  6. 61805 Seifu TURA
    ETH
    ETH 2:07:17
  7. 72307 Gabriel Gerald GEAY
    TAN
    TAN 2:07:31 SB
  8. 81609 Daniel DO NASCIMENTO
    BRA
    BRA 2:07:35
  9. 91634 Shumi DECHASA
    BRN
    BRN 2:07:52 SB

Kwa matokeo yote bofya :
Source : World Athletics | Marathon Result | World Athletics Championships, Oregon 2022
 
Alphonce Felix Simbu atashiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Uingereza ,28 Julai Hadi Agosti 8 mwaka Huu
 
Alphonce Felix Simbu atashiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Uingereza ,28 Julai Hadi Agosti 8 mwaka Huu

Habari nzuri hii, upande wa riadha wanaibeba bendera yetu ya taifa na kuitangaza nchi yetu, mfano mashindano ya dunia Oregon mkimbiaji Geay ktk marathon alikuwa ktk tatu bora na kutajwa tajwa sana ktk TV ingawa mwishoni mapafu ya waEthiopia na uzoefu wao ukawafanya washinde. Lakini kwa hakika Geay atashinda michuano mingi ijayo.
 
JINSI WAKIMBIAJI WA MARATHON ZA DUNIA WALIVYOKIMBIA HATUA KWA HATUA OREGON22



Bendera ya Tanzania ilikuwa inaonekana sana ktk kilometa zote 42 KM kupitia mkimbiaji wake. Video hii ni ya sayansi ya michezo na inatizamwa na wengi ktk kubaini uzuri na nani ni miongoni mwa wakimbiaji bora wa mbio za marathon duniani kwa sasa.

Source : Slowly channel
 
Habari nzuri hii, upande wa riadha wanaibeba bendera yetu ya taifa na kuitangaza nchi yetu, mfano mashindano ya dunia Oregon mkimbiaji Geay ktk marathon alikuwa ktk tatu bora na kutajwa tajwa sana ktk TV ingawa mwishoni mapafu ya waEthiopia na uzoefu wao ukawafanya washinde. Lakini kwa hakika Geay atashinda michuano mingi ijayo.
Naunga Mkono Hoja, Alphonce Felix Simbu, Gabriel Gerald Geay na Emanuel Giniki Gisamoda ni Wanariadha wa Kali Kwa sasa Tanzania Kwa Marathon. Wangekuwa Wote tungepata Medali.
 
Back
Top Bottom