Marashi ya Pemba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marashi ya Pemba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Apr 17, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Why is Pemba poor? why is the government leave the beautiful island that sits on a rain belt to deteriorate like this?

  Sasa mpaka mafuta hakuna? according kwa waandaji wa maandamano ya CUF kupinga Mwafaka, wameshindwa kuandamana kutokana na kisiwa kukosa mafuta. When did Tanzania had oil shortage? Is this a delibarate move by both Union and Revolutionary Governments to inflict pain and suffering to Pemba because they are light skinned and anti CCM?

  Si suala la mafuta tuu, ni mambo mengi unasikia kulivyo na umasikini wa kutisha!

  When will Marashi ya Pemba drift away and win the hearts of our policy makers?
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  The day people in power realize that we have only one country thus we gat be moving forward as united as we can!
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tatizo la mafuta hata Unguja hutokea mara kwa mara. Usambazaji wa mafuta visiwani hutegemea meli, na inapotokea meli kupata matatizo katika kutia nanga hasa katika bandari ya Mombasa ina maana mafuta yatachelewa kufika Unguja na yatachelewa zaidi kufika Pemba.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni kukata komunikesheni kwa wapemba si wanaona wana umoja usio tetereka na waliposema CCM hawaitaki tena ni kweli ccm wameipiga pande na haipo kama ipo ,hilo ndio kosa lao ,hata Unguja CCM imekataliwa lakini genge la Karume linataka kuonyesha eti waunguja ni CCM na waPemba ni CUF wamesahau kuwa Wazanzibari wanataka mabadiliko ya uongozi na sio watu bali Chama ,Wazanzibari wanataka mabadiliko ya Chama kinachoongoza serikali wameshachoka na chama chenye viongozi wanaojali matumbo yao.
  Huko ndiko waliko WaZanzibari kwa ujumla bado Tanganyika ambako mtu akihongwa basi anaichagua CCM au akiekewa masanduku ya gongo anasahau kama CCM ni jaa la manyang'anganyi na manyang'au. Lakini naona kila siku zikienda WaTanganyika wanaanza kujiona wanakufa huenda wakaikataa hongo wakati wa Uchaguzi ,Zanziba CUF ilifanikiwa baada ya kuwaeleza wananchi kuwa ukipewa hongo ichukue lakini msimamo ni ule ule wa kuikataa CCM kwani hiyo wanayokupa ni haki yako ,usikatae feza chukua na kura yako huitoi kwa CCM ,hivyo Zanzibar CCM inaogopa kutoa rushwa kwa ajili ya ucaguzi wanajua jamaa feza wataitafuta na hawapati kitu.
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mheshimiwa wacha kucheza ngoma usiyoijua. Hivi kweli wewe umetembelea Pemba?, na hakika huko kwenu Mikoani Bara kuna sehemu nyingi umepita. Jee hakuna umasikini huko wa kuusikitikia ambao unauzidi wa Pemba. Wacha jazba za Kipemba (au za watu wa Visiwani).
   
 6. R

  Ras-nungwi Member

  #6
  Apr 17, 2008
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pakachaaaa

  Acha kuleta ukereketwa pahala ambapo haustahiki. unataka kuniambia kwamba Pemba hali ni nzuri au mwenzetu uko nje ya TZ hujatembelea visiwanimuda mrefu..
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Pakacha,

  Nimefanya kosa gani kuhoji kuhusu haki ya watu kunyimwa mahitaji muhimu kurutubisha Utu wao?

  What difference does it make if it is Kyela or Pemba? You must have something personal against Pemba to lash out at the serious issue like that!
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  pemba wamewakosea viongozi baada ya kusema hawaitaki ccm.
  na hasa pale walipokuwa wabishi kiasi cha kuwa kura haziibiki pemba.
  ccm inajua haitakiwi kwa hiyo nayo haiwajali watu wa kule, japo kuwa serikali haipaswi kutoa huduma kwa waliowapigia kura za ndio tu
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wewe Ras Nungwi mimi sina ubavu hata wa kuvuka maji kuiona Kimbiji. Niko kwetu Tazari-Kigunda. Lakini nakuuliza umeiona Nungwi, Donge, Potowa, Mtende, Bambi,Fumba, Ndijani na kadhalika. Jee kuna maghorofa huko au mabarabara ya fahari, Mambo si ndo hayo hayo kama yalivypo Jadida, Kengeja na Mtambwe. Acha ushabiki wewe na jazba za Kipemba. Tunataka Umoja tuunganishe nguvu zetu ili tuondokane na umasiki unaotukabili kwa ujumla wetu, na sio vilio vya Pemba twaonewa tu. Amka Baba.
   
 10. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nani kakwambia kura haziibiki Pemba. Uliza usiyoyajua Baba, Wewe hujui kuwa huko ndio eneo la CUF kuiba kura na kuuchezea uchaguzi watakavyo. halafu wanazusha lawama za uzushi. Au kwa kuwa CCM haijapiga kelele. Na kwa nini ilalame wakati inajua hata CUF waibe namna gani Pemba kwa nguvu ya CCM iliyopo Mkoa Kaskazini Unguja, na Mkoa Kusini Unguja, CUF hawawezi wakashinda uchaguzi daima.
   
 11. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kaka haiingii akilini mtu haibiwe na asilalamike, Pemba haibiwi mtu kura na ndo maana CCM hawawezi kushinda lakini unguja kwenye mikono mingi ndo maana wanashinda.
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sio wote wa Bara tunakuunga mkono kwa maneno yako za kibaguzi dhidi ya mwenzio.

  Napinga na kudharau mawazo yako ya kikabila kwa moyo wangu wote.

   
 13. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kama adhabu kwao kwani si wakati huu tu toka enzi na enzi maendeleo Pemba hayaendi wa kasi na inasababishwa na mambo mengi mojawapo ikiwa ni huo upinzani kwa serikali. Lakini la kujiuliza Wapemba wenyewe wamefanya juhudi gani kujaribu kurekebisha hili licha na kulia na Seikali tu ambayo wanajua kuwa haitawasaidia kitu.

  Jee CUF ambao wanaungwa mkono huko wamechukua hatua gani ya kuwasaidia wanajamii wa Pemba kuongeza kipato chao na kuboresha maisha yao? Wana wawakilishi na wabunge wengi kuliko mkoa wowote wa Tz kwa hivyo kama wakiamua kutoa nusu tu ya zile pesa wanazopewa kwa matumizi ya jimbo basi ingesaidia japo kidogo.Wangeweza kuonjesha njia na kutumia wadhifa wao kuzisaidia NGO zilioko Pemba kuwezakuomba misaada na kuleta miradi ya maendeleo - lakini wapi ni kuwatumia tu kama wengine wanavyotumiwa na CCM.
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bi Kirembwe,

  Ni sawa kuwahoji CUF wamefanya nini, lakini wao hawaushiki mfuko wa Bajeti za matumizi au maendeleo. Wanachopewa wao ni ruzuku na mishahara. Sasa unatarajia vipi hata wakitoa michango ya 10% ya mishahara yao kuwa Pemba kutakuwa na maendeleo?

  Maslahi ya Pemba na Wapemba ni jukumu la kila mtu na dhamana kubwa imepewa Serikali ya Muungano na Serikali ya Baraza la Mapinduzi. Ikiwa dhamira za Wapemba ni kuwa wao haikubali CCM, ndipo basi Serikali ya CCM iamue kuwaadhibu kwa makusudi, huoni kuwa hiyo ni ubaguzi na dhambi?
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tujaribu kuwa na upeo mpana katika kujadili hii kadhia... Pemba ni sehemu ya Zanzibar na imekuwa ikipata mahitaji ya lazima kama inavyohitajika na kadiri ya uwezo wa SMZ. Katika kuhakikisha hilo kila kinachofanyika Unguja katika eneo la maendeleo basi hufanyika vilevile huko Pemba.

  Ujenzi na matengenezo ya barabara yafanyikao Pemba huenda sambamba na yale yafanyikao Unguja. Ujenzi wa Nyumba, hospitali, skuli n.k yote hufanyika sawa na Unguja.

  Tatizo kubwa la kisiwa cha Pemba ni Umeme, ambapo hadi leo wanatumia majenereta hivyo kuwa ghali mno na kufanya upatikane kwa mgao. Hata hivyo zipo juhudi za kufunga umeme tokea Tanga kwa mfumo ule ule wa kidatu-unguja.

  Kuna Matatizo ya maji, lakini haya yanatapatiwa uvumbuzi kwa ushiriki wa Wakaazi wa Pemba na SMZ.

  Katika Awamu zote za SMZ, awamu ya Karume imefanya mengi mno huko Pemba kuliko awamu zingine zote ukiondoa awamu ya kwanza ya Marehemu Karume.

  Hata hivyo jitihada nyingi za SMZ zimekuwa zikifunikwa na ushabiki mkubwa wa kisiasa, na hasa ikizingatiwa kuwa huko Pemba ndio ngome kuu ya CUF. Waakazi wa huko wengi wao hawapendi kuishi huko na kila mmoja apatae nafasi ya kuondoka kule hufanya hivyo na wengi hupenda kukimbilia Mkoa wa Mjini Magharibi. Hili ni tatizo ambalo lipo dunia kote la watu kukimbilia mijini. na sio huko Pemba pekee.

  Tatizo la mafuta Zanzibar lipo na litaendelea kuwepo iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kuondoa ukiritimba katika usambazaji wa mafuta visiwani humo. Meli inayotumika kuleta mafuta Zanzibar ni ndogo na hata hailingani na ukuaji wa kasi wa visiwa hivyo, ingawa kuna wakati fulani fulani meli zingine zimekuwa zikikodiwa kuleta mafuta visiwani humo. Meli ya sasa ilinunuliwa wakati ule wa awamu ya kwanza. Na sasa imeshachoka.

  Msambazaji wa mafuta ni mtu/kampuni moja mmoja, hakuna ushindani wa kuleta na kusambaza mafuta visiwani humu. Hii inatokana na kuwa SMZ ndio wapangaji wa bei. Sehemu za kuhifadhi mafuta visiwani humo ni ndogo mno.

  Hakuna sehemu yeyote ile katika Tanzania ambayo unaweza kuuziwa mafuta katika mfuko wa Rambo zaidi ya Zanzibar. Hii pekee inaonyesha ni kwa namna gani mafuta ni tatizo visiwani humo. Bei ya mafuta katika visiwa hivi ni tofauti kabisa na ile ya Bara, na hili ukiliangalia kwa upeo litakupa hali halisi ya upatakinaji wa mafuta visiwani humo.
   
 16. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe Rev. na kweli hii ni dhambi - na ni kama ile dhambi ya asili ambayo wanadamu sote tunayo na kwa Wapemba kwa vile hawajataka kubadili mtazamo wao kwa Mapinduzi dhambi hii itawaandama milele.
   
Loading...