Marangu: Mabweni ya Shule ya Sekondari wasichana Ashira yanayeketea kwa moto

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,406
2,000
Mabweni ya shule ya sekondari wasichana Ashira,iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro yanateketea kwa moto.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi.Anna Mghwira amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza kuwa askari wa kikosi cha zimamoto wanaendelea na jitihada za kuuzima

=====

Mabweni ya shule ya Wasichana Ashira yateketea kwa moto

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa amepokea kwa masikitiko ajali ya moto iliyotokea leo Mei 23, 2019, kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.

Mghwira amesema kuwa bado hajapata tathmini kamili ya ajali, lakini Kamanda wa Polisi mkoani humo ambaye amewahi eneo la tukio, amemweleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa hakukuwa na mwanafunzi bwenini.

”Shule ya Ashira ni miongoni mwa shule kongwe ambazo zipo kwenye mpango wa kufanyiwa marekebisho na niliitembelea hivi karibuni, lakini nasikitika leo imeungua upande wa mabweni. baadaye tutapata tathmini maana Kamanda yupo kule na RAS naye amekwenda,”amesema Mghwira
Mapema leo Mei 23, 2019, majira ya saa 6:00 mchana ulizuka moto shuleni hapo na kuunguza mabweni ya wanafunzi.
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,754
2,000
hii shule ni ya watanzania wote, wanasoma watoto kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hii, WATANZANIA KWA UMOJA WETU TUICHANGIE SHULE HII MAALUMU YA KITAIFA
Ile shule tuliijenga sisi watu wa marangu maana serikali ilikuja kuuchukua. Moshi shule tunajenga sisi serikali haitii mkono wake ila sasa shule ikishakamilika ndo serikali inakuja na kunyang'anya. Ni shule yangu ile na nilishaichangia
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,754
2,000
#watu mna roho za kwann, kwan kama kungekuwa siyo nyumbani usingechangia..

#na sisi hatachangii sasa kwa kuwa siyo kwetu.
Jamani nilishiriki jamani kwenye harambee ya kuiboresha pale jamani alafu ni karibia na nyumbani kwetu

Mimi nimesema hivyo kwa sababu ni jadi yetu kuchangia mbona tunachangia kwa wengine kama kwa Tundu lissu, yule mtoto kule kwa page ya Mange, tumechangia kwenye tetemeko, lucky vicent ile ajali etc

Mimi ni mdau wa elimu sipendi watoto wetu wapate shida. Kuna sehemu moja nilipita walikuwa wanachangishana ujenzi wa bweni kule Ngudu nikashangaa sana watu walikuwa wanalalamika eti wanabebeshwa matofali na shule mpaka leo haijakamilika

Anyway nimepakumbuka nyumbani
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,754
2,000
Tushawahi sema humu, wachaga ni wabaguzi saaana,... Wakubali wakatae,... Itabaki kuwa ukweli...
Huo ubaguzi ni upi wewe kusema mtoe account namba kwa ajili ya kuchangia bweni la watoto wa kike ili wasifanyiwe kitu kibaya ndo wabaguzi

Tulishawahi kukubaguaje kama hela ni kweli tunazo lakini hatutoi ata ndururu. Mtafute na nyie alafu muache kusema sisi ni wabaguzi sema tulishakubagua nini
 

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,754
2,000
Mchagga akisema nyumbani kwake kuna shule na imejengwa na wenyeji ndiyo imekuwa ubaguzi?

Vyasaka mna tabu sana, na hii tabu itabakia kwenu vizazi na vizazi.

Too inferior!
Waambia hawa watu nikishakaa Kwimba tukataka jenga shule moja tukashirikiana na mbunge wa kule lakini nilishangaa hakuna mwamko. Watu walikuwa wanalalamika kwamba wanabebeshwa matofali.

Ila ndo hivyo aliyelala amelala tuuu acha tuujenge mkoa na shule zetu mkija karibuni sana ila muwe na pesa ukiwa kapuku ata udondoke hapa hatukunyanyui ng'ooo na kama tukikunyanyua tutakupiga sachi nyinyi laleni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom