marandu: mgombea wa ccm ni mtoto wa baba na mbabe- hafai kuchaguliwa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

marandu: mgombea wa ccm ni mtoto wa baba na mbabe- hafai kuchaguliwa!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Oct 18, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  joto la kampeni za uchaguzi limezidi kupanda hapa dodoma baada ya malumbano ya hoja za kuchafuana kwenye kampeni za kuwania udiwani kata ya kizota baada ya joseph marandu wa chadema na juma bakari wa ccm kufikia hatua hiyo; huku kila mmoja akituma 'vipandikizi' vya kupata habari na kufanya mrejesho kwa mhusika.

  hayo yalionekana zaidi jana kwenye kampeni za udiwani za chadema kwenye kata hiyo yaliyokuwa yakifanyika kwenye mtaa wa salama kwenye viwanja vya nkuhungu stedi wakati marandu akiwasilisha ahadi zake kwa ngazi ya kata.

  akijibu mapigo ya mgombea bakari wa ccm,omari bakari alizotoa siku 2 kabla ya mkutano huo wa kampeni, kwenye viwanja hivyo hivyo, ( ambapo bakari aliwasihi wana kizota kutokumchagu marandu kwa kuwa bado ni 'bwana mdogo' tena anaishi kwenye nyumba ya kupanga), bw marandu (huku akivaa kombati la chadema) kwa ujasiri mkubwa;

  • alikiri kuishi kwenye nyumba ya kupanga ambapo amedai kulipa kiasi cha shilingi laki moja kwa mwezi; lakini akasisitiza kwamba kwa msingi huo bakari (ccm) ndiye hafai kuchaguliwa kwa sababu anaishi kwa baba yake mzazi, akauliza wananchi kwamba ikiwa mwenyezi mungu ataamua kumchukua mzazi wa bakari, bakari ataingia kwenye ugomvi wa urithi na hata kuwa na uwezo wa kupanga nyumba pindi atakaposhindwa kuwadhulumu nyumba wadogo zake ambao ni wengi kwa idadi.
  • kuhusu kwamba yeye ni bwana mdogo, alitoa mfano wa zitto kabwe ambaye aliingia bungeni akiwa na umri wa miaka 28 tu; sembuse yeye ambaye sasa anakaribia miaka 31.
  • bakari hivi karibuni alitembeza kibakora kwa waandishi wa habari, kisha akapigana msikitini answar sunna na hivyo ni mbabe kunakopelekea kutafaa tena kuwa mwakilishi wa wana kizota
  • akasisitiza kwamba endapo bakari, alishindwa kuwasaidia wana kizota kwa muda wa miaka 15 aliyokuwapo madarakani kama diwani, atawafanyia nini wana kizota?
  • akasisitiza tena kwamba akipewa fursa ya udiwani atahakikisha ndani ya miaka 2 ana tatua matatizo ya wana kizota kwa njia shirikishi tofauti na bakari ambaye haitishi mikutano na badala yake huishia kwenye chama chake tu.
  • akaahidi kwamba endapo atapewa hiyo ridhaa atahakikisha hakuna bomoabomoa ya uonevu kwani hatatia saini documenti ya cda ambayo kwa kawaida husainiwa na diwani wa kata husika; kama alivyoshawishika bakari kwa mlungula wa cda (akataja kiasi) kulikopelekea watu wa mtume, na bochela kubomolewa nyumba zao.
  mamia ya watu waliohudhuria walimshangilia kijana marandu na kumkubali kwamba watampa ridhaa ya kuwa diwani wao wa kata ya kizota.

  kabla ya kujibu mapigo hayo, marandu aliwasihi watanzania kumchagua kiongozi kwa kuangalia uwezo wake na sio chama chake. akaahidi kutumia njia shirikishi kutatua matatizo yafuatayo katika kata ya kizota;

  • maji (tatizo la duwasa kubambikiza ankara za maji)
  • elimu ( kupata walimu wa kutosha kwenye shule 2 zilizopo katika kata hiyo badala ya wale wa part-time waliopo sasa; na kufuatilia matumizi ya fedha za capitation kwa shule za msingi na upili zilizopo kwenye kata hiyo. msisitizo ukawa ni elimu bure kwa ngazi ya kitaifa.
  • afya ( kupata zahanati na kituo cha afya; hakuna kwa sasa)
  • kusukuma upatikanaji wa kata mpya ya nkuhungu ; kitu ambacho bakari amekibania kwa miaka 15 kwa sababu za kisiasa; ambapo inasemwa ya kuwa eneo la nkuhungu ni ngome ya chadema na kizota ni ccm na chadema zinagombania kwa ushawishi.

  ama kwa hakika , kijana marandu anafaa kuwa mwakilishi wa kizota!!

  naomba kuwasilisha!!!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Siasa na vinywa/midomo ina wenyewe. chota kila neno la wagombea kwa uangalifu usije chukuliwa na upepo wa kisiasa ukaangukia mavumbini.
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mimi binafsi nilihudhuria mkutano huo wa kampeni jana wakuu.
   
Loading...