Marando sasa apaa na helikopta ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marando sasa apaa na helikopta ya Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Marando  *AAHIDI KUMPIGIA DEBE DK SLAA NCHI NZIMA

  Ramadhan Semtawa

  WAKILI na mwanasiasa mwanzilishi wa mageuzi, Mabere Marando, amejitoa NCCR- Mageuzi na kujiunga Chadema huku akieleza kuwa atakata mbuga nchi nzima kuhakikisha Dk Willibrod Slaa anashinda urais mwezi Oktoba.

  Marando amejiunga na Chadema katika kipindi ambacho Dk Slaa, amechanganya hisia za watu huku baadhi wakiuona uamuzi wa kukubali kuingia mbio za urais ni sahihi na wengine kuuona uamuzi huo kuwa sawa na kujimaliza kisiasa.

  Akizungumza na wahariri na wawakilishi wao jijini Dar es Salaam jana, Marando alisema: “Nimejiunga Chadema ili nishiriki kuiondoa CCM madarakani.”

  “Chadema ni chama ambacho kimefanya kazi kubwa ya siasa ikiwemo Operesheni Sangara. Niliwahi kumwambia Dk Slaa akiingia katika kuwania urais, nitakata mbuga nchi nzima kuhakikisha anashinda. Dk Slaa ana uwezo mkubwa.”

  Marando alifafanua, yeye na waasisi wenzake wa mageuzi wamekuwa na malengo mawili makuu, ambayo kwanza ni wananchi kufahamu umuhimu wa mfumo wa vyama vingi na pili, kuanzisha vyama kwa lengo la kuing’oa CCM madarakani.

  Aliongeza kwamba:, “Kwa hiyo kuhamia Chadema sijapotea njia, Chadema ni wapambanaji na mimi mapambano ni asili yangu.”

  Kwa mujibu wa Marando ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kabla na baada ya kupigwa na dhoruba ya kisiasa, alisema Chadema ni chama ambacho kimeweza kujiimarisha kisiasa, kutoa mwamko kwa wananchi na kuinua nguvu za mageuzi nchini.

  “Kwa hiyo, wanaosema Dk Slaa kugombea urais ni kujimaliza, hawako sahihi. Dk Slaa anahitajika zaidi ya Karatu, anahitajika nchi nzima,” alisema na kuongeza:,

  “Hao ni waoga, wanaogopa wanajua kuna Challenge (changamoto) kubwa ambayo rais Kikwete atakabiliana nayo kutoka kwa Dk Slaa.”

  Marando alisema ni kweli Dk Slaa ameweza kutoa mchango mkubwa bungeni, ameweza kuibua mambo mazito, anajua kuchambua mambo kwa kina, lakini alisema mchango wake (Slaa) sasa unahitajika kwa nchi nzima.

  “Kwa sababu Tanzania ni kubwa kuliko Karatu, hata leo (jana) pale ofisini kwangu nimekuta watu wanasema hivyo Dk Slaa kakosea. Ilibidi nitulie nikachukua muda kuwaelimisha kidogo.”

  Marando alikisifia Chadema kuwa kimetoa mchango mkubwa bungeni na ni chama chenye mawazo mazuri, wabunge wake wachache wameweza kuibua mambo mengi bungeni.
  "Hata hizi ajenda za ufisadi ni za akina Dk Slaa na akina Zitto,” alisisitiza Marando na kuongeza:

  “Nani angejua mambo ya EPA kama si akina Dk Slaa? Nani angeweza kujua haya mambo ya madini kama si Zitto? Hata CCM wamedandia hoja hii, kwa hiyo utaona mchango wa Chadema ni mkubwa.”

  Alisema kwa kifupi, ni wabunge wachache wa upinzani hasa wa Chadema ndiyo wameonyesha na kuamsha watanzania kuhusu nchi yao inavyoliwa na iilivyokosa uongozi makini.

  Wakili huyo alisema kwamba, nafasi ya chama cha upinzani si kukosoa na kushauri chama tawala, bali ni kuhakikisha wanaing’oa CCM madarakani.

  Kuhusu yeye kama ataogombea Rorya, alisema hatagombea nafasi yoyote si ubunge wala udiwani isipokuwa ameamua kujiunga Chadema kuongeza nguvu ili waweze kuing’oa CCM.

  Alipoulizwa haoni kuingia Chadema ni kudandia mafanikio wakati aliacha kuimarisha chama chake cha NCCR, alijibu:,” Ni kweli kabisa nimedandia mafanikio. Ila hilo neno la kudandia kidogo linanipa tabu.”

  “Lakini, siku zote watu wenye malengo ya kisiasa wanaangalia sehemu ambazo kazi ya siasa imefanyika kama chama ambacho kina matawi, ndiyo maana unaona maprofesa kutoka vyuo vikuu wanakwenda CCM wanajua tayari kina matawi kila sehemu huku kwetu wanaogopa. Mimi nimeamua kuunganisha nguvu na wenzangu wa mageuzi.”

  Juzi, Kamati Kuu Chadema ilimpendekeza Dk Slaa kupeperusha bendera ya chama hicho katika mbio za urais wa Oktoba, hatua ambayo imebua mgawanyiko wa mawazo miongongoni mwa watanzania.

  Wananchi wa Karatu juzi waliandamana kupinga Dk Slaa kuwania kiti hicho cha urais wakimataka aendelee kutetea kiti chake jimboni humo.

  Chanzo ni http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/3414-marando-sasa-apaa-na-helikopta-ya-chadema

  Hongera Mzee Marando ningeomba na viongozi wengine waige mfano wa Mzee Marando. Ili kuweza kukishinda Chama Tawala CCM.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Askari wa mwavuli huyo! Au?
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Marando siyo mnafiki kisiasa wala hanunuliki kwa sababu yoyote ile kama mabavyo wanasiasa njaa walivyo; hakuwa na haja ya kujiunga na chma chochote baada ya NCCR yake kufa. Nikikumbuka jinsi alivyofanya kazi ya ziada chini ya NCCR (kabla hata hakijawa chama cha siasa) kuwafunulia watanzania kuwa hawakuzaliwa kutawaliwa na CCM tu, ninabaki na imani kuwa he can do something for CHADEMA.

  NCCR ilibadilisha sana mawazo ya watu kiasi kuwa hata machinga wengi hapo Dar walikuwa wanavaa tai kuwaiga wanasheria wa NCCR waliokuwa wakivaa tai kama Marando na Lamwai, wacha ndugu yangu. Tusubiri tuone mwisho wake.
   
 4. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  kICHUGUU MIMI NAKUUNGA MKONO 100% kURA KWA DR.SLAAA KURA KWA CHADEMA KURA KWA MARANDU. CHADEMA OYEEEEEEEEEE,
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hapo penye bold sina hakika kama ni kweli. Mkuu acha kutufunga kamba bana.
  Besides, Mgombea wa URAHISI wa NCCR Mageuzi bado kutangazwa?
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Marandu aungwe mkono na wapiganaji wenggine wenye nia ya dhati.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nasema kufa kwa maana ya kukosa nguvu na mwelekeo kama kilivyokuwa miaka ya 1994 hadi 1996. Najua bado chama hicho bado kipo kwenye vitabu lakini hakina nguvu kama zile za miaka hiyo mitatu nilyosema.
   
 8. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Karibu chadema mzee marandu
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Duh Mkuu una Obsession na Dr Slaa kweli kweli sasa hilo neno Mwenyewe la nini wakati Topic ina mhusu Marando
   
 10. Mpiganaji tz

  Mpiganaji tz Member

  #10
  Jul 25, 2010
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HODI wana JF.
  Baada ya kifo cha Hayati Chacha Wangwe baadhi ya watu walijaribu kmtuhumu mhe. Freeman Mbowe kuhusika na kifo kile eti kwasababu hayati Wangwe alikuwa ngangari ktk kuikaba koo serikali ya CCM pale ilipovurunda!

  Sikutaka kuamini tuhuma hizo kwani imani na mapenzi niliyokuwa nayo juu ya mhe. Mbowe vilikuwa ktk kiwango cha juu mno. Ila kitendo cha mhe. Mbowe kufurahia Chadema kumsimamisha Dkt Slaa kuwania urais kinanipa shaka. Kwanini Mhe. Mbowe afurahie mpiganaji kama yule kuondoka bungeni? Kitu cha pili kunipa wasiwasi ni kitendo cha Marando kuruhusiwa kujiunga na Chadema! Marando anafahamika vyema alivyo kigeugeu na inasemekana marando ni ile type ya Mrema sasa kwanini mhe. Mbowe hakutumia influence na position aliyonayo ktk chadema azuie mtu kama Marando kujiunga na Chadema? Napata wasiwasi hapa!!

  Kumbuka wote Mrema na Marando walikuwa NCCR mageuzi. "Wamekiua" kile chama! Mrema akatinga TLP nayo kaipotezea mwelekeo! Kesho haijulikani atatua wapi, sijui atakuwa amemaliza kazi na kurudi "nyumbani" I mean CCM au...? Na huyu Marando amekuja kuimaliza Chadema!!

  Wana JF naomba maoni yenu juu ya wasiwasi wangu kwa mhe. Mbowe.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema na viongozi wote wa kweli ktk kambi ya upinzani.

  Si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila kusema kweli naipenda Chadema, nawapenda viongozi wake hususan Slaa na Mbowe.

  ndimi mpiganajitz@gmail.com
   
 11. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Usemacho Kina ukweli kidogo, japo mimi nitapingana kidogo, kwanza marando hawezi kukataliwa kujiunga na Chadema kwa sababu kule ni chama huru tena cha Demokrasia. Hivyo hata wewe unaweza kujiunga leo hii. Ila sisi tutamshangaa Mbowe na hata Dr, Slaa mwenyewe kama watamuruhusu jamaa kumpa uongozi wowote.
  Kwasababu hawa jamaa hawana msimamo,
  Ni wavurugaji,
  Na ni mashushushu kama si wavurugaji wa Demokrasia nchini.

  Sasa Mbowe kufurahia Dr. Slaa ni kwamba ameshaona yeye kwa sasa hawezi kupata chochote, katika urais ukitegemea kipindi kile alifanya kazi na mavuno yakawa vile. So, Dr. kidogo kavuna sifa na anaweza kufurukuta katika urais. Mbowe si CCM ila Marando
  kama Mbowe atakuwa CCM basi na Dr. slaa atakuwa hivyo maana kwa uelewa wangu angejua na asingekubali kwenda kicwa kichwa kuliachia jimbo kirahisi tu! pia Mbowe anataka naye ale kidogo hizo milioni za ubunge kakaa nje kwa mda mrefu hadi kajisikia baridi. Ngoja aingie kama ataweza.
  Usiwe na hofu mbowe ni Chadema hayupo kama Mrema
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Karibu mpaka ndani. Naona hii ndo post yako ya kwanza kabisa. Tunakukaribisha.
   
 13. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Asante babu yao! Kweli wewe unastahili sikuona kabla ya kuchangia. Akaribie sana, na hata hivyo haikuwa vema kumkaribisha mimi kabla ya BABU YAO!
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watu kwa spinning hawajambo ........nampenda .........simpendi..........nampenda....alimradi siku hazigandi.
   
 15. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  MTWA usemacho ni kweli kabisa huyu Bwana Marando hata mie simwamini kabisa. game alolicheza yeye, Dk. Lamwai na Mrema kule NCCR kwa kweli inabidi wawaombe radhi wana mageuzi maana wao wamekuwa sababu kubwa sana ya upinzani kuzorota nchini Tanzania. na hakuna asiyejua kuwa huyo Marando ni sumu kwa vyama vya siasa. Haiwezekani mtu ajiunge na chama leo eti kesho tayari yupo kwenye kampeni team. tena anahamia after kusikia Dr Slaa kateuliwa kuwa Mgombea urais. This guy is kidding with Tanzanians tunaopenda mageuzi ya kweli. Chadema you dont need Marando in your compain team ama la mtajutia kumpokea. Hivi sasa wanaCCM wanafiki wengi tu watakimbilia CHADEMA you ll see them. lakini hawaji kwa mema hata kidogo bali kutafuta njia m badala ya kuneemesha matumbo yao. Please Please Chadema dont allow that.

  Kama kweli huyo marando anaikubali chadema mpeni miaka miwili tu awe kwenye chama kama mwanachama wa kawaida muone kama ataweza. Huyo alipotoka tu NCCR CCM wamempa ubunge wa Africa mashariki.

  Jamani lets say NO for Marando in chadema campaigns.
   
 16. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,227
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Marando ni askari wa siri wa CCM, kazi alionayo ni kuja kusoma technique za CHADEMA na ku report back kwa BOSS wake JK, Nyie CHADEMA mruhusuni tu aingie kwenye Ngome yenu mtakuja kutuambia. Anawezaje kumpigia Debe Dr Slaa leo wakati alishidwa kufanya hiyo kwa Mrema alipokuwa huko NCCR? Atuambie watanzania wanamwamini kiasi gani hata wawe tayari kusikiliza Debe lake? Walioanza kuijenga CHADEMA waachwe wamalize kazi yao. Mtu asije kujitafutia umaarufu kwamba he was key Player on CHADEMA presidential success. Hawa watu wasio na misimamo kutulia kwenye vyama vyao ndio mwiba wa kuepuka katika dakika hizi za mwisho kuelekea uchaguzi. Kama kweli wanakipenda chama walipaswa waingie CHADEMA mapema sio miezi 3 kabla ya uchanguzi. Kwa kipindi kifupi hivyo mtu atawezaje kuelewa Sera na ilani ya chama na kuweza kusimama kuitetea? Au wanataka kutuletea kampeni za matusi na mipasho?

  Kwenye Kampeni team ya urais hao new comers wasipewe nafasi kwa sasa. Waende wakatafute ubunge, tena sehemu ambapo CHADEMA haiko imara ili waiimarishe.
   
 17. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Chadema tujipange Marando hana sera jipya zaidi ya Agenda ya siri aliyonayo ya Kuwania U RAIS 2015 through Chadema, with full suport ya ccm ccm ccm.CCM kitamuhunga mkono kama kililivyomuhunga mkono 2001 Ubunge wa EA ,Na ndio itakuwa mwisho wa Chadema,Tujifunze yaliyotokea NCCR -Mageuzi

  ''forgive your enemy but never forget his Name"
   
 18. bona

  bona JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  it was a bad idea kwa slaa kugombea urais, timing sio proper, nchi hii ina wapumbavu wengi sana ambao hawajali uwezo wa mtu bali chama na kuogopa vita, ingekua kura si idadi slaa angeshinda, ingekua kura zina different weight kutegemea na elimu na uelewa basi slaa angeshinda, jk hategemei kura za wasomi au waelewa ambao ni wachache, yeye ana take advantage of majority ignorance kushinda! kwenye biashara inaitwa kutake advantage of customer ignorance unauziwa kitu usichojua technolojia yake unaambiwa ni bora kwani you can not tell otherwise.
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  To me Marando is a "spoiler" - Ni Mr "Y"
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  ''twendeni tukatekeleze maneno yetu kwa vitendo'' blabla hazitufikishi popote... tuanze tupige hatua kwa kupunguza kusema na kuongeza kutenda...
   
Loading...