Marando na Prof Safari nao wamcharaza Nape ile mbaya

Hivi nyie CDM mbona mnafikir chama chenu ni untouchable wakati sisi tunajua kwamba nayo ina mapungufu mengi sana ambayo nilifikiri huu ndiyo wakati wake wa kuyafanyia kazi kama mnataka chama chenu kije kipewe dhamana ya kuongoza nchi hii hapo baadae. Kuna utoto na ushabiki wa kijinga humu ndani na fikra za kwamba wao CDM peke yao ndiyo wana hati miliki ya kuzungumzia ufisadi, na kwamba mtu aliye CDM ni malaika.

CDM you are not indispensable, kama kuna ufisadi tutausema na ni vizuri wafuasi wake wawe na maturity na kuelewa kwamba nao wanafanya makosa na inapotokea hivyo waache juvenile arguments na ku-attack personalities.



Come down dear - come down!
IIIINSHU iko hivi: Nape - huyu katibu mwenezi wenu wanted to jumb ship, yaani alitaka kuhamia CHADEMA ili agombee ubunge jimbo la Ubungo baada ya kutemwa na CCM lakini Mnyika wa too good to be left uwani. Sasa kabla ya kumshambulia jirani yako CHADEMA jiulize how loyal is that mouthpiece of yours?
 
Marando na Prof Safari nao wamcharaza Nape ile mbaya

Wakati makamanda wakuu wako huko kusini wakiendelea na ile ‘twanga kote kote' nasikiavyo hapa Dar makamanda wengine – Mabere Marando na Prof Safari le wametema cheche kali – pande zote mbili wakimjia juu yule dogo wa CCM – Nape – kwa harakati zake za kujaribu kuisafisha CCM kwa usanii tu.
[FONT=Arial[SIZE=4]]Nasikiavyo hawa wa Dar wamechakaza kabisa Nape kwa kumuelezea kwamba haiwezi kazi hiyo aliyopewa kwani naye ni fisadi mkubwa – akihusishwa na kufaidika na hela za EPA za Jeetu Patel.[/FONT]

[/SIZE] Marando anapoeleza waliofaidika na hela za EPA ni authority tosha kwani yeye anajua maana anamtetea Jeetu. Anamtetea Jeetu kwa sababu msimamo wa huyu mdosi ni kwamba hakurudisha hela za EPA, anashikilia kwamba nyingi ya hela alizokwapua walichukuwa CCM wenyewe – akiwemo Nape (na JK wake) etc etc.

Nadhani haya yote yatawekwa hadharani kesi ikifikia mahala husika.

Mimi hayo yote nimeyasikia kwa swahiba wangu ambaye ni ripota wa gazeti moja aliyekuwapo kwenye hiyo briefing ya akina Marando. Mwenye habari kamili atusaidie kuongezea hapa, au kurekebisha.

- Great Thinking sana!, what a genius!

FMEs!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, hajawahi kuomba wala kushinikiza alipwe mshahara mnono.

Badala yake, chama hicho ndicho kilimshinikiza na kumwomba kimlipe vizuri, chini kidogo ya maslahi ya Mbunge, kwa kuthamini mchango wake katika uchaguzi mkuu uliopita, hasa ikizingatiwa kuwa kama angegombea ubunge angeshinda, lakini alikubali ombi la chama la kugombea urais, ambao alishinda akachakachuliwa.

Chama hicho kimesema kitaendelea kuenzi mchango wa Dk Slaa kwa kumwezesha ipasavyo ili asitetereke katika kukiongoza CHADEMA kwenye harakati na mapambano ya kukiondoa CCM madarakani miaka minne ijayo.

Malezo hayo yalitolewa jana na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu, alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam.

Komu alikuwa ameita vyombo vya habari kuzungumzia alichokiita porojo za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama, ambao wameamua “kujilipua” kwa kuwatetea mafisadi wakubwa ndani ya chama kw akigezo cha kujivua gamba.

Alisema kinachowauma CCM ni kwamba wanatambua kwamba Dk. Slaa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe wakiendelea kusitawi, ndiyo mwisho wa utawala wa CCM.

Komu alisema kauli za viongozi wa CCM wanaotapatapa haziwezi kukinusuru chama hicho tawala, na haziwezi kukizuia CHADEMA kufanya kazi yake ya kuwatumikia wananchi kwa kuwaamsha dhidi ya watawala wabovu.

Alisema kauli za Nape ni propaganda zisizo ma mashiko, ambazo Watanzania watazipuuza, kwa sababu wanajua kazi nzuri iliyofanywa na Dk Slaa na wenzake wakiwa Bungeni, wakati wa uchaguzi na sasa katika operesheni inayoendelea kuamsha wananchi juu ya haki zao na wajibu wa serikali.

Alisema kauli za Nape hazitapunguza kasi ya CHADEMA kupambana na mafisadi, kwani haziwezi kupunguza ugumu wa maisha ya Watanzania, wala hazitaweza kudhibiti mipango mkakati ya chama hicho.

Kwa nyakati tofauti, Mukama na Nape wamekaririwa wakiwashutumua viongozi wakuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, kwa maelezo kuwa wameshnikiza mshahara mkubwa wa Sh milioni 7.5 kwa Dk Slaa, na uuzaji wa magari matatu ya Mbowe kwa pesa nyingi mno.

Komu jana alisema kwanza Mukama na Nape wanapotosha umma kuhusu ukweli wanaoujadili, na akasema hata hiyo sehemu ya ukweli wanaougeuza tuhuma imeshapitwa na wakati, kwa kuwa CHADEMA hakifanyi mambo kwa kificho, na kilishafafanua hoja hizo.

Alisema Dk. Slaa hajawahi kushinikizwa alipwe Sh.7.5 milioni. “Kwanza, hatumlipi kiasi hicho, lakini pia Dk. Slaa hajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka kuaminisha umma,” alisema Komu.

Badala yake, alisema, chama ndicho kilipanga jinsi ya kumwezesha Dk Slaa kwa kuwa ndicho kilichomwomba agombee urais, huku kikujua kuwa angegombea ubunge na kushinda kirahisi.

Lengo la chama kufanya vile ni kumwezesha Dk Slaa kutenda vema kazi zake za katibu mkuu kama alivyokuwa akitenda kazi za ubunge; hivyo kwa pamoja wakakubaliana awezeshwe kulingana na masharti ya utumishi katika nafasi ya ubunge.

Huku akikosoa takwimu za Nape, Komu alisema Dk. Slaa analipwa Sh 7,174,000 kama kwa mwezi, na si Sh. 7,500,000.

Alisema vilivyochukuliwa vipengele vichache sana katika marupurupu ya mbunge, hivyo si sahihi kusema kuwa Dk. Slaa alipwa sawa na mbunge.

Mkurugenzi huo yalisema vipengele hivyo ni mshahara wake Sh. 1,725,000, wakati mbunge analipwa Sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

Komu alisema kiongozi huyo analipwa mafuta ya kwenda ofisini na kurudi nyumbani kwake lita 30 kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi; kwa bei ya kila lita moja Sh. 2000.

Wakati mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi kwa bei ya kila lita moja Sh. 2,500, bei ambayo haipo, lakini Bunge limeridhia kulipa.

Alisema sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka pendekezo hilo katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu kupitishwa kwa njia ya uwazi na likaingizwa katika mpango kazi wa chama.

“Wakati wote wa kujadili pendekezo hilo, Dk. Slaa aliachia nafasi yake na kikao kiliendeshwa na katibu wa Wanawake, Dk. Naomi Kaihula, ambaye ni mbunge wa Viti Maalum kutoka Mbeya,” ilisema.

Alisema mbunge akikaa katika kikao cha Kamati ya Bunge au akihudhuria mkutano wa Bunge analipwa Sh. 70,000 kama posho ya kikao, Sh. 30,000 posho ya mafuta na Sh. 80,000 posho ya kujikumu akiwa Dodoma.

Na akiwa Dar es Salaam, mbunge analipwa Sh. 50,000 kama posho ya mafuta, Sh. 70,000 posho ya kikao na Sh. 80,000 kama posho ya kujikimu huku fedha hizo zikilipwa bila kujali kama mbunge huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na amekwenda nalo Dodoma.

Akahoji: “Mbona hakuna mtu alishawahi kuuliza wakati hizo zote ni fedha za umma?”

Alihitimisha kwamba Dk. Slaa anastahili kulipwa kiasi hicho kwa kuwa aliombwa na chama kugombea urais, naye kukubali, zaidi kukubaliwa na umma pamoja na wanachama kutokana na ukweli wake katika kazi ya siasa.

“Baada ya kukubaliwa na umma, alionyesha umakini, umahiri na uwezo wa hali ya juu katika kujenga hoja zenye tija kwa taifa, na kwamba Dk. Slaa alithibitisha na bado anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni kiongozi bora na shupavu anayestahili kulipwa mshahara mzuri,” alisema Komu.

Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo Dk. Slaa alikuwa mgombea wao wa urais yanathibitisha kuwa hata bila kuzingatia uchakachuaji wa kura, ameanzisha ukurasa mpya wa mwisho wa mwanzo wa zama za mwisho wa CCM.

Akifafanua kuhusu tuhuma za Mbowe kuhusu kuuzia chama magari chakavu, alisema CHADEMA ndiyo iliomba kuuziwa hicho wanachoita “magari chakavu.”
Alisema hayo si magari ya kawaida na hayawezi kufananishwa kwa kiwango chochote na magari ya FUSO yanayotembea mitaani, na kwamba hiyo ni mitambo maalumu ya uenezi wa siasa.

Alisema katika magari hayo kuna vipaza sauti vyenye thamani ya dola za Marekani 148,000 sawa na Sh. milioni 222, jenereta tatu zilizonunuliwa kwa Sh. milioni 47 kwa kila gari kwamba yana bodi maalumu yenye uwezo wa kubeba watu wasiopungua 12.

Pia alisema magari hayo kila moja lina uwezo wa kubeba mapipa ya mafuta ya helikopta, jukwaa la kuhutubia na vifaa vya matangazo ambavyo vyote vimejengwa kwa Sh. milioni 48.4.

Alisema Mbowe aliombwa, na kamati kuu iliunda kamati ya watu wanne chini ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mohammed Issa kumwomba akiachie chama mitambo hiyo baada ya majadiliano marefu.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo, waliobariki kuwa ni Mabere Marando, Mkurugenzi wa Rasilimali, Suzan Lyimo (MB) na Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Aidha Komu alisema dai la CHADEMA kwamba inanunua magari chakavu si jipya kwao, kwani inao uwezo mdogo wa kifedha na kwamba imezoea kununua magari chakavu siku zote Japani na Uarabuni.

“Kwanza magari yanayozungumziwa chakavu yamenunuliwa nje na kuanzia kazi CHADEMA mpaka leo, na hayajawahi kutumiwa na Mbowe,” alisema
Alisema kama CHADEMA imeweza kuweka wazi hoja walizozielekeza kwao, ni vema na wao wakawaeleza Watanzania fedha walizozitumia katika uchaguzi mkuu na mshahara wa Katibu Mkuu wao Mukama, badala ya kukwepa hoja za msingi.

“Tunasisitiza kuwa CHADEMA imeweka wazi malipo ya viongozi wake, gharama za uchaguzi na vyanzo vyake vya mapato na jinsi inavyotumia mapato yake...tunaitaka CCM nayo iweke wazi malipo ya viongozi wake wakuu, gharama za uchaguzi na vyanzo vya mapato yake,” alisema.

Alisisitiza kwamba CCM ni chama cha kifisadi kwa kuwa viongozi wake ni mafisadi, wanafiki na wasio wa kweli kwa kuwa walikiri wenyewe katika hicho wanachoita kujivua gamba kuwa katika siku 90 wanachana na mafisadi.

Alisema CHADEMA wanataka kuona hilo likifanyika bila visingizio na kuelekeza mashambulizi kwa Nape hana hadhi ya kuinyoshe akidole chama kwa kuwa si mtu makini mwenye agenda kwa watanzania.

Na kwamba Nape anatakiwa kuonwa na watanzania ama kuitwa vuvuzela anayecheza ngoma asiyoijua na kwamba ni mnafiki, mzushi na mtu asiye na msimamo.

Komu alisema CHADEMA inao ushahidi wa kutosha kuwa ni mmoja wa watu walionufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia kwa kwa Jeetu Patel ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya kamati ya rais kwamba alitumia fedha hizo katika kampeni zake.

Komu alisema hivi sasa Nape analipwa mshahara wa ukuu wa wilaya na huku akilipwa na CCM na kutumia fedha za serikali kufanya kazi za CCM.

Alienda mbali zaidi na kusema kwamba baada ya kushindwa kupata nafasi ya kugombea Ubunge kupitia CCM aliomba agombee kupitia CHADEMA akakataliwa kwa kuwa hakuwa na sifa za kumzidi John Mnyika.

Mbali na hilo alisema pia ni mmoja wa waasisi wa chama cha CCJ na kuhoji iweje leo awe na ubavu wa kuionyeshea kidole CHADEMA?

Aidha alisema yeye (Nape) ndiye aliyetumwa CCM kuiwakilisha katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA 2010 na kukisifia chama hicho: “CHADEMA inaenda vizuri kama taasisi na kwa hoja.”

Katika hatua nyingine madiwani wa CHADEMA katika manispaa ya Kinondoni wanatarajia kuuelezea umma sababu ya kuibuka kwa vurugu katika baraza la bajeti la 2011/ 2012 lililoketi hivi karibuni.

Licha ya kuuelezea umma pia wanajipanga kutoa tamko juu ya kukiukwa kwa sheria na kanuni na baraza hilo kuamua kupitisha bajeti isiyokuwa na tija kwa wananchi.

Wakizungumza jana na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema kuwa umma unapaswa kufahamu yale yaliyojitokeza ndani ya baraza hilo ambapo bila kuweka jitihada za pamoja kuna uwezekano kata zinazoshikiliwa na wapinzani kushindwa kupata maendeleo.

Diwani wa Saranga Ephraim Kinyafu alisema kuwa bajeti hiyo imejaa uozo huku wakiacha kuweka kipaumbele katika masuala ya maendeleo.

Alisema ili kuondoa dhana ya madiwani wa chadema ni wakorofi suala hilo linatarajiwa kufikisha kwa wananchi na kuwafafanulia suala la milioni 95 kutumika kwa ajili ya ulinzi wa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

“Hata kama wameipitisha bajeti hiyo…tunaamini wananchi watakuwa waamuzi wetu tutawafahamisha sababu za sisi kuipinga bajeti maana haiwezekani mavazi ya madiwani yatengewe sh milioni 100 hizo fedha ni nyingi zipoelekwe katika miradi ya maendeleo,” alisema.

Alieleza kuwa iwapo manispaa hiyo ingeweza kuongozwa na chama hicho basi wanahakiki wangepiga hatua kubwa katika maendeleo kuliko ilivyo hivi sasa masuala ya anasa yanapewa kipaumbele.

Alifafanua kuwa imeshangaza kuona kuwa kata kubwa kama ya ubungo kushindwa kupewa miradi jambo ambalo linaashiria kuwa viongozi wa eneo hilo waonekane kwa wananchi kuwa hawawezi kuwajibika.

Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kawe, Esther Samanya alisema kuwa si kwamba madiwani walipanga kufanya vurugu bali walikuwa wakipigania maendeleo kwani haifurahishi kuona thamani za ofisi zikitengewa fedha huku miradi ya maendeleo ikipewa kisogo.

Alisema pamoja na kujitokeza kwa masuala hayo bado madiwani wa chama hicho wamepanga kutoa tamko na kupinga bajeti hiyo ambayo haina tija kwa wananchi.

“Hivi kweli viongozi makini wanaweza kuacha kuwapigania wananchi na wakasimama kwa ajili ya kutetea watumishi wa idara ambapo wanalipiwa maji na umeme wakati jukumu hilo si la manispaa,”alihoji.

Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/ 2012 ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilielezwa kuwa ya kifisadi, hali iliyosababisha kutokea kwa vurugu baada ya madiwani wa CHADEMA kuamua kuipinga.

Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya siku tano vya kamati za kudumu za madiwani wa Manispaa ya Kinondoni lakini katika hatua ya upitishaji wa bajeti hiyo, mabishano makali yaliibuka baada ya madiwani wa CHADEMA kuipinga bajeti hiyo wakieleza kuwa vipaumbele havijazingatiwa kwenye baadhi ya kata, huku wale wa CCM ambao ni wengi wakiiunga mkono.

Madiwani hao wa CHADEMA pia walihoji kiasi cha zaidi ya sh milioni 44 kuwekwa katika bajeti ya manispaa kwa ajili ya kuandaa ilani ya uchaguzi wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, hali ambayo ilisababisha mvutano mkali kwa madiwani wa CHADEMA na CCM.

Mvutano huo wa madiwani baina ya pande mbili ulisababisha baadhi ya madiwani kuchana hansard za bajeti wakidai kuwa bajeti ni ya kihuni na isiyokuwa na masilahi kwa ajili ya wananchi kuweza kupata maendeleo.


Habari hii ni kutoka gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa CHADEMA wamuumbua Nape

Inasikitisha sana, aliyetoa taarifa hii ni mbabaishaji wa kutupa na inashangaza CDM wamemuamini vipi aende kujibu hoja nzito ya mshahara mnono wa Slaa! Kwamba amepewa mshahara mzuri kwa kuwa ali-sacrifice ubunge akijua wazi kuwa angeshinda akaenda kwenye Urais ambao alijua wazi kabisa angeshindwa! Na kweli akashindwa, sasa chama kinamlipa fadhila na kum-compensate malipo yanayofanana na Ubunge! Shame on him...anajipambanua na kutaka kuwashawishi watu kuwa ni mpenda haki na usawa huku aki-negotiate apewe mshahara mzuri kwa kuwa amepoteza ubunge na marupurupu yake kwa kukibeba chama - he is trying to portray a picture of a fighter with a higher up cause kumbe he does not even believe in the cause per se, and nevertheless what he is fighting for! This is very low! He is nothing but a mere hypocrite, soon Tanzanians who had started to believe in him would know him in his true colours and forget all about him!
 
kazi ipo. Ulinzi wa Mkurugenzi milioni 95.

Hivi kweli ufisadi tanzania utakwisha kweli?

Wananchi kazi kwenu
 
Mbunge Kigwangala;vipi hatujasikia lolote hadi sasa kuhusu maandamano yako ya kudai maslahi bora kwa wana Nzega kuhusu yale machimbo ndani ya jimbo lako badala yake tukajionea wenyewe wananchi walipokuzomea kwa kuleta wajenzi ya nyumba yako Nzega toka nje ya jimbo lako!!Maandamano hayo yapo au hayapo tena Mbunge?

By the way kulipwa milion 7 Dr Slaa au zaidi ya milion 11 anayolipwa katibu wa CCM-Mukama ndiyo chanzo cha wana Nzega kukosa maji salama,kukosa huduma za afya na kukosekana kwa huduma zote za kijamii kwenye jimbo lako??
 
Bora noma na iwe noma

mmesahau kuna kabinti alikuwa anakifwata fwata sana pale kimara bucha akawa anakitumia kuwapa vijana kumi kumi ili waipigie ccm ukifika bucha unaingia kulia kama umetokea ubungo ukiulza kwa mama joji mbele yake kuna nyumba moja ya kupangisha imejaa mabinti na vijan wa mjini..akawa anakuja usiku loh jamaa alipomwagawa kwenye ubunge na binti akammwaga fyaaaa mpaka leo hii ukimuuliza binti anasema mi nasoma nykati we mapenzi gani ya lindi sijui newala na dar...pole sana kijana unatakiwa ukipenda usitangaze vyeo vyako wanwake wengi sasa wako kimaslahi wako kwenye ujasiriamali ndoa baadae....sijajua kama ana ndoa huyu kijana ila tulikuwa tunafurah sana maana akiondoka kale kabinti asbh kanaita watu wanagawiwa nyekundu kama anavyogawa 500 ..nilikuwa namhurumia sijui alikuwa na mategemeo kweli kabisa vijana wangeipigia ccm na hakika tumekura za ccm sisemi uongo mafuta ya kumi kumi ayakuwa yanaoiga chenga....asitutibue tkam letea na vyuoni atahama chama
 
inasikitisha sana, aliyetoa taarifa hii ni mbabaishaji wa kutupa na inashangaza cdm wamemuamini vipi aende kujibu hoja nzito ya mshahara mnono wa slaa! Kwamba amepewa mshahara mzuri kwa kuwa ali-sacrifice ubunge akijua wazi kuwa angeshinda akaenda kwenye uraiA ambao alijua wazi kabisa Ungeshindwa! Na kweli akashindwa, sasa chama kinamlipa fadhila na kum-compensate malipo yanayofanana na ubunge! Shame on him...anajipambanua na kutaka kuwashawishi watu kuwa ni mpenda haki na usawa huku aki-negotiate apewe mshahara mzuri kwa kuwa amepoteza ubunge na marupurupu yake kwa kukibeba chama - he is trying to portray a picture of a fighter with a higher up cause kumbe he does not even believe in the cause per se, and nevertheless what he is fighting for! This is very low! He is nothing but a mere hypocrite, soon tanzanians who had started to believe in him would know him in his true colours and forget all about him!


mheshimiwa embu tusaidie
binafsi sikujua uraia unagawiwa ccm na unarudishwa na ccm
embu tuweke bayana hivi yule kijana aliekupita kwenye kugombea ubunge anaitwa bashe...hivi mlimuondoolea uraia kwa muda tena bila aibu ya mavi mwenyekiti wako akadai si raiA alafu leo hii ndio anaongoza kamati ya mapinduzi uvccm
unaweza kutusaidia huko ccm nguvu za kuvua na kumvalisha uraia gafla zinatokea wapi ana kuna ofisi za immigration umo ndani??tusaidien tusiiende kujazana folen pale posta kumbe kuna sub immg office pale lumumba mtatusaidia na hope akuna rushwa kama immigration yenyewe

na kama amerudi kuwa mtanzania huoni hiyo nafasi yako ya ubunge ni batili na kafiri na uitaji kuitwa mheshimiwa kama mheshimiwa

tatu kuna unafiki uliingilia wa wale jamaa wa migodi binafsi nilijua unatafuta jina nikamwambia nduguyako mmoja subiri nyakati zinasema na kweli makelele yameisha unaweza kutuambia huko ccm kuna chuo cha wanafiki na sie labda tunaweza kuwa trainning na kutoka sikumoja???

Kwako mheshimiwa wa nzega
 
Hii ni namna ya takwimu na uchambuzi tunaohitaji kupewa na viongozi wetu walioko madarakani.
Sio kusema tu nakanusha, au naunga mkono hoja. Ukiona maelezo yanaendana na hali halisi au yanakaribiana na ukweli halisi ni rahisi kukubalika.
Hongera Malando na Prof Safari kwa ufafanuzi ulio wazi
 
inasikitisha sana, aliyetoa taarifa hii ni mbabaishaji wa kutupa na inashangaza cdm wamemuamini vipi aende kujibu hoja nzito ya mshahara mnono wa slaa! Kwamba amepewa mshahara mzuri kwa kuwa ali-sacrifice ubunge akijua wazi kuwa angeshinda akaenda kwenye urais ambao alijua wazi kabisa angeshindwa! Na kweli akashindwa, sasa chama kinamlipa fadhila na kum-compensate malipo yanayofanana na ubunge! Shame on him...anajipambanua na kutaka kuwashawishi watu kuwa ni mpenda haki na usawa huku aki-negotiate apewe mshahara mzuri kwa kuwa amepoteza ubunge na marupurupu yake kwa kukibeba chama - he is trying to portray a picture of a fighter with a higher up cause kumbe he does not even believe in the cause per se, and nevertheless what he is fighting for! This is very low! He is nothing but a mere hypocrite, soon tanzanians who had started to believe in him would know him in his true colours and forget all about him!

acha porojo, tangu uchukue jimbo hakuna chochote ulichojitahidi kuanza kukifanya, barabara mbovu, umeme hakuna, hospitali ya ndala hakuna umeme wagonjwa wanapata tabu. Utakiona 2015! Sio mbali baba
 
Dogo amekwishaanza kupumulia mashine bado kidogo atapumzika milele

Halafu ana kikuku cha shingo,

2750785.jpg
 
Bw. HK heshima kwako,
Naona umeiwekea hii habari masikio,pua,mikono ili upate maana unayotaka wewe. Umekwisha ambiwa Dr. Slaa hakuomba wala kushinikiza alipwe mshahara huo wa 7.2, bali wao CHADEMA waliona anastahili alipwe hivyo. Shida hapo ni huelewi au unapiga siasa au unataka kupotosha?

Watu wenye kufanya kazi kisayansi huweka malengo na viwango ili vifikiwe katika muda fulani. Baadaye wanafanya tathmini kisha matokeo....sasa kama katika appraisal yao CHADEMA waliona utumishi uliotukuka kwa Dr. Slaa je sio sahihi kumtuza (reward) kwa mkataba bora zaidi?

Nijuavyo mimi, hapo Tz kuna watu wengi sana wangejitolea na watajitolea kulipa mshahara wa Dr. Slaa ukitaka, then kama hiyo (mshahara wa Dr. Slaa) ndio hoja yenu yenye turufu mmefiliska sana na hamna uhalali wa kuendelea kuongoza WaTz kuwapeleka kusikojulikana?
 
kwani mwenyekiti wa ccm, JK, mshahara wake na maslahi yake mengine yapo vipi? je safari zake za chama zanalipwa na serikali au chama? Je safari zake za nje ya kwenda mapumzikoni na kuatalii zinaigharimu nchi kiasi gani?...
 
Inashangaza ...kumbe Nape ni mamluki ndani ya CCM? Chadema walimkataa kwa sababu ya kuhusika kwake na EPA, Jamaa akataka kuanzisha chama chake cha CCJ.....CCM wakamziba, sasa amerudi CCM ili kuimaliza kwa sababu za hasira yake kukosa CCJ....CCM wawe macho....Jamaa hatari.........watanzania tuwe macho na blah blah za Nape....anatudanga CCM wamejua gamba wakati Nape ndo gamba lenyewe...Anazunguka kupiga blah blah kumbe mshahara wa U-DC anautia ndani......siku hizi naona anatembea V8 eti?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom