Marando na Prof Safari nao wamcharaza Nape ile mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marando na Prof Safari nao wamcharaza Nape ile mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 12, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wakati makamanda wakuu wako huko kusini wakiendelea na ile ‘twanga kote kote' nasikiavyo hapa Dar makamanda wengine – Mabere Marando na Prof Safari le wametema cheche kali – pande zote mbili wakimjia juu yule dogo wa CCM – Nape – kwa harakati zake za kujaribu kuisafisha CCM kwa usanii tu.

  Nasikiavyo hawa wa Dar wamechakaza kabisa Nape kwa kumuelezea kwamba haiwezi kazi hiyo aliyopewa kwani naye ni fisadi mkubwa – akihusishwa na kufaidika na hela za EPA za Jeetu Patel.

  Marando anapoeleza waliofaidika na hela za EPA ni authority tosha kwani yeye anajua maana anamtetea Jeetu. Anamtetea Jeetu kwa sababu msimamo wa huyu mdosi ni kwamba hakurudisha hela za EPA, anashikilia kwamba nyingi ya hela alizokwapua walichukuwa CCM wenyewe – akiwemo Nape (na JK wake) etc etc.

  Nadhani haya yote yatawekwa hadharani kesi ikifikia mahala husika.

  Mimi hayo yote nimeyasikia kwa swahiba wangu ambaye ni ripota wa gazeti moja aliyekuwapo kwenye hiyo briefing ya akina Marando. Mwenye habari kamili atusaidie kuongezea hapa, au kurekebisha.
   
 2. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aangalie contempt of court
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nape hafai kabisa kutembeza bendera ya CCM. Anasahau kwamba naye anaishi katika nyumba ya kiyoo.

  Isitoshe -- ni mtu wa visasi. Hivi JK hana mtu mwingine credible? Haoni kama hii vita ni ya kufa na kupona.
   
 4. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Makamba kashindwa , je huyu ambaye bado anatongotongo za ujana , yeye akiwa UVCCM alifanya nini cha maana mpaka ashindane na Babayake Bigwa wa Mabomu teketezi dhidi ya Wavua Gamba (CCM) Lakini hata hivy inzi kufia kwenye kidonda ni halali yake naye atakufa na CCM na Mafisadi wakiwemo
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Yani nape bora hata makamba mkubwa. Anajua wapi kaongeza chumvi, na akichemsha anasawazisha na 'vifungu'. Huyu dogo mang'aa tu
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Kipigo hicho anakistahili dogo maana amejisahau.

  Ni huyu huyu alikuwa akimshutumu sana JK kwa kushindwa kuongoza CCM mpaka inatekwa na mafisadi. Ni huyu huyu aliingia katika deal ya kujiunga na Chadema kwa sharti la kuachiwa jimbo la Ubungo ili Mnyika afanye kazi za chama.

  Ninapomuona anawasema Chadema simuelewi.

  Yeye apambane na mafisadi wa chama chake aachane na Chadema.

  Ufisadi ndani ya CCM na serikali yake ni hatari kuliko "ufisadi" wa Chadema wa kumlipa Dr. Slaa shilingi milioni saba kwa mwezi.
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  yangu macho na masikio
  ila tumwache nape afanye kazi aliyotumwa
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nchi hii hakuna kitu kama hicho. Pinda aliwahi kusema Bungeni kwamba viongozi wa chadema wana hatia katika yale maandamano ya Arusha -- wakati kesi iko mahakamani.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Namhurumia nape atazeeka haraka sana kwani amepewa mzigo mzito sasa ambao hawezi kuubeba kwa namna yoyote tena kwa kutumia hoja dhaifu dhidi ya chadema...........kwanza anaropoka tu ili mradi kuwagiribu akili watz kitu ambacho hakiwezekani...............km chadema mafisadi na yey nape,kikwete na ccm yao inavyombo vyote vya dola na intelijensia yenye uwezo mdogo wa kuzuia maandamano tu inakuwaje wameshinwa vp muda wote kuwakamata?......nchi hii tukiendelea kuzaa na kuwalea watu ili waje kuwa wanafiki km akina mukama na nape basi hatutakuja kujikwamua hata kidogo...........hawa ccm,nape,kikwete na magamba mengine waendelee tu kuishukuru chadema kwa kuwaonesha nia mpaka kwa aibu wanadai kujivua magamba na kubaki na sumu ileile na utumbo uleule na hoja dhaifu zielzile zizlizopitwa na wakati.... Akina nape...................ccm iliishakosa sifa ya kuwa watetezi wa watz kwa kuamua kwa makusudi kujigawia miongoni mwao mali za nchi..............kikwete akiwa kinara wa kuanzisha makampuni feki akishirikiana kwa karibu na maswaiba wake wakuu akina rostam na loowasa
   
 10. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Marksman, JK atapata wapi wa kumtuma kwani katika Sisiem yooote, huyo Nape pamoja na uvundo woote alionao, ndo anaonekana mwenye nafuu, lakini wengine wakifugua vinywa vyao-watachafua hali ya hewa Sisiem!

  Kumbuka mwaka fulani Sofia Simba alishawahi kusema kwenye vikao vyao kuwa; ...kama wakianza kuumbuana (CCM) hakuna msafi...! "Wooote maji ga nyanja", wameoza wananuka rushwa Mwl. alisema!
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nape hana hoja, mbona wabunge la JMT wanalipwa zaidi ya 12mil kwa mwezi ukijumlisha nahela ya mfuko wa jimbo? Ina maana bunge nalo linafanya ufisadi kuliko wa CHADEMA!

  Kijana hayuko serious kuvamia maji bila kujali kina chake! Alianza vizuri lakini anataka kumaliza vibaya!
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nape ni mchafu na akizidi kulopoka hovyo tutamuanika hadharani; kwa kuanzia tu huyu kijana aseme hela za harusi yake zilifadhiliwa na nani kabla ya kuondoka kwenda India mara tu Kikwete aliposhinda uchaguzi?
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mungu bariki hii hali ya kisiasa iendelee kuwa hivi hivi....
  Mh jamani huko jikoni kwa mkuu wa kaya hali nimbaya zaidi ya tunavyojadili.
  Hata Nape mwenyewe shahidi, anachofanya ni kujaribu kuokoa ambacho hata yeye naamini tena kama anauwezo wa kuokoa.
  kwanza pamoja na kujikakamua kote, Jk kamuacha peke yake tena kwani haitaki tena vita na mapacha 3 (wimbo wa kujivua gamba) sababu hawezi ku-bare consequences zake kama na wao walivyomuonyeshea kwamba wanauwezo w kumwaga mboga.
  So, wote tunaona nafasi ya Nape.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mabere aangalie asije kuharibu kesi tu mahakamani kama kweli ikithibitika amesema hayo.
   
 15. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu dogo ni limbukeni. anajipeleka mbele mbele kama mnyama nyumbu bila kujua anachofanya. Agenda ya ufisadi imeishia wapi?? makelele meeeeeeeeeengi yasiyo kuwa na maana wala tija, zaidi ya kujimaliza tu.
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nimewahi kueleza kwamba CCM wana tatizo la ki-historia. Historia iliwapumbaza wakabaki na viongozi wenye ufahamu mdogo wakati ufahamu wa wananchi wengi wa TZ ukipanda.

  Kumbukeni siasa za CCM hazikuhitaji ufahamu. zilihitaji ujasili au kukosa aibu tu! Kidumu chama .........................., CCM hoyeeee..........!, nk. ni maneno ambayo hayakuwa na maana yoyote ya ubora wa chama au nchi. Wachache, akina Nyerere walibaki na ufahamu na wakafa nao.

  CCM wamejikuta bado wana kundi la watu wa aina hiyo. Wengi wenye ufahamu wako upande wa pili. Vyuo vikuu au elimu ya juu hawaoni sifa ya kuwa na CCM, Huko vijijini pia vijana wa fomu 4, ufahamu na umri wao uko nje ya CCM.

  Wapo akina Nape. Hawa ndo wanaoonekana wana ka-uwezo ka kuweza hata kubofya na kuingia kwenye internet. Yuko juu ki-chama lakini ukimuangalia ufahamu wa mambo ya Dunia, mambo si mazuri kwake. Bahati mbaya kwake itakuwa kama atadhani anajuwa.

  Muangalie katibu mkuu, Mukama. Kweli anaweza akakusimulia muelekeo wa kisiasa Duniani? Nchini je? Ninachokiona kwa Mukama ni elimu ya nadhalia aliyoisoma hapo zamani za kale kwa bahati mbaya anadhani bado ina matumizi miaka hii ya .com.

  Naona kama anasahau hata majukumu ya kazi yake kama alivyokuwa Makamba kuwa kundi moja na akina Tambwe.
   
 17. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hawa wanasiasa wapya wa JK wavalishwe nappy kwanza. Mukama karopoka eti Chadema kilianzishwa kwa shinikizo la IMF!!!!!!!!! Naivity in the extreme.

  Ni kweli muasisi wa CDM, Edwin Mtei, alitofautiana na Nyerere juu ya sera za uchumi baada ya vita vya Nduli Idi Amin, akajiuzulu. Tz ilipokumbatia siasa za vyama vingi na CDM kuanzishwa, hata Nyerere mwenyewe alikiri CHADEMA ndicho chama kilichokuwa na sera ambazo zingeweza kuwa m'badala wa zile za CCM. Sera za CDM toka mwanzo zilitamka zitazingatia uhuru wa soko na udhibiti wa raslimali za nchi yetu kwa manufaa ya waTz.

  Nina hakika Muasisi wa CCM na Baba wa Taifa angekuwa hai leo, sio kwamba angejivua gamba, bali angeungana na CDM na kuondoka katika Chama cha Mafisadi. Wakati wa uhai wake alipata kutamka kwamba "CCM si mama yangu", na angeweza kukiacha.
   
 18. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  makamba aliaga kwa kusema naenda waandalia makazi, huyu makamba alishatofautiana na nape huko nyuma. inawezekana nape ni kati ya watu waaoandaliwa makazi na makamba. meaning that amewekwa mtegoni.
   
 19. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, hajawahi kuomba wala kushinikiza alipwe mshahara mnono.

  Badala yake, chama hicho ndicho kilimshinikiza na kumwomba kimlipe vizuri, chini kidogo ya maslahi ya Mbunge, kwa kuthamini mchango wake katika uchaguzi mkuu uliopita, hasa ikizingatiwa kuwa kama angegombea ubunge angeshinda, lakini alikubali ombi la chama la kugombea urais, ambao alishinda akachakachuliwa.

  Chama hicho kimesema kitaendelea kuenzi mchango wa Dk Slaa kwa kumwezesha ipasavyo ili asitetereke katika kukiongoza CHADEMA kwenye harakati na mapambano ya kukiondoa CCM madarakani miaka minne ijayo.

  Malezo hayo yalitolewa jana na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa CHADEMA, Anthony Komu, alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam.

  Komu alikuwa ameita vyombo vya habari kuzungumzia alichokiita porojo za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama, ambao wameamua "kujilipua" kwa kuwatetea mafisadi wakubwa ndani ya chama kw akigezo cha kujivua gamba.

  Alisema kinachowauma CCM ni kwamba wanatambua kwamba Dk. Slaa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe wakiendelea kusitawi, ndiyo mwisho wa utawala wa CCM.

  Komu alisema kauli za viongozi wa CCM wanaotapatapa haziwezi kukinusuru chama hicho tawala, na haziwezi kukizuia CHADEMA kufanya kazi yake ya kuwatumikia wananchi kwa kuwaamsha dhidi ya watawala wabovu.

  Alisema kauli za Nape ni propaganda zisizo ma mashiko, ambazo Watanzania watazipuuza, kwa sababu wanajua kazi nzuri iliyofanywa na Dk Slaa na wenzake wakiwa Bungeni, wakati wa uchaguzi na sasa katika operesheni inayoendelea kuamsha wananchi juu ya haki zao na wajibu wa serikali.

  Alisema kauli za Nape hazitapunguza kasi ya CHADEMA kupambana na mafisadi, kwani haziwezi kupunguza ugumu wa maisha ya Watanzania, wala hazitaweza kudhibiti mipango mkakati ya chama hicho.

  Kwa nyakati tofauti, Mukama na Nape wamekaririwa wakiwashutumua viongozi wakuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, kwa maelezo kuwa wameshnikiza mshahara mkubwa wa Sh milioni 7.5 kwa Dk Slaa, na uuzaji wa magari matatu ya Mbowe kwa pesa nyingi mno.

  Komu jana alisema kwanza Mukama na Nape wanapotosha umma kuhusu ukweli wanaoujadili, na akasema hata hiyo sehemu ya ukweli wanaougeuza tuhuma imeshapitwa na wakati, kwa kuwa CHADEMA hakifanyi mambo kwa kificho, na kilishafafanua hoja hizo.

  Alisema Dk. Slaa hajawahi kushinikizwa alipwe Sh.7.5 milioni. "Kwanza, hatumlipi kiasi hicho, lakini pia Dk. Slaa hajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka kuaminisha umma," alisema Komu.

  Badala yake, alisema, chama ndicho kilipanga jinsi ya kumwezesha Dk Slaa kwa kuwa ndicho kilichomwomba agombee urais, huku kikujua kuwa angegombea ubunge na kushinda kirahisi.

  Lengo la chama kufanya vile ni kumwezesha Dk Slaa kutenda vema kazi zake za katibu mkuu kama alivyokuwa akitenda kazi za ubunge; hivyo kwa pamoja wakakubaliana awezeshwe kulingana na masharti ya utumishi katika nafasi ya ubunge.

  Huku akikosoa takwimu za Nape, Komu alisema Dk. Slaa analipwa Sh 7,174,000 kama kwa mwezi, na si Sh. 7,500,000.

  Alisema vilivyochukuliwa vipengele vichache sana katika marupurupu ya mbunge, hivyo si sahihi kusema kuwa Dk. Slaa alipwa sawa na mbunge.

  Mkurugenzi huo yalisema vipengele hivyo ni mshahara wake Sh. 1,725,000, wakati mbunge analipwa Sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.

  Komu alisema kiongozi huyo analipwa mafuta ya kwenda ofisini na kurudi nyumbani kwake lita 30 kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi; kwa bei ya kila lita moja Sh. 2000.

  Wakati mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi kwa bei ya kila lita moja Sh. 2,500, bei ambayo haipo, lakini Bunge limeridhia kulipa.

  Alisema sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka pendekezo hilo katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu kupitishwa kwa njia ya uwazi na likaingizwa katika mpango kazi wa chama.

  "Wakati wote wa kujadili pendekezo hilo, Dk. Slaa aliachia nafasi yake na kikao kiliendeshwa na katibu wa Wanawake, Dk. Naomi Kaihula, ambaye ni mbunge wa Viti Maalum kutoka Mbeya," ilisema.

  Alisema mbunge akikaa katika kikao cha Kamati ya Bunge au akihudhuria mkutano wa Bunge analipwa Sh. 70,000 kama posho ya kikao, Sh. 30,000 posho ya mafuta na Sh. 80,000 posho ya kujikumu akiwa Dodoma.

  Na akiwa Dar es Salaam, mbunge analipwa Sh. 50,000 kama posho ya mafuta, Sh. 70,000 posho ya kikao na Sh. 80,000 kama posho ya kujikimu huku fedha hizo zikilipwa bila kujali kama mbunge huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na amekwenda nalo Dodoma.

  Akahoji: "Mbona hakuna mtu alishawahi kuuliza wakati hizo zote ni fedha za umma?"

  Alihitimisha kwamba Dk. Slaa anastahili kulipwa kiasi hicho kwa kuwa aliombwa na chama kugombea urais, naye kukubali, zaidi kukubaliwa na umma pamoja na wanachama kutokana na ukweli wake katika kazi ya siasa.

  "Baada ya kukubaliwa na umma, alionyesha umakini, umahiri na uwezo wa hali ya juu katika kujenga hoja zenye tija kwa taifa, na kwamba Dk. Slaa alithibitisha na bado anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni kiongozi bora na shupavu anayestahili kulipwa mshahara mzuri," alisema Komu.

  Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo Dk. Slaa alikuwa mgombea wao wa urais yanathibitisha kuwa hata bila kuzingatia uchakachuaji wa kura, ameanzisha ukurasa mpya wa mwisho wa mwanzo wa zama za mwisho wa CCM.

  Akifafanua kuhusu tuhuma za Mbowe kuhusu kuuzia chama magari chakavu, alisema CHADEMA ndiyo iliomba kuuziwa hicho wanachoita "magari chakavu."
  Alisema hayo si magari ya kawaida na hayawezi kufananishwa kwa kiwango chochote na magari ya FUSO yanayotembea mitaani, na kwamba hiyo ni mitambo maalumu ya uenezi wa siasa.

  Alisema katika magari hayo kuna vipaza sauti vyenye thamani ya dola za Marekani 148,000 sawa na Sh. milioni 222, jenereta tatu zilizonunuliwa kwa Sh. milioni 47 kwa kila gari kwamba yana bodi maalumu yenye uwezo wa kubeba watu wasiopungua 12.

  Pia alisema magari hayo kila moja lina uwezo wa kubeba mapipa ya mafuta ya helikopta, jukwaa la kuhutubia na vifaa vya matangazo ambavyo vyote vimejengwa kwa Sh. milioni 48.4.

  Alisema Mbowe aliombwa, na kamati kuu iliunda kamati ya watu wanne chini ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mohammed Issa kumwomba akiachie chama mitambo hiyo baada ya majadiliano marefu.

  Wajumbe wengine wa Kamati hiyo, waliobariki kuwa ni Mabere Marando, Mkurugenzi wa Rasilimali, Suzan Lyimo (MB) na Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

  Aidha Komu alisema dai la CHADEMA kwamba inanunua magari chakavu si jipya kwao, kwani inao uwezo mdogo wa kifedha na kwamba imezoea kununua magari chakavu siku zote Japani na Uarabuni.

  "Kwanza magari yanayozungumziwa chakavu yamenunuliwa nje na kuanzia kazi CHADEMA mpaka leo, na hayajawahi kutumiwa na Mbowe," alisema
  Alisema kama CHADEMA imeweza kuweka wazi hoja walizozielekeza kwao, ni vema na wao wakawaeleza Watanzania fedha walizozitumia katika uchaguzi mkuu na mshahara wa Katibu Mkuu wao Mukama, badala ya kukwepa hoja za msingi.

  "Tunasisitiza kuwa CHADEMA imeweka wazi malipo ya viongozi wake, gharama za uchaguzi na vyanzo vyake vya mapato na jinsi inavyotumia mapato yake...tunaitaka CCM nayo iweke wazi malipo ya viongozi wake wakuu, gharama za uchaguzi na vyanzo vya mapato yake," alisema.

  Alisisitiza kwamba CCM ni chama cha kifisadi kwa kuwa viongozi wake ni mafisadi, wanafiki na wasio wa kweli kwa kuwa walikiri wenyewe katika hicho wanachoita kujivua gamba kuwa katika siku 90 wanachana na mafisadi.

  Alisema CHADEMA wanataka kuona hilo likifanyika bila visingizio na kuelekeza mashambulizi kwa Nape hana hadhi ya kuinyoshe akidole chama kwa kuwa si mtu makini mwenye agenda kwa watanzania.

  Na kwamba Nape anatakiwa kuonwa na watanzania ama kuitwa vuvuzela anayecheza ngoma asiyoijua na kwamba ni mnafiki, mzushi na mtu asiye na msimamo.

  Komu alisema CHADEMA inao ushahidi wa kutosha kuwa ni mmoja wa watu walionufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia kwa kwa Jeetu Patel ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya kamati ya rais kwamba alitumia fedha hizo katika kampeni zake.

  Komu alisema hivi sasa Nape analipwa mshahara wa ukuu wa wilaya na huku akilipwa na CCM na kutumia fedha za serikali kufanya kazi za CCM.

  Alienda mbali zaidi na kusema kwamba baada ya kushindwa kupata nafasi ya kugombea Ubunge kupitia CCM aliomba agombee kupitia CHADEMA akakataliwa kwa kuwa hakuwa na sifa za kumzidi John Mnyika.

  Mbali na hilo alisema pia ni mmoja wa waasisi wa chama cha CCJ na kuhoji iweje leo awe na ubavu wa kuionyeshea kidole CHADEMA?

  Aidha alisema yeye (Nape) ndiye aliyetumwa CCM kuiwakilisha katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA 2010 na kukisifia chama hicho: "CHADEMA inaenda vizuri kama taasisi na kwa hoja."

  Katika hatua nyingine madiwani wa CHADEMA katika manispaa ya Kinondoni wanatarajia kuuelezea umma sababu ya kuibuka kwa vurugu katika baraza la bajeti la 2011/ 2012 lililoketi hivi karibuni.

  Licha ya kuuelezea umma pia wanajipanga kutoa tamko juu ya kukiukwa kwa sheria na kanuni na baraza hilo kuamua kupitisha bajeti isiyokuwa na tija kwa wananchi.

  Wakizungumza jana na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema kuwa umma unapaswa kufahamu yale yaliyojitokeza ndani ya baraza hilo ambapo bila kuweka jitihada za pamoja kuna uwezekano kata zinazoshikiliwa na wapinzani kushindwa kupata maendeleo.

  Diwani wa Saranga Ephraim Kinyafu alisema kuwa bajeti hiyo imejaa uozo huku wakiacha kuweka kipaumbele katika masuala ya maendeleo.

  Alisema ili kuondoa dhana ya madiwani wa chadema ni wakorofi suala hilo linatarajiwa kufikisha kwa wananchi na kuwafafanulia suala la milioni 95 kutumika kwa ajili ya ulinzi wa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

  "Hata kama wameipitisha bajeti hiyo…tunaamini wananchi watakuwa waamuzi wetu tutawafahamisha sababu za sisi kuipinga bajeti maana haiwezekani mavazi ya madiwani yatengewe sh milioni 100 hizo fedha ni nyingi zipoelekwe katika miradi ya maendeleo," alisema.

  Alieleza kuwa iwapo manispaa hiyo ingeweza kuongozwa na chama hicho basi wanahakiki wangepiga hatua kubwa katika maendeleo kuliko ilivyo hivi sasa masuala ya anasa yanapewa kipaumbele.

  Alifafanua kuwa imeshangaza kuona kuwa kata kubwa kama ya ubungo kushindwa kupewa miradi jambo ambalo linaashiria kuwa viongozi wa eneo hilo waonekane kwa wananchi kuwa hawawezi kuwajibika.

  Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kawe, Esther Samanya alisema kuwa si kwamba madiwani walipanga kufanya vurugu bali walikuwa wakipigania maendeleo kwani haifurahishi kuona thamani za ofisi zikitengewa fedha huku miradi ya maendeleo ikipewa kisogo.

  Alisema pamoja na kujitokeza kwa masuala hayo bado madiwani wa chama hicho wamepanga kutoa tamko na kupinga bajeti hiyo ambayo haina tija kwa wananchi.

  "Hivi kweli viongozi makini wanaweza kuacha kuwapigania wananchi na wakasimama kwa ajili ya kutetea watumishi wa idara ambapo wanalipiwa maji na umeme wakati jukumu hilo si la manispaa,"alihoji.

  Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/ 2012 ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilielezwa kuwa ya kifisadi, hali iliyosababisha kutokea kwa vurugu baada ya madiwani wa CHADEMA kuamua kuipinga.

  Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya siku tano vya kamati za kudumu za madiwani wa Manispaa ya Kinondoni lakini katika hatua ya upitishaji wa bajeti hiyo, mabishano makali yaliibuka baada ya madiwani wa CHADEMA kuipinga bajeti hiyo wakieleza kuwa vipaumbele havijazingatiwa kwenye baadhi ya kata, huku wale wa CCM ambao ni wengi wakiiunga mkono.

  Madiwani hao wa CHADEMA pia walihoji kiasi cha zaidi ya sh milioni 44 kuwekwa katika bajeti ya manispaa kwa ajili ya kuandaa ilani ya uchaguzi wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, hali ambayo ilisababisha mvutano mkali kwa madiwani wa CHADEMA na CCM.

  Mvutano huo wa madiwani baina ya pande mbili ulisababisha baadhi ya madiwani kuchana hansard za bajeti wakidai kuwa bajeti ni ya kihuni na isiyokuwa na masilahi kwa ajili ya wananchi kuweza kupata maendeleo.


  Habari hii ni kutoka gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa CHADEMA wamuumbua Nape
   
 20. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Prof safari na Marando hawa jajibu hoja ya Nape kuhusu Dr Slaa kulamba 12m kama wabunge wakati yeye mwenyewe alishasema wabunge wanalipwa hela nyingi!
   
Loading...