Marais wengine wanaweza kuiga alichofanya Rais Magufuli

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Na Joshua M Mwakalukwa

Kinachojadiliwa sasa sio chochote bali, ushindi Tanzania ilioupata, unaweza igwa na maraisi wengine, Hofu imetanda kwa wawekezaji kwenye sector ya Madini

Ukisoma report ya leo Oct 25 na Reuters, yenye kichwa cha habari "Barrick Gold's Tanzania deal may set expensive precedent - shareholders"

Utaona wazi kabisa, hawajadili tena yale tuliyokuwa tunayasikia kutoka kwa yule mwanasheria kuwa tutashitakiwa, bali ni hofu ya ushindi tulioupata na matokeo yake!

Inasema, Baadhi ya wawelezaji wanawalaumu Barrick Gold Kwa kukubali matakwa ya Raisi wa Tanzania JPM, kwani inaweza kuwatia moyo nchi nyingine wenyeji kutaka mgao mkubwa kutoka kwa wachimbaji
Wakielezea wasiwasi wao wawekezaji wengi wiki hii wamesema kwa kukubali kuwapa Tanzania 50% ya "Economic Benefits" kwenye Migodi mitata ya Accacia, Barrick wanaweza kuwa wameset baseline ambayo nchi nyingine watataka kupata kutoka kwa Makampuni ya uchimbaji madini, na kitu kitakacho sababisha kuponguza kasi ya kuendeleza machimbo

Msemaji wa Barrick Andy Lloyd anasisitiza kuwa "Huku sio kuwapa tu bure, ni kufuata matakwa ya sheria"

Msemaji huyo wa Barrick anasema " Wao, Barrick wanaamini kuwa washirika na serekali utawapa matokeo mazuri na endelevu kwa wanahisa"

Wanaisa wengine wa Barrick wameonyesha kuwa bado wanaimani na kampuni yao katika maamuzi haya.

Wanaisa wengine wamesema sasa ni wakati wa kuzoea kukutana na matakwa kama hayo kutoka kwa nchi wenyeji.

Dan Denbow, ambaye ni senior portfolio manager at USAA Investments wamiliki wengine wa share ndani ya Barrick anasema "kutoa zaidi ya 40% hadi 50% si kitu cha ajabu"

Jisomee mwenyewe hapa;
Barrick Gold's Tanzania deal may set expensive precedent - shareholders

MPONGEZE JPM, JEMBE LETU, MAANA FAIDA HII SIO YETU PEKE YETU NI KWA WOOTE WANAOKANDAMIZWA NA WAWEKEZAJI WANYONYAJI KAMA ACCACIA.
[HASHTAG]#Watamuelewa[/HASHTAG] tu.
 
Wewe nani aige...??
Labda kama kuna anayetaka kuiminya Demokrasia sawa, jamaa ni mfano wa kutosha.
Tofauti na hapo hakuna cha kuiga
 
Nikisoma mazuri yanayoongelewa juu ya JPM.. yaani roho inafurahia na kuzidi kunipa motisha wa kulishangilia lori lake zaidi na zaidi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom