Elections 2010 Marais wastaafu waogopa kumkampenia JK?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wana-JF:

Gazeti moja liitwalo Tahmini leo lina stori kuu ukurasa wa mbele kwamba marais wastahafu -- Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa wamekacha kumkampenia JK, kwa sababu wanaogopa kuumbuliwa na masuala ya ufisadi.

Hili gazeti, ambaloi hutoka kila Jumatatu nimelipenda sana na linakuja juu sana siku hizi kwani haliko katika class ya HOJA, TAZAMA, SAUTI YA UMMA, MTANZANIA, CHANGAMOTO, RAI au TAIFA TANZANIA yanayomilikwa au kufadhiliwa na mafisadi. TATHMINI ni gazeti linaloandika mambo objectively ambayo yanareflect hali halisi ya kisiasa ya nchi hii, siyo majungu au kupakana matope.
 
Kwani ni lazima marais wastahafu wampigie kampeni JK? Wameamua kukaa kimya kwa sababu wameona mgombea wao anakubalika kwa wananchi bila matatizo yeyote
 
Hawaogopi kuhojiwa kwa mambo ya ufisadi tu bali hata baadhi ya madhambi yao. Nina uhakika siku Mkapa akisimama na nkuingia kwenye kampeni, mtaona vyombo watakaloandika. Kiwira coal mines, na wizi mwingine aliofanya!!!!! JK, Mgonjwa wetu hauziki. :A S 100:
 
Wanaona ni dhambi kubwa sana kumkampenia urais mtu wanayeona no dhaifu kabisa kiuongoza na alafu hawako tayari watz tuendelee kuongozwa na rais ambaye ana afya ya mgogoro kwani wakifanaya hivyo watakuwa wanavunja katiba ambayo inasisitiza afya ya kiongozi wa nchi............wamefanya vyema..
kwani ni lazima marais wastahafu wampigie kampeni jk? Wameamua kukaa kimya kwa sababu wameona mgombea wao anakubalika kwa wananchi bila matatizo yeyote
 
Siku Mkapa akisimama atawakumbusha wananchi mambo ya Kiwira na wapinzani watapata hoja nyingine ya ziada.
 
Wameona ni busara kukaa kimya bse Mwinyi alishawai kumponda na Ben anaogopa madhambi yake ya Kiwila,mahotel watu wanaweza yaaaaaaanika bure
 
wanaona kikwete habebeki tena waacha afie mbali huko.........
Wameona ni busara kukaa kimya bse Mwinyi alishawai kumponda na Ben anaogopa madhambi yake ya Kiwila,mahotel watu wanaweza yaaaaaaanika bure
 
Wameona ni busara kukaa kimya bse Mwinyi alishawai kumponda na Ben anaogopa madhambi yake ya Kiwila,mahotel watu wanaweza yaaaaaaanika bure

Maraisi wastaafu wanasoma na kutafakari mchakato mzima wa uchaguzi,labada watajitokeza saa za majeruhi.Lakini inawezekana hawakualikwa kumpigia kampeini kwa sababu labda ya tofauti zao binafsi na mgombea wa chama chao.Isitoshe Kampeini meneja BW Kinana anaweza asiwahitaji kwani wanaweza wakawa mtaji hafifu kwa kipindi hiki.
 
Mbona walikuwapo Jangwani siku ya mdondoko?walialikwa bwana au mdondoko umewatisha nini?
 
Wana-JF:

Gazeti moja liitwalo Tahmini leo lina stori kuu ukurasa wa mbele kwamba marais wastahafu -- Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa wamekacha kumkampenia JK, kwa sababu wanaogopa kuumbuliwa na masuala ya ufisadi.

Hili gazeti, ambaloi hutoka kila Jumatatu nimelipenda sana na linakuja juu sana siku hizi kwani haliko katika class ya HOJA, TAZAMA, SAUTI YA UMMA, MTANZANIA, CHANGAMOTO, RAI au TAIFA TANZANIA yanayomilikwa au kufadhiliwa na mafisadi. TATHMINI ni gazeti linaloandika mambo objectively ambayo yanareflect hali halisi ya kisiasa ya nchi hii, siyo majungu au kupakana matope.

Unamjua mmiliki wake lakini au unasema tu?
 
Tathmini na Tazama ni mama mmoja tumbo mbalimbali, kama hujui hilo. 2 X 2 = 10 VERY GOOD!!! NOW YOU'VE GOT THE ANSWER!
 
Walau mzee Mkapa alishasema hataki tena habari za kujihusisha na siasa. Mwacheni apumzike!
 
Kwani ni lazima marais wastahafu wampigie kampeni JK? Wameamua kukaa kimya kwa sababu wameona mgombea wao anakubalika kwa wananchi bila matatizo yeyote

Angelikuwa anakubalika mabango yaliyojaa hadi kuelekea misalani ni ya nini, kama anakubalika hivyo kuna haja gani ya kupotumia mabilioni ya fedha kwa matangazo na mabango? Acheni urongo wenu. CCM maji yako shingoni. Washukuru mtandao walioujenga waasisi wa chama cha TANU ndio unawasaidia vinginevyo wangehenya mwaka huu na mgombea wao!
 
Na kule Bagamoyo pia anakubalika sana ila kwengine hakubaliki

Nasikia kuna mama alikuwa kwenye coaster ya M/sho - B/Moyo alishindwa kujizuia baada ya kuona bango kubwa la picha ya JK pale kona ya Kunduchi na kusema "Mwangalie kama mtu vile"
 
tehetehe alipatwa na msiba gani huyo mama hadi aseme hivyo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom