Marais wastaafu wa Tanzania Mkapa na Kikwete kushiriki mazishi ya Daniel Arap Moi leo

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,790
4,428
MARAIS wastaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ni miongoni mwa wageni mashuhuri, watakaoshiriki mazishi ya kitaifa ya Rais wa zamani wa Kenya, Daniel Arap Moi, yakayofanyika nchini humo leo.

Serikali ya Kenya imetenga siku ya leo kuwa ya mapumziko, ili kuwapa nafasi Wakenya wengi, kushiriki mazishi hayo ya kitaifa, ambapo ibada ya mazishi itafanyika Uwanja wa Michezo wa Nyayo uliopo mkabala na Barabara ya Uhuru jijini Nairobi.

Mkapa na Kikwete wataungana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, viongozi wengine wa nchi hiyo na kutoka mataifa mbalimbali kushiriki mazishi hayo ya kitaifa. Hayati Mzee Moi aliyefariki dunia mwanzoni mwa wiki hii, akiwa na umri wa miaka 95.

Atazikwa rasmi nyumbani kwake eneo la Kabarak Kaunti ya Nakuru kesho. Kabarak ipo kilometa 220 kutoka jiji la Nairobi.

Moi alitawala Kenya kwa miaka 24 kutoka mwaka 1978 hadi mwaka 2002 na alifariki Februari 4, mwaka huu.Wakati wa uongozi wake, falsafa yake maarufu ilikuwa ni Nyayo, ambayo misingi yake ni amani, upendo na umoja. Kila mahali alikokwenda alikuwa akibeba kirungu, ambacho kilikuwa kama ndicho kitambulisho chake.

Wakati huohuo, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Kikwete, wamesema Rais huyo wa zamani wa Kenya, Moi, alisaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa tena kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya sasa.

Viongozi hao waalisema hayo wakati walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti na vyombo vya habari vya Kenya, kuhusu kifo cha Rais huyo wa pili wa Kenya, aliyechukua madaraka baada ya kifo cha Rais wa kwanza, Mzee Jomo Kenyatta, mwaka 1978. Kikwete alisema Mzee Moi alikuwa na shauku kubwa ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo, baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977.

Kwamba katika kipindi chote hicho, alikuwa akitafuta namna bora ya kushirikiana na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Ali Hassan Mwinyi.

“Wakati nilipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika kipindi cha Rais Benjamin Mkapa ndipo juhudi zilizoongozwa na Rais Moi, zilipamba moto za kuirudisha Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyokufa mwaka 1977,” alisema.

Kikwete alisema baada ya Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995 na kumchagua yeye kama Waziri wa Mambo ya Nje, waliamua kuunga mkono azma ya Rais Moi ya kuirudisha jumuiya hiyo, iliyokuwa na nchi tatu wanachama, ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda, ambapo mwaka 1999 lengo hilo lilitimia.

Aidha, Kikwete alisema Mzee Moi alichangia kwa kiasi kikubwa, kuleta amani katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwamo Kenya yenyewe, Uganda, Burundi na Rwanda.

Alisema kiongozi huyo wakati wa uhai wake, pia aliimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya na mataifa mengine kwa ujumla.

Kikwete alimtaja Mzee Moi, kama mpenda maendeleo ya kikanda, kutokana na hatua yake ya kuunga mkono ushirikiano wa uzalishaji wa umeme wa pamoja na Tanzania, kutokana na gesi asilia ya Songosongo, inayopatikana Kusini mwa Tanzania.

“Niliagizwa na Rais wangu Mkapa nije kwa Rais Moi nimweleze kama atakuwa tayari kujiunga na Tanzania katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia. Kwa bahati nzuri Mzee Moi alikubali na kumuagiza Waziri wa Mafuta na Madini, Kyaro,” aliongeza Kikwete.

Alisema katika kuyafanyia kazi mawazo ya Rais Moi na Mkapa, walianza kukaa vikao vya kujadili mradi huo na kikao cha kwanza kilifanyika katika mji wa Mombasa.

Rais Museveni alisema Mzee Moi alikuwa mkereketwa wa muungano wa nchi za Afrika Mashariki, baada ya jumuiya hiyo kuvunjika kwa mara ya kwanza mwaka 1977.

“Alikuwa anatamani jumuiya yetu ya Afrika Mashariki ifikie hadhi ya kuwa shirikisho haraka, akiamini kuwa itakuwa ni mwisho wa matatizo ya kisiasa yaliyokuwa yakisumbua baadhi ya nchi za jumuiya hiyo,” alisema Rais Museveni.
 
Kushindwa kuhudhuria Rais wetu na yeye kujikita katika uzinduzi wa jengo ni aibu kubwa sana sana.
Hivi tuna nini sisi na huyu Rais hadi analiaibisha taifa namna hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Chakaza naamini alitaka kushiriki ila kuna Wanahabari BBC, Aljazeera ..nk ..huko angeulizwa maswali asiyokuwa na majibu..

Ni vigumu kujenga hoja za uongo kwa lugha usiyoimudu..

Jiwe alikua hana namna zaidi ya kuingia chaka.
 
Mkuu Chakaza naamini alitaka kushiriki ila kuna Wanahabari BBC, Aljazeera ..nk ..huko angeulizwa maswali asiyokuwa na majibu..

Ni vigumu kujenga hoja za uongo kwa lugha usiyoimudu..

Jiwe alikua hana namna zaidi ya kuingia chaka.
Kwani wakati wakimuhoji si angevaa king'amuzi masikioni m
 
  • Kicheko
Reactions: prs
Kwani wakati wakimuhoji si angevaa king'amuzi masikioni m
Tatizo ni Majibu ya Maswali..Kwani M7 si aliwahi kumtafsiria na bado akashindwa kujibu swali!.:D
Haha do you love kolapshen ..
 
Moi alikuwa kiongozi katika nchi waanzilishi wa EAC. Rais wetu kutoungana na viongozi wenzake wakuu waanzilishi wa jumuia, haileti picha nzuri katika jicho la diplomasia.

Anyway, kila mmoja na hekima yake. RIP Moi. Umejaliwa miaka si haba ya kuishi Duniani. Nina imani uliitumia vema zawadi hii uliyopewa na Muumba wetu. Basi akujalie pumziko la milele pamoja na wateule wake.
 
Sijaelewa! Mara atazikwa leo mara mbele nakutana na neno "atazikwa rasmi kesho"!
 
Mkuu Chakaza naamini alitaka kushiriki ila kuna Wanahabari BBC, Aljazeera ..nk ..huko angeulizwa maswali asiyokuwa na majibu..

Ni vigumu kujenga hoja za uongo kwa lugha usiyoimudu..

Jiwe alikua hana namna zaidi ya kuingia chaka.
Sasa atakimbia mpaka lini masikini!? Mambo yakikuzidi mtu si unaachia wengine? Unang'ang'ania ya nini madaraka usiyo yaweza? Au mke anakushinikiza? Ndugu na jamaa? Au mganga wa kienyeji?
Tunachoka sana jamani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Chakaza naamini alitaka kushiriki ila kuna Wanahabari BBC, Aljazeera ..nk ..huko angeulizwa maswali asiyokuwa na majibu..

Ni vigumu kujenga hoja za uongo kwa lugha usiyoimudu..

Jiwe alikua hana namna zaidi ya kuingia chaka.
Hakuna rais anayehojiwa kwa kusthukizwa, Kuna itifaki maalum
 
Back
Top Bottom