VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi, hakuwahi kutembelea Ikulu kwenda ima kumpongeza au kuzungumza na Rais Magufuli. Lakini, Marais wastaafu Mkapa na Kikwete wa awamu ya tatu na ya nne wamekuwa wakienda Ikulu mara kwa mara.
Kwenda Ikulu kwa wastaafu kuna tafsiri yake. Wachambuzi wa kisiasa wanaziona ziara hizo kama ni kwenda 'kumwelekeza' Rais cha kufanya kwenye teuzi na mchakato wake wa kutumbua majipu. Kwenda Ikulu ni kumbana na kumwingilia Rais,wanasema wachambuzi wa kisiasa.
Nani asiyejua kuwa Rais Magufuli analazimika kuwaheshimu na kuwasikiliza waliomtangulia? Atakataaje ushauri wa Mzee Mkapa au Mzee Kikwete? Akikubali ushauri wao,wakiwa si washauri wake rasmi, si kuwafanya watoaushauri kuwa waamuzi?
Mzee Mwinyi anajua kuwa zama zake zimepita. Anamwacha wa zama hizi kujidai kiutawala na kiuamuzi. Hataki kutafsiriwa vibaya. Ni Mzee Mwinyi tu ndiye yuko sahihi kujitenga na tafsiri zisizo vutizi. Hongera Mzee Ruksa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam