Marais wapya wanatoa wapi mfumo mkali wa harufu ya rushwa kutoka kwa mabosi wao wa zamani?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Viongozi wa Afrika Kuna sehemu wanakwama katika utendaji wa kazi zao. Inawezekana si wakweli na wazalendo au Kama ni wakweli na wazalendo Basi tafsiri ya uzalendo inapaswa kutafsiriwa upya.

Kiongozi anaishi ndani ya Baraza la Waziri, anaishi Ikulu na anakuwa karibu sana na mtangulizi wake lakini umsikii akilalamika au kushauri baadhi ya miradi ichunguzwe au kuhoji uhalili wa miradi anayoona ina mianya ya rushwa. Kila kitu kinaonekana kinakwenda sawa na akihojiwa anaeleza kila kitu kipo sawa.

Akiingia Kushika dola kwa nafasi ya Urais sehemu ya Kwanza utamsikia akielekeza flani akamatwe, flan achukuliwe hatua na kadhalika kwa madai miradi waliyosimamia inanuka rushwa. Je hii harufu ya rushwa ambayo ukiwa wazir uisikii unaisikiaje ukiwa Rais? Au hii harufu inatokea Ikulu? Kwann hao wanaowafukiza hii harufu ya rushwa wasitumbuliwe Kwanza kwa kutowafukiza watangulizi wenu hadi rasilimali za nchi zinatumika vibaya?

Au hii harufu ya rushwa ni mgongo wakupitia kuwachafulia CV walio chini yenu ionekane Kuna kazi inafanyika? Kwanini hii harufu ya rushwa haiwagusi Mawaziri na Manaibu Waziri inawagusa watumishi wa Umma tu ambao bosi wao ni Waziri?
 
Nilipokuwa waziri nilijichukulia nyumba za NHC na nyengine nilihonga kwa demu wangu, Raisi wangu alikuwa anachukuwa na kugawa miradi ya serikali kwa mabepar na mabeberu.
 
Back
Top Bottom