Marais Waliomfuatia Mzee Karume Zanzibar Wote Wabovu: Shamsi Nahodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marais Waliomfuatia Mzee Karume Zanzibar Wote Wabovu: Shamsi Nahodha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Nov 3, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, amesema rekodi ya miaka minane ya uongozi wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume katika utendaji kazi hakuna kiongozi yoyote aliyeweza kuivunja hadi sasa.
  Nahodha aliyasema hayo juzi wakati akifunga Kongamano la wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar lililokuwa likizungumzia kuwaenzi waasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
  Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar na ambalo lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, kwa kuwashirikisha Wasomi wa Vyuo Vya Zanzibar.
  Vyuo vilivyoshiriki Kongamano hilo ni Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar, (ZJMMC), SUZA, Chuo Cha Ualimu Benjamin Mkapa na Nkurumah, Chuo Cha Kiislamu Zanzibar na Pemba na Chuo cha Afya. Vyengine ni Chuo Cha Utalii, Chuo cha Utumishi Zanzibar, Chuo cha Ufundi, Mbweni, Mikunguni, Chuo Cha Waandishi wa Habari cha CCM na Chuo cha Fedha cha Chwaka .
  Alisema, wasomi wa vyuo vya elimu ya juu wanapaswa kuona elimu wanayoipata baada ya kumaliza masomo yao wanaifanyia kazi vilivyo ili waweze kuwa na rekodi ilioachwa na Muasisi wa Taifa la Zanzibar, Mzee Abeid Amani Karume, kwani hakuna kiongozi yoyote katika kipindi cha miaka minane aliyeifikia.
  Alisema haiwezekani kwa vijana wa sasa wakaamua kuanzisha utaratibu wa kumuenzi Mzee Karume wakati wakiwa wanashindwa kuliwajibikia taifa lao vizuri jambo ambalo litakuwa ni sawa na kumkebehi kiongozi huyo. Alisema Rais Karume katika utawala wake alijali zaidi kuwasaidia wanyonge katika kipindi kifupi cha utumishi wake kwa kwa kuwapatia ardhi ya kilimo eka tatu tatu huku akiwajengea makaazi bora .
  "Nilikuwa nasikia akitoka nyumbani kwake wakati nyumba za Michenzani zikijengwa lazima apitie hapo kuangalia maendeleo yake na akirudi haendi nyumbani kwake hadi apitie hapo. Amekufa ameyaacha majumba machache ambayo serikali hii imeamua kuyamalizia " alisema Nahodha.
  Alisema kuwa aina ya uongozi kama huo hivi sasa unakosekana; kwani viongozi wengi wanasema wasiyoyafanyia kazi na kutenda wasiyoyasema. "Karume alikuwa ni msikivu ambaye ni jasiri wa kusikiliza watu kwa kuangalia yale yenye mustakbali wa nchi hii; tena alikuwa mfuatiliaji mambo; jambo ambalo halipo kwa viongozi wa sasa. Unaweza kuwa na viongozi 20; lakini, hakuna hata mmoja ambaye amejijengea sifa za aina hiyo" alisema Nahodha.
  Ili kuweza kuwaenzi kivitendo viongozi hao ni vyema kwa vijana wa sasa kufuata utumishi wa kiongozi ndio utumishi bora ambao vijana na wasomi watapaswa kuufuata ikiwa ni moja na njia kuu ya kuwaenzi viongozi hao.
  Akimzungumzia Mwalimu Nyerere, alisema alipenda kujituma pamoja na kupenda nchi yake; jambo ambalo vijana wanapaswa kujifunza. Alisema haitawezekana kumuenzi Mwalimu Nyerere ikiwa wataacha kudumisha amani ya nchi kwani haitawezekana kuwa na umoja bila ya amani.
  Akizungumzia Muungano, Nahodha alisema kuwa Serikali itahakikisha inafanya kila njia kutimiza ahadi zake za kutatua kero za Muungano . "Ni wajibu wa kutekeleza kila jambo ambalo liliasisiwa na viongozi wetu kwani waliusia wajadili Muungano; lakini, wasiuvunje kwa kufanya kila njia kuona tunaudumisha" alisema Nahodha.
  "Kama kuna wakati wa kuwapa uongozi vijana ni huu ili wazee waweze kuwaonya na tukisubiri wakosolewe ni nani atakaeifanya kazi hiyo wakati huyo ni mzee kwani sio sahihi kumpa mtu uongozi ambaye akitaka kukosolewa aseme hapana kwa kutumia mfano wa zamani" alisema Nahodha.
  Alisema kinadharia umri unaozidi miaka 40 mara nyingi unatumika kutoa busara na hekima na vijana ndio mara nyingi huweza kufanya vyema ikiwa atapewa nafasi ya kuutumikia ngazi ya uongozi kwa vile bado nguvu hazijamwishia.
  Alisema serikali itafikiria njia za kuwainua zaidi vijana kimaslahi kwa kuanzisha mifuko ya uwezeshaji kwa vijana ambapo hivi sasa tayari imekuwa ikitoa mikopo kwa wananchi kupiti mfuko wa AK na JK.
  Mapema Waziri wa Kazi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Asha Abdalla Juma alisema Wizara yake itahakikisha inaendeleza vijana kwa kuona fursa za ajira zinashikkwa na wazanzibari katika soko la sekt binafsi.
  source: zanzibar yetu web blog
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  He He he he he he he he he!!!!!!!!!!!
  Hapa anazungumza na watu wenye vichwa vyao, akikutana na vichwa maji waliokunywa maji ya bendera na chanikiwichi atawaambia tu...rais fulani alikuwa "karume mdogo" na huyu wa sasa "ndo simba mtoto"...ameshatekeleza ilani ya CCM kwa 100% na kama Nahodha hatoona haya wala kujuwa vibaya atafika mbali akiwaambia vichwa maji hawa kuwa wanaonaje kama "karume mtoto" huyu ataongezwa term nyingine, kama vile "komandoo wa kidombo", alivyotaka kufanya...wananchi watakubali tu....lakini si kizazi hichi cha sasa cha vijana wasomi ambao kwa saivi Zanzibar ndo asilimilia kubwa ya wapiga kura...na wanategemewa katika uchaguzi wa 2015 kuwa asilimia karihu 80%,ambao wana mawazo ya kimabadiliko kuliko hali ilivyokuwa chaguzi zilizotangulia,si muda mrefu hata chembe...zanzibar tutaona mabadiliko ya system..anaekataa na akatae dalili ndo mnaziona hizo...wanakiri wenyewe mbele ya wenye akili zao kuwa tokea Mzee Karume aondoke(ASP) na kuja CCM hakuna la maaana lililofanywa na waliomfuatia...hata huyu mwanawe pia kashindwa.Hongera Nahodha kwa kusema kweli
   
 3. c

  chimbondi JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2014
  Joined: Dec 16, 2013
  Messages: 380
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  kweli huyu ni Nahodha anatoa ukweli wote huyu si sisiem ni cuf
  mbona anatuvua nguo?\
   
 4. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2014
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mpenda makuu anajisema mwenyewe
   
Loading...