Marais wa Afrika wanapokewa vipi Ulaya na America

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Hivi jamani naomba kuuliza'hivi hawa marais wetu wa Africa wanapokewa vipi waendapo kikazi Ulaya na America?

Au waendapo kwenye hizi nchi tajiri duniani mfano Marekani, uk, Canada, France, Japani, Germany, Denmark, Spain, na hata China.

Je,wanapokelewaje pale airport za nchi hizo?

Na je,ulinzi unakuwa wa hali ya juu?

Maana tumezoea kuona marais au mawaziri wakuu wa hizo nchi nilizozitaja hapo juu kama wanakuja Bongo na nchi zingine za Afrika kama Tanzania basi utakuta au utaona Marais wetu wanaenda kuwapokea pale airport kwa mizinga na magwaride na ulinzi unakuwa wa hali ya juu kiasi kwamba sometimes mitandao ya simu huwa wanaiblock kuzunguka eneo lote la airport na maeneo yaliyojirani na eneo hilo.

Baada ya hapo basi msafara wa mapikipiki na magari huanza kuelekea ikulu njia ikiwa nyeupeeeee hata sisimizi hakuna achilia mbali magari! na ole wako ukatishe na kigari chako' chamoto utakiona.

Na wakishafika huko Ikulu ya magogoni basi vyakula vyao hupimwa na madaktari wao kabla ya kuvila,na wakisema walale hapa Bongo kwa siku kadhaa, basi ulinzi atakaopewa huyo mgeni ni wakufa mtu kwenye hiyo hotel atakayofikia.

Ndiyo maana leo nawauliza magreat thinkers wenzangu wa JF.

Je hivi maraisi wetu wa Afrika akiwemo Rais Kikwete anapokwenda kikazi Uk au Marekani' je huwa anapokelewa kuanzia pale airport?

1. Huwa anapokewa na Rais au PM wa nchi hiyo husika?

2.Anakagua gwaride na kupigiwa mizinga mfano wa Bongo?

3.Escort za mapikipiki na magari yaendayo kwa kasi huwepo?

4.Huwa ali chakula hadi daktari wake athibitishe ubora na usalama wa chakula?

5.Hapo airport simu huwa hazifanyikazi mfano wa Bongo?

6.Analala nyumbani kwa balozi au five stars hotel? Na ulinzi wa usiku unakuwaje? Nakaribisha mgongano wa kimawazo na wa kimtazamo.

Ahsanteni!
 
Mzee Mwanakijiji hupo? wadau wengine mpooooo? haya nasubiri manews ya majibu toka kwenu
 
Hakuna hata anayewajua huko, wanapokelewa na mabalozi wao na hawana ulinzi wowote zaidi ya wale mgambo wanaotoka nao bongo,hawawezi kufunga mtaa kwa masaa kumi kama wanavyowafanyia huko na kukimbizana kama wanafukuza kibaka
 
Kwanza huwa wanafika kama wezi tu, hata kwenye vyombo vya habari hawatangazi ila kama ni Mtanzania basi utapata news kutoka kwa watz wenzako tu au social networks za home.
 
Kwanza huwa wanafika kama wezi tu, hata kwenye vyombo vya habari hawatangazi ila kama ni Mtanzania basi utapata news kutoka kwa watz wenzako tu au social networks za home.
Ni kweli, ziara nyingi zinakuwa kama watu wa kawaida tu wanaposafiri, kama wanaaahadi za kukutana na wakuu wa hizo nchi basi ratiba huandaliwa na vyombo vya habari huitwa kwajili ya kutoa taarifa za mwisho.
Tena kunabaadhi husachiwa airport kama wamebeba madawa
 
Kwanza huwa wanafika kama wezi tu, hata kwenye vyombo vya habari hawatangazi ila kama ni Mtanzania basi utapata news kutoka kwa watz wenzako tu au social networks za home.

KWELI KABISA, wakubwa wa ulaya na marekani hawana maslahi nao,bora hata ziara ya nzi kwenye makalio ya ng'ombe inaweza kuvuta attention ya mkia
 
...hupokelewa kama mashoga watarajiwa...
Hivi jamani naomba kuuliza'hivi hawa marais wetu wa Africa wanapokewa vipi
waendapo kikazi Ulaya na America? Au waendapo kwenye hizi nchi tajiri duniani
mfano marekani,uk,canada,france,japani,Germany,Denmark,Spain, na hata China.
Je,wanapokelewaje pale airport za nchi hizo? Na je,ulinzi unakuwa wa hali ya juu?
Maana tumezoea kuona marais au mawaziri wakuu wa hizo nchi nilizozitaja hapo
juu kama wanakuja Bongo na nchi zingine za Africa kama Tanzania'basi utakuta au
utaona Marais wetu wanaenda kuwapokea pale airport kwa mizinga na magwaride
na ulinzi unakuwa wa hali ya juu kiasi kwamba sometime mitandao ya simu huwa
wanaiblock kuzunguka eneo lote la airport na maeneo yaliyojirani na eneo hilo. Baada
ya hapo basi msafara wa mapikipiki na magari huanza kuelekea ikulu njia ikiwa nyeupeeeee hata sisimizi hakuna achilia mbali magari! na ole wako ukatishe na kigari chako' chamoto utakiona!. Na wakishafika huko ikulu ya magogoni basi vya
kula vyao hupimwa na madaktari wao kabla ya kuvila,na wakisema walale hapa Bo
ngo kwa siku kazaa, basi ulinzi atakaopewa huyo mgeni ni wakufa mtu kwenye hiyo hotel atakayofikia.
Ndiyo maana leo nawauliza magreat thinkerz wenzangu wa JF, Je hivi maraisi wetu
wa Africa akiwemo rais Kikwete apokwenda kikazi Uk au Marekani' je huwa anapo
kelewaje kuanzia pale airport?
1. Huwa anapokewa na Rais au PM wa nchi hiyo husika?
2.Anakagua gwaride na kupigiwa mizinga mfano wa Bongo?
3.Escort za mapikipiki na magari yaendayo kwa kasi huwepo?
4.Huwa ali chakula hadi daktari wake athibitishe ubora na usalama wa chakula?
5.Hapo airport simu huwa hazifanyikazi mfano wa Bongo?
6.Analala nyumbani kwa balozi au five stars hotel? Na ulinzi wa usiku unakuwaje?

Nakaribisha mgongano wa kimawazo na wa kimtazamo. Ahsanteni!
 
Back
Top Bottom