Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,947
- 14,391
Ushiriki wa Marais wa nchi za Afrika uliofanyika jiijini ST. Petersburg nchini Urusi si sahihi kuupa sura kuwa Marais hao wamemsusia raisi Putin kama wapinzani wa nje wa Urusi wanavyojaribu kuteka akili za watu.
Jumla ya Marais 17 wameshiriki na wawakilishi wa nchi 47 wameripoti kwenye mkutano huo. Nchi zilizokuwa hazikwenda nyingi zimepeleka wawakilishi wao wa ngazi za juu.
Kunaweza kuwepo na sababu nyengine za Marais wengine kutokwenda wenyewe kama vile za kiusalama wakati nchi hiyo iko kwenye vita. Sababu nyengine pia inawezekana ikawa ni kutojiamini baadhi yao kwenda kinyume na ushawishi wa Marekani na NATO.
Kwa vyovyote itakavyokuwa Marais waliokwenda nao ni Marais na baadhi yao wanaongoza mataifa yenye hadhi ya Kiafrika kuliko hao waliojizuilia kwa sababu zao kwenda kwenye mkutano huo.
Muhimu ni kuwa hata hao walioshiriki wamekwenda na mawazo ya njaa njaa zaidi kuliko ubinadamu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat alisema “The disruptions of energy and grain supplies must end immediately. The grain deal must be extended for the benefit of all the peoples of the world, Africans in particular.”
Raisi wa jamhuri ya Congo Denis Sassou Nguesso naye akasema the African initiative deserves the closest attention “Urgently” for peace.
Kwa upande wake Rais Putin amekubali kuwa Bara la Afrika kwa sasa ni kitovu cha masoko ya bidhaa na linapitia kipindi muhimu cha mageuzi ya kiuchumi na kiutamaduni na kwamba matatizo mengi wanayopata nchi hizo ni zao la vikwazo vya kiuchumi vinavyofanywa na mataifa ya NATO kwa nchi kadhaa duniani.
Baada ya hapo akaahidi kuzifutia madeni nchi hizo na kwamba hazitokosa chakula kama ngano kwani wataendelea kuwasafirishia kupitia njia zao za baharini.
Kinachoshangaza kwa Marais wa Afrika ni hilo ombi lao kuitaka Urusi iendelee na mkataba wa kusafirisha ngano za Ukraine japo kufanya hivyo Urusi imeona hakuna faida kwani kunampa nguvu adui yake kuendeleza vita.
Sasa wao wanataka mwenzao aendeleze mkataba unaoidhuru ili wao tu wapate ngano kutoka Ukraine!
Al-Jazeera